Wazazi Mnaosomesha Watoto Shule za Private jifunzeni kufanya tathmini ya Pesa mnayowekeza katika Elimu hiyo na matokeo yake (Hawatazeekea Nyumbani)?

Elimu ilikuwa Dili Miaka hiyo.

Watu wameshtuka Dili likiwa expired.

Utumie gharama kubwa kusomesha alafu mtoto mwenye degree anashindwa kujiajiri Wala kuajiriwa hizo ni akili matope.
Tatizo pia wazazi hawataki kuwajibika kuwafundisha watoto maadili wakiwa nyumbani. Siku hizi wazazi wamekubali upumbavu wa waalimu kuhakikisha watoto hadi muda wa likizo ni kusoma tu ili kupata ONE kali badala ya muda wa likizo kuutumia kufanya kazi za mikono. Hata majumbani kumewekwa maids kana kwamba ni hotelini badala ya watoto kuwajibika wenyewe. Mtoto mwenye maadili bora na elimu bora hata akijiajiri anatoboa.
 
Ni challenge ametoa ambayo ni kweli. Ila wengi wanaosomesha watoto wao private wanakuwaga pia na uwezo wq kuwekeza kwenye viwanja na mashamba ila huwa hawavifikirii kwa badae. Kwaio wadau kama mtu anaweza wekezeni kwenye viwanja na shule nzuri mpeleke mtoto. Vinasaidia miaka ya mbele
 
Ndugu @Rorscharch nimekuona juha baada ya kuandika kuwa unawekeza kwenye elimu ya watoto ili uje upate faida ya uwekezaji kupitia ajira zao.
Ndugu yangu, mnafarijiana hapa kwa falsafa za kiafrika ambazo hazina tija; Mangi kumfundisha mwanae Biashara ya duka ili aje kufungua yake kamrithisha elimu kubwa kuliko wewe unayechoma 20 M ili mtoto aje kutangatanga mtaani na degree ya sociology
Yaani nimeandika hapo mpaka takwimu za uwezekano wa mtoto kupata ajira baada ya chuo lakini nyie hamuelewi tu; yaani mwanao bila kuwa na connection ya maana basi uwezekano wake wa kupata ajira baada ya kumaliza chuo hauzidi 30% kwa soko letu la ajira
Nachoongelea hapa ni Vipaumbele mkuu, aidha utumie jasho jingi kutupa hela kwenye elimu ya mwanao au tumia pesa kidogo ndani ya utaratibu maalum huku ukihakikisha mpaka anakua mtu mzima basi umemuachia urithi wa kizazi ambao una guarantee ya kukunufaisha wewe, yeye na wajukuu wako
Hatukatai elimu ni ufunguo wa maisha lakini elimu hiyo ianzie katika muktadha ya wewe mzazi kabla haujaiwekeza kwa mwanao ; kama una pesa ya kutosha kusomesha EM na kufanya miradi ya maendeleo at the same time basi good for you brother (you do you!) ila kama wewe ndio mwenzangu na mimi ambaye unajikamua mpaka unatembelea viatu vimetoboka ili mtoto asome EM basi kusema kweli elimu Yako haijakukomboa
 

Itashangaza mzazi aliyesoma kufanya mambo ya namna hiyo.

Hata suala la mtoto kupewa homeworks ati mzazi aje kumsaidia nyumbani kwangu naona ni upuuzi tuu.

Mtoto wa pre unit au Class one unakuta kametoka shule kamefundishwa labda majina ya vitu vya nyumbani kwa kingereza. Daftari linaonyesha amepata Tick lakini ukikauliza hakajui kitu chochote.

Kwenye homework unakuta maswali kalikosahihishwa kwenye daftari yamejirudia kwenye homework lakini hakawezi kuyajibu.

Mtoto Hana Muda WA kupumzika nyumbani
Mtoto Hana Muda WA kupumzika likizo.

Mimi mambo hayo kwa watoto wangu hayatawezekana.

Alafu kwa sehemu kubwa Elimu ni Subject matter based mtoto anakosa ubunifu na uwezo wa KUFIKIRI kwa kina, uwezo mdogo wa kutatua matatizo yake.
Sasa hiyo ndio Elimu gani
 
Ndugu acha kujificha kwenye kichaka cha kurithisha mtoto duka la mangi. Ni wajibu wako mzazi kuhakikisha mtoto anapata elimu bora itakayomsaidia kwenye maisha yake. Na maisha sio kuajiriwa tu. Usipohakikisha anapata elimu bora utaishia kumrithisha hivyo vibiashara vyako vilivyokufanya ukose hata Tsh 1m ya ada. In short utamrithisha umaskini wako. Mzazi makini huhakikisha mtoto anafanya makubwa kuliko yeye. Tatizo ni huu UPUMBAVU wa wazazi kama wewe kudhani mtoto anasoma ili baadae aajiriwe na kuja kumsaidia.
 
