Wazazi wenye wanafunzi waliofutiwa matokeo ya Darasa la Saba 2022 tukutane hapa tutiane moyo

Wazazi wenye wanafunzi waliofutiwa matokeo ya Darasa la Saba 2022 tukutane hapa tutiane moyo

Sasa mtashauriana vipi wahanga kwa wahanga.

Pole ila ruhusu na ambao si wahanga wakushauri.
 
Hakuna kitu unachoelewa mkuu jitahidi uulizie kwa watu wanaojua,angalia matokeo ya 2021 ndiyo utaelewa ninachozungumzia
Mwanafunzi ufutiwa matokeo tu endapo yeye kashiriki kwenye udanganyifu yaan amekamatwa na kitu ambacho kinaashiria wizi wa mtihan mfno kushikwa na nondo, kuwa na picha tofauti...

Matokeo hayo yameshikiliwa sioo kufutwa ndo maaan yameandikwaa W*

Fatilia baraza la mitihan pale BAMAGA utapata matokeo ya mwanao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wengi humu wanajifanya wajuaji Sana wakati wanayoyaongea ni uongo.Siku hizi kuanzia shule ya msingi wako kwenye mfumo mmoja wa serikali.Kumhamisha mtoto shule ya private ni lazima kupita ngazi zote kwa mujibu wa serikali,unaanzia shuleni,unaenda kati hadi halimashauri.Nyie mdanganyeni wakati anaomba ushauri.Mifano mnayotoa ni ya Zamani.
Umeishia kulaumu bila kutoa kwa ufasaha nini anatakiwa afanye. Ukiishia kulaumu na kuponda bila kutoa way forward unakuwa huna tofauti na unayemlaumu.
 
Kwanza kumpeleka Private sio tatizo ila lazima afanye mtihani wa STD 7. Huwezi kufanya mtihani wa Form 2 kama hukufanya mtihani wa STD 7, kwakuwa wamefutiwa matokeo maana yake ni kama hajafanya mtihani sasa.
Mfumo wa sasa hivi mtoto akimaliza STD 7 kuna namba anapewa na ili asajiliwe kufanya mtihani wa Form 2 lazima namba ile utumike, kinyume chake hawezi kamwe.
Wanaokuambia mpeleke tu, wakuambie mwakani wakat anaendelea na huko Secondary basi sharti arudie mtihani wa la Saba, hakuna kona hapo.
Umeeleza vizuri sana... Nina swali je kwa sasa hivi ule utaratibu wa mwanafunzi kurudia darasa upo? Yaani kama amefeli au kutofanya mtihani anaweza mwakani akarudia darasa la 7 na mwisho wa mwaka akafanya mitihani?
 
Hapa watu wasikudanganye humu, mifumo ya elimu imebadilika namba aliyofanyia mtihani la 4 itamruhusu afanye mtihani wa la Saba

Na ya la Saba itamruhusu afanye mtihani wa form 2

Na ya form 2 itamruhusu afanye mtihani wa form4 kama akitaka kurndelea six kama atafaulu au chuo hizo namba za form 4 zitamruhusu aenedelee huko hamna mkato. Hapa dogo arudie tu apige Pepa ya std 7
Inaruhusiwa kurudia darasa la 7 mkuu? Utaratibu ukoje?
 
Hakuna uchawi hapo, anaenda sekondari kama kawaida, ishu ingrkuwa sisi ambao tunategemea mtoto afaulu tuuze kuku kumpatia pesa asome sekondari ya serikali
Umewahi kuona mtu yeyote kwa miaka hii miwili hakumaliza la saba na kaenda sekondari? Nijuavyo kwa Sasa ili apande kwenye prems lazima uweke no ya psle.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Poleni sana wakuu

Mimi nashauri ufuate taratibu zitakazotolewa na wizara husika usichukulie poa kabisa. Kabla ya kupiga hatua consult watu wa wizara watakupa muongozo kwa faida ya mwanao baadae.

Pili, nawashauri muifungulie shule mashtaka ya madai, haiwezekani wakawapoteza hivi, tafuteni wakili au mnaweza nipa hii kazi mimi pia, kuna uzembe wa taasisi umewagharimu ninyi na watoto wenu pia. Ipo nafuu Mahakamani ni nyie tu muamue.

Poleni sana. Haya mambo yanafadhaisha,, yana uzi na kukasirisha sana.
 
Umewahi kuona mtu yeyote kwa miaka hii miwili hakumaliza la saba na kaenda sekondari? Nijuavyo kwa Sasa ili apande kwenye prems lazima uweke no ya psle.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
Watu wanachukulia poa cheti/namba ya elimu ya msingi ila hii kitu ina cost sana maana kuna wakati vinatumika kwenye uraia au kujua mtu alipokulia, in short kina mambo mengi nyeti yasiyohusu elimu hata.
 
Wasimamizi hawajui lolote kivipi mkuu!?
wizi wa mitihani wa kutumia wasimamizi ni wakizamani sana na huo sio wizi ni udanganyifu na mara nyingi unatokea ndani ya chumba cha mitihani (lazima ujue tofauti ya wizi na udanganyifu)

udanganyifu hifanywa na vishule vyetu hivi.... wizi wanafanya giants na wana hadi mawakala wa hizo kazi kuanzia mwanzo (maandalizi) ya mtihani hadi mwisho wanajua....

baadhi ya shule ziliyumba baada ya mawakala wao kukamatwa fuatilia utazijua
 
Naungana na serekali kufungia matokeo baadhi ya shule serekali ipo sahihi kabisa uhuni wa shule za binafsi haukubaliki kabisa, maana haiwezekani ndani ya darasa moja, swali la kwanza wanafunzi wote wajaze B, swali la pili wanafunzi wote wajaze C swali la tatu darasa ZIMA wakose, swali la nne wanafunzi wote wapate, alkadhalika hivyo hivyo kwa maswali yote 25. This is evils.
Kama B ndo jibu sahihi wafanyaje?
 
Aisee pole Sana inauma mno ku-invest kwa mtoto ukiamini anapewa elimu Bora kumbe Kuna wengine wanafanya ukora ili waongeze "umaarufu" kