Naweza kutabiri unatokea sehemu gani.Watu wa sehemu hii ndio wana IQ ndogo sana
Ndugu yangu mtu hampeleki mtoto wake shule ili akaajiriwe unampeleka mtoto ili aelimike
Nyerere alisema elimu hamfanyi mtu asiwe masikini bali elimu humfanya mtu kujua namna ya kupambana na huo umasikini.
Ingekuwa ni hivyo kina Mo Dewji na Mbowe wasingekuwa na haja ya kwenda kusoma vyuo vikuu vya nje ili hali ukwasi wanao wa kutosha.
Umeshawahi ona mtu tajiri sana na mali nyingi asiye na elimu anavyoishi maisha ya kijima na wasiwasi shauri ya kutokuwa na elimu?.Unakuta mtu ana ngombe zaidi ya 5000 lakini analalia ngozi ya ngombe
Matajiri wakubwa duniani mfano Elon Musk,Bill Gate,Warren Buffet,Aliko Dangote,Marc Zuckeberg umeshawahi kufuatilia ukajua viwango vyao vya elimu?.
Kuna usemi unasema if you thing education is expensive try ignorance.Au kama basi unaona elimu ni gharama sana basi jaribu ujinga uone gharama yake.