Tatizo ni huu UPUMBAVU wa wazazi kama wewe kudhani mtoto anasoma ili baadae aajiriwe na kuja kumsaidia.
Sio aajiriwe kuja kunisaidia bali nimejenga generational wealth (utajiri unaohamia kizazi kimoja kwenda kingine)
Nimetoa hapa mifano ya wahindi pia, alichoanza nacho babu kinakua katika mikono ya mwanae, mwanae naye anamrithisha mikoba mtoto wake na kila hatua inakuja na maendeleo makubwa zaidi
Wakati nyinyi ndugu zangu hapa mnakazana kumkaririsha mtoto tu yale ya darasani afu eti mnaiita hiyo bookish education ndio urithi (hopeless kabisa) wenzenu wahindi na waarabu hiyo elimu ni brush tu ya mtoto kujifunza skills za usimamiaji wa miradi ya familia (urithi ni rasiliamali za familia na sio elimu )
Familia kama za kina Azam, Asas na wengine tutazitoa wapi sisi waafrika kwa mentality ya aina hii; yaani mtoto anasoma akimaliza chuo akaajiriwe huko mbali kabisa na miradi Yako kama mzazi na aanze upya kwenye msoto kama wako; yaani unasomesha mtoto kwa 20M afu adi aje kujitegemea na kazi akapata unakuta uwezo wa kununua hata kiwanja ajibangaize tena miaka 5 tena kwa pesa anayozalisha usishangae akafanya kazi Posta huku anaishia chalinze
Rithisheni watoto mali na Biashara , hivi visingizio vya kusema mnawarithisha elimu ni umaskini tu
 
Tunawapeleka shule za bei sio kwa ishu ya ajira bali ni kutengeneza life connection private Pana watoto wa matajiri,wabunge, foreigners, wafanyabiashara wakubwa so wakikua watapeana connection ya maisha na sio kwamba tunapesa nyingi hapana.
Huku kayumba hata walimu wenyewe wanaowafundisha hao wanafunzi watoto wao hawasomi shule za kayumba.
 
Tunawapeleka shule za bei sio kwa ishu ya ajira bali ni kutengeneza life connection private Pana watoto wa matajiri,wabunge, foreigners, wafanyabiashara wakubwa so wakikua watapeana connection ya maisha na sio kwamba tunapesa nyingi hapana.
Unampeleka mtoto shule ya primary na sekondari private kwajili ya connection ? Hivi unafahamu takwimu ya namna watoto wako wanavyochuja ukaribu na marafiki katika steji moja ya elimu mpaka nyingine? Binafsi naona hii sababu ni ya kujifariji tu na haina uhalisia

1. Urafiki wa Msingi hadi Sekondari: Takriban 30-50% ya marafiki wa shule ya msingi huendelea kuwa marafiki katika sekondari.

2. Urafiki wa Sekondari hadi Chuo: Hii hupungua zaidi, na wastani wa 10-30% tu wa marafiki wa sekondari huendelea kuwa marafiki wa karibu chuoni.

3. Urafiki wa Msingi, Sekondari hadi Chuo: Watu wachache sana (chini ya 5-10%) huweza kudumisha urafiki kutoka shule ya msingi, sekondari, hadi chuo.

Swali: huyu mtoto muda wote huo anasoma umemwambia kwamba umechoma 15+ milioni kwajili ya connection au ndio vile kila kitu kwa kudra za mwenyezi Mungu
 
Msingi ni kumpa vyote elimu bora na mali pia
 
Basi anzia miaka ya 2000 kama itamake sense zaidi au hata 2010
Tuanzie 2010, wapi huko kwenye viwanja million 3 leo ni mamillion hayo unayoyasema?

JE Goba au Mmbweni?, hata huko hakuja fika hayo mamilioni unayoyasema.

Ni wazazi wangapi wanaosomesha million 3 mtoto mmoja ambao hawana uwezo wa kununua Goba hata ya leo, njoo na takwimu.

Japo wewe umesema laki 8 na kwamba mtoto mpaka anamaliza chuo katumia around 20m, ila unasahau gharama za inflation nakadhalika , una assume umechukua 20m ukainunua kiwanja, kumbe ni installation ambazo hata usipo zitoa kwenye shule , unaweza usizi make vile vile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…