Wazazi Mnaosomesha Watoto Shule za Private jifunzeni kufanya tathmini ya Pesa mnayowekeza katika Elimu hiyo na matokeo yake (Hawatazeekea Nyumbani)?

Wazazi Mnaosomesha Watoto Shule za Private jifunzeni kufanya tathmini ya Pesa mnayowekeza katika Elimu hiyo na matokeo yake (Hawatazeekea Nyumbani)?

Mkuu huu ni Mjadala mbona kama umechukia. Changia kwa kujenga sio kususa vile
1. unajua majukumu na wajibu wa mzazi kwa watoto?

2. unajua maana ya msemo jikune unapoweza?

3. unajua maana ya msemo kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake?

kwa uchache ukiyajua hayo unaweza kuwa kwenye nafasi nzuri ya kutathmini hizi mada za kukataa ems kwa kuzipigia chapuo kayumba schools.

note: katafute wimbo wa freddie mcgregor 'to be poor is a crime usikilize wakati ukisoma uzi huu.
 
1. Hatusomeshi watoto ili waje watulipe. Hilo ni jukumu la mzazi kuhakikisha mtoto wake anapata elimu ili awe na tija katika jamii.
Tija gani kwenye jamii wakati mtoto wako umemsomesha kwa milioni 20 sahizi anazunguka mjini na gari za OYA akidaka wadaiwa sugu na degree yake ya sociology huku akiwa analipwa tshs 300,000 kwa mwezi (hana bima wala NSSF)
 
Tija gani kwenye jamii wakati mtoto wako umemsomesha kwa milioni 20 sahizi anazunguka mjini na gari za OYA akidaka wadaiwa sugu na degree yake ya sociology huku akiwa analipwa tshs 300,000 kwa mwezi (hana bima wala NSSF)
Kwa hiyo wote waliosoma kwa million ishirini wanazunguka na Oya na kulipwa 300,000?
 
Somesha unapoweza. 800,000/- kwa mwaka ni hela nyingi kama huna hela. Watu wanasomesha international schools 10+ millions na Bado wananunua viwanja na wanawekeza.
Somesha unapopaweza.
Uhalisia huu naongea kwa watu ambao hawana hela, anayemsomesha mtoto wake 10 M kwa mwaka hiyo sio English Medium mkuu bali ni international school (vitu viwili tofauti)
 
Kwa hiyo wote waliosoma kwa million ishirini wanazunguka na Oya na kulipwa 300,000?
Sekta binafsi sio OYA tu ila asilimia kubwa ukikutana na graduate sekta binafsi basi wewe assume tu analaliwa, ujira wa kuvutia sekta binafsi ni changamoto sana hasahasa katika kampuni ndogo na za size ya kati
 
Yaani unashauri tununue viwanja badala ya kuwapeleka watoto shule haujui kuwa wakikosa Elimu watakuja kuuza hizo mali ulizochuma ili waukesha nyoka tu..
Elimu ndio ufunguo wa vitu vingi sio ajira tu mkuu.
Watakuuziaje mali wakati hela yote ya kuwekeza kwenye hiyo mali ungewekeza kwenye elimu Yao
Na wewe hizo akili za kuuza mali mbona huna wakati umesoma saint kayumba ?
 
Watakuuziaje mali wakati hela yote ya kuwekeza kwenye hiyo mali ungewekeza kwenye elimu Yao
Na wewe hizo akili za kuuza mali mbona huna wakati umesoma saint kayumba ?
Nakwambia watoto wakikosa Elimu watauza mali utakazowaachia Elimu ndio kila kitu faza fungua kichwa hicho..unataka kudumaza watoto kisa 20m daah.
 
unajua maana ya msemo kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake?
Misemo yenu mwingine sio hata ya kuiga wala kuishi ndani yake maana imekaa kimaskini sana ; we unadhani hao wahindi waliotapakaa huko mtaani nao wana mawazo kama haya..... Yaani asomeshe afu ainue mikono kumuachia mola hatma ya mbegu yake mwenyewe?
Wenzenu wanasomesha watoto kimkakati mf. Biashara ya Familia inahitaji mhasibu mwenye vigezo Fulani hivyo Rajit anapelekwa kusoma accountancy (hata nje ya nchi ikiwezekana ) ili akirudi nafasi inayotakiwa kujazwa inajazwa
Wewe hapo unasomesha mtoto afu unamtupia kwenye soko la ajira ambalo hata kwa juhudi zake binafsi uwezekano wa kuajiriwa (tena sio ilimradi ajira bali ajira kweli kweli) unaweza usifike hata 50%
 
Tatizo tumekazania kurithisha watoto elimu afu wanaishia kuja kutumikishwa kwa ujira ambao unaweza usifike hata tshs 500,000 kwa mwezi (yaani umemwaga milioni 20 kwenye elimu ya mwanao afu anaishia kulipwa vichenchi
Tatizo ni mawazo yako finyu kuhusu elimu, wewe umeshikilia hapo kwenye ajira ya serikali tu. Unadhani hizo business unazosema awekeze mzazi, bila ya watoto kuwa na elimu muafaka zitaweza kuendelea? Hayo mapesa atakayoinvest mzee kwenye mashughuli yake yatashughulikiwa na nani?

Hao wanaosomesha kwa gharama kubwa ujue target ya kazi za watoto wao pia kwa asilimia kubwa zinakuwa za kimataifa.
 
Bwana wee! Kabla ya wewe kufanya tathmni. Hata sisi tulishafanya muda sana. Ndio maana tukaja na maamuzi hayo. Wewe ukiona gharama peleka huko kwenye unafuu.

Kila jambo linalofanywa au kutekelezwa lina mipango yake.
Nyie Kila siku ni kuandama wazazi wanaosomesha EM.
 
Nakwambia watoto wakikosa Elimu watauza mali utakazowaachia Elimu ndio kila kitu faza fungua kichwa hicho..unataka kudumaza watoto kisa 20m daah.
Ndugu yangu.... Inakuuma nini wenyewe kuuza hizo mali kama uliwarithisha wewe ukatangulia mbele ya haki? Yaani uwaachie degree uchwala za bongo au uwaachie viwanja vyenye thamani ya mamia ya mamilioni huko goba.... Kipi Bora ?
Yaani umhukumu mwanao na umaskini akawe mwalimu simanjiro huko au bank teller benki ya ualimu eti kisa unaogopa angeuza viwanja vyenye thamani ya milioni 800? Are you serious?
 
Bwana wee! Kabla ya wewe kufanya tathmni. Hata sisi tulishafanya muda sana. Ndio maana tukaja na maamuzi hayo. Wewe ukiona gharama peleka huko kwenye unafuu.

Kila jambo linalofanywa au kutekelezwa lina mipango yake.
Nyie Kila siku ni kuandama wazazi wanaosomesha EM.
Nipe mchanganuo wa hizo tathmini
Najua huna hata picha huyo mtoto wako atasoma nini akifika chuo, nyingi ndio ile sampuli ya "mjomba wako kashauri usomee sheria, kasema ajira zipo za kutosha" miaka 4 baadae unaanza kumuuliza mwanao kama na yeye anakula mchana
 
Shule nyingi za private ndizo zinazozalisha mashoga..kwasababu wanalazimisha kulea watoto wa kiafrika kizungu wakati wazungu walishafeli kwenye malezi...mtoto wa kiume hajawai kufagia shuleni...hajawai kumwagilia maua...hajulawaii kuchoma takataka shuleni...hajawaai kupigana shuleni unakuta shule nzima hakuna watemi..hajawai kutembea hata 1Km kwenda shuleni na kurudi...hajawai kupigwa bakora za matakoni...hajawai kula mihogo na visheti shuleni watoto wanalishwa vyakula vya ajabu mpk wanaota maziwa na wananenepa matako...watoto wa kiume wamelegea kama watoto wa kike....siwezi kumpeleka mwanangu private...kama inshu ni kingereza ni bora nimtafutie tution ya kingereza mengine atayakuta sekondari akifika...wacha hii hela ninunue kiwanja vikawe akimalisha shule atafanya miradi mengine ya maendeleo
 
Naweza kutabiri unatokea sehemu gani.Watu wa sehemu hii ndio wana IQ ndogo sana
Ndugu yangu mtu hampeleki mtoto wake shule ili akaajiriwe unampeleka mtoto ili aelimike
Nyerere alisema elimu hamfanyi mtu asiwe masikini bali elimu humfanya mtu kujua namna ya kupambana na huo umasikini.

Ingekuwa ni hivyo kina Mo Dewji na Mbowe wasingekuwa na haja ya kwenda kusoma vyuo vikuu vya nje ili hali ukwasi wanao wa kutosha.

Umeshawahi ona mtu tajiri sana na mali nyingi asiye na elimu anavyoishi maisha ya kijima na wasiwasi shauri ya kutokuwa na elimu?.Unakuta mtu ana ngombe zaidi ya 5000 lakini analalia ngozi ya ngombe
Matajiri wakubwa duniani mfano Elon Musk,Bill Gate,Warren Buffet,Aliko Dangote,Marc Zuckeberg umeshawahi kufuatilia ukajua viwango vyao vya elimu?.

Kuna usemi unasema if you thing education is expensive try ignorance.Au kama basi unaona elimu ni gharama sana basi jaribu ujinga uone gharama yake.
 
Back
Top Bottom