Wazazi wenye wanafunzi waliofutiwa matokeo ya Darasa la Saba 2022 tukutane hapa tutiane moyo

Wazazi wenye wanafunzi waliofutiwa matokeo ya Darasa la Saba 2022 tukutane hapa tutiane moyo

Nanunua wazo hili..

Shule hizo zimeshafungiwa kuwa exam centers
Serekali haiwezi kosa namna, ili wafanye mitihani yao, kwa sababu kiidadi wanafahamika na pengine wanajulikana kwa idadi,hili litawatuliza wazazi majumbani na kuipenda serekali yao kuona imeona tatizo na inashughulikia.
 
Shule huwa zinafungiwa kwa kipindi fulani, afu zinafunguliwa.
Mwaka huu ndo zimetia fola,shule 24
Alafu ni walimu wa sekondari eti..
Yani wanapewa sh ngapi hadi wahusike ktk hujuma hii!!??
 
Ndugu zangu, usiku wa leo sijalala vizuri, nimefadhaishwa sana na kitendo cha mwanangu wa darasa la saba aliyekuwa anasoma shule ya St Anne Marie academy ya jijini Dar es Salaam kufutiwa matokeo. Yaani nina hasira kali sana kiasi sijajua nichukue hatua gani dhidi ya uongozi wa shule.

Naombeni tushauriane, kama wewe siyo mhanga wa jambo hili unaweza pita kimya kimya tu maana kwa sasa sihitaji kejeli, nahitaji faraja na ushauri.

Hivi mtoto ataenda private? Je, haiwezi kuwa na athari kwenye mitihani ya form four?

Naomba kuwasilisha.
Pole sana,
Ikaumiza.

Mungu awatie nguvu.

Sent from my TECNO CG6 using JamiiForums mobile app
 
Alafu ni walimu wa sekondari eti..
Yani wanapewa sh ngapi hadi wahusike ktk hujuma hii!!??
Wasimamizi saa zingine hawajui mchezo.
Mchezo unafanyika kabla. Na hao wamedakwa kwa sababu ya kukaririshwa, kuwa unakuta darasa zima linakosa swali moja.

Unakuta darasa zima lina andika kitu 1
 
Kwanza kumpeleka Private sio tatizo ila lazima afanye mtihani wa STD 7. Huwezi kufanya mtihani wa Form 2 kama hukufanya mtihani wa STD 7, kwakuwa wamefutiwa matokeo maana yake ni kama hajafanya mtihani sasa.
Mfumo wa sasa hivi mtoto akimaliza STD 7 kuna namba anapewa na ili asajiliwe kufanya mtihani wa Form 2 lazima namba ile utumike, kinyume chake hawezi kamwe.
Wanaokuambia mpeleke tu, wakuambie mwakani wakat anaendelea na huko Secondary basi sharti arudie mtihani wa la Saba, hakuna kona hapo.
Huu mfumo umeanza lini?

Sent from my TECNO CG6 using JamiiForums mobile app
 
Ninachojua NECTA wamefungia kituo cha mitihani (sio shule) fatilia matokeo yake yapo na utayapata.

usipotoshwe humu kwa sasa sajili za wanafunzi zinafanyika kuanzia primary na inahama kila mwaka na hata unapomuhamisha shule ni mfumo sio enzi zetu.

narudia Matokeo ya mwanao yapo na ukifatilia unayapata ni kituo cha mitihani ndicho kimefungiwa (sio shule)
 
Ngoja tuyaone mtandaoni kama yapo....shule yenyewe kaitaja hapo juu

Sent from my SM-T585 using JamiiForums mobile app
 
W
Nitumie namba yako inbox. Nipo naunda group la Whatsapp la wazazi wa watoto wote ambao wamefutiwa matokeo. Tusimame pamoja na kuongea kwa sauti moja
Weka Link tu hapa watajiumga wenyewe.

Hili ni kama janga la kitaifa
 
Hakuna matokeo huyo nae
Hakuna matokeo
Screenshot_20221203-162828.jpg
Screenshot_20221203-162758.jpg

Sent from my SM-T585 using JamiiForums mobile app
 
Ila Mimi kama mwalimu sijaona mantiki ya serikali kuwawajibisha watoto kwa makosa ya wasimamizi wa mitihani pamoja na wamiliki wa shule serikali iangalie namna ya kuwasaidia watoto hawa ikiwezekana warudie kufanya mtihani kwa gharama za waliopelekea kufutiwa matokeo yao.

Poleni sana Wahanga
 
sijasema aangalie mtandaoni lama atakuta *W kwa sababu kituo kimefungiwa

mzazi nenda baraza matokeo ya mwanao yapo tena kwa ukamilifu wake kulingana na alichopata......

humu utapigiwa kelele tu... FATILIA MATOKEO YA MWANAO BARAZA...
 
Back
Top Bottom