OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Unategemea kuajiriwa? Yaani kama leo ajira hakuna, unategemea madogo wa Grade 5 watajuta ajira? Peleka mtoto EM sambamba na Treasury Bond ya 30m kwa 15yrs. Mtaji sio haba
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tatizo pia wazazi hawataki kuwajibika kuwafundisha watoto maadili wakiwa nyumbani. Siku hizi wazazi wamekubali upumbavu wa waalimu kuhakikisha watoto hadi muda wa likizo ni kusoma tu ili kupata ONE kali badala ya muda wa likizo kuutumia kufanya kazi za mikono. Hata majumbani kumewekwa maids kana kwamba ni hotelini badala ya watoto kuwajibika wenyewe. Mtoto mwenye maadili bora na elimu bora hata akijiajiri anatoboa.Elimu ilikuwa Dili Miaka hiyo.
Watu wameshtuka Dili likiwa expired.
Utumie gharama kubwa kusomesha alafu mtoto mwenye degree anashindwa kujiajiri Wala kuajiriwa hizo ni akili matope.
Ndugu yangu, mnafarijiana hapa kwa falsafa za kiafrika ambazo hazina tija; Mangi kumfundisha mwanae Biashara ya duka ili aje kufungua yake kamrithisha elimu kubwa kuliko wewe unayechoma 20 M ili mtoto aje kutangatanga mtaani na degree ya sociologyNdugu @Rorscharch nimekuona juha baada ya kuandika kuwa unawekeza kwenye elimu ya watoto ili uje upate faida ya uwekezaji kupitia ajira zao.
Ila watoto zao hawatawapeleka tena kayumba.Kwani hao watoto ma genius waliosoma Manzese Primary na sasa ni Madaktari bingwa, engineers si walisoma shule zenye mazingira magumu lakini wamefika mbali bila hayo mazingira mazuri
Tatizo pia wazazi hawataki kuwajibika kuwafundisha watoto maadili wakiwa nyumbani. Siku hizi wazazi wamekubali upumbavu wa waalimu kuhakikisha watoto hadi muda wa likizo ni kusoma tu ili kupata ONE kali badala ya muda wa likizo kuutumia kufanya kazi za mikono. Hata majumbani kumewekwa maids kana kwamba ni hotelini badala ya watoto kuwajibika wenyewe. Mtoto mwenye maadili bora na elimu bora hata akijiajiri anatoboa.
Hamna cha BureElimu ni gharama.
Ndugu acha kujificha kwenye kichaka cha kurithisha mtoto duka la mangi. Ni wajibu wako mzazi kuhakikisha mtoto anapata elimu bora itakayomsaidia kwenye maisha yake. Na maisha sio kuajiriwa tu. Usipohakikisha anapata elimu bora utaishia kumrithisha hivyo vibiashara vyako vilivyokufanya ukose hata Tsh 1m ya ada. In short utamrithisha umaskini wako. Mzazi makini huhakikisha mtoto anafanya makubwa kuliko yeye. Tatizo ni huu UPUMBAVU wa wazazi kama wewe kudhani mtoto anasoma ili baadae aajiriwe na kuja kumsaidia.Ndugu yangu, mnafarijiana hapa kwa falsafa za kiafrika ambazo hazina tija; Mangi kumfundisha mwanae Biashara ya duka ili aje kufungua yake kamrithisha elimu kubwa kuliko wewe unayechoma 20 M ili mtoto aje kutangatanga mtaani na degree ya sociology
Yaani nimeandika hapo mpaka takwimu za uwezekano wa mtoto kupata ajira baada ya chuo lakini nyie hamuelewi tu; yaani mwanao bila kuwa na connection ya maana basi uwezekano wake wa kupata ajira baada ya kumaliza chuo hauzidi 30% kwa soko letu la ajira
Nachoongelea hapa ni Vipaumbele mkuu, aidha utumie jasho jingi kutupa hela kwenye elimu ya mwanao au tumia pesa kidogo ndani ya utaratibu maalum huku ukihakikisha mpaka anakua mtu mzima basi umemuachia urithi wa kizazi ambao una guarantee ya kukunufaisha wewe, yeye na wajukuu wako
Hatukatai elimu ni ufunguo wa maisha lakini elimu hiyo ianzie katika muktadha ya wewe mzazi kabla haujaiwekeza kwa mwanao ; kama una pesa ya kutosha kusomesha EM na kufanya miradi ya maendeleo at the same time basi good for you brother (you do you!) ila kama wewe ndio mwenzangu na mimi ambaye unajikamua mpaka unatembelea viatu vimetoboka ili mtoto asome EM basi kusema kweli elimu Yako haijakukomboa
Nakwambia watoto wakikosa Elimu watauza mali utakazowaachia Elimu ndio kila kitu faza fungua kichwa hicho..unataka kudumaza watoto kisa 20m daah.
Mkuu hata sijui wanachotoa maana wakimaliza huko naona wanahangaika na bahasha tu..Kwani shule za serikali ambazo ni bei nafuu huwa hazitoi elimu?
Sio aajiriwe kuja kunisaidia bali nimejenga generational wealth (utajiri unaohamia kizazi kimoja kwenda kingine)Tatizo ni huu UPUMBAVU wa wazazi kama wewe kudhani mtoto anasoma ili baadae aajiriwe na kuja kumsaidia.
Unampeleka mtoto shule ya primary na sekondari private kwajili ya connection ? Hivi unafahamu takwimu ya namna watoto wako wanavyochuja ukaribu na marafiki katika steji moja ya elimu mpaka nyingine? Binafsi naona hii sababu ni ya kujifariji tu na haina uhalisiaTunawapeleka shule za bei sio kwa ishu ya ajira bali ni kutengeneza life connection private Pana watoto wa matajiri,wabunge, foreigners, wafanyabiashara wakubwa so wakikua watapeana connection ya maisha na sio kwamba tunapesa nyingi hapana.
Msingi ni kumpa vyote elimu bora na mali piaUnampeleka mtoto shule ya primary na sekondari private kwajili ya connection ? Hivi unafahamu takwimu ya namna watoto wako wanavyochuja ukaribu na marafiki katika steji moja ya elimu mpaka nyingine? Binafsi naona hii sababu ni ya kujifariji tu na haina uhalisia
1. Urafiki wa Msingi hadi Sekondari: Takriban 30-50% ya marafiki wa shule ya msingi huendelea kuwa marafiki katika sekondari.
2. Urafiki wa Sekondari hadi Chuo: Hii hupungua zaidi, na wastani wa 10-30% tu wa marafiki wa sekondari huendelea kuwa marafiki wa karibu chuoni.
3. Urafiki wa Msingi, Sekondari hadi Chuo: Watu wachache sana (chini ya 5-10%) huweza kudumisha urafiki kutoka shule ya msingi, sekondari, hadi chuo.
Swali: huyu mtoto muda wote huo anasoma umemwambia kwamba umechoma 15+ milioni kwajili ya connection au ndio vile kila kitu kwa kudra za mwenyezi Mungu
Tuanzie 2010, wapi huko kwenye viwanja million 3 leo ni mamillion hayo unayoyasema?Basi anzia miaka ya 2000 kama itamake sense zaidi au hata 2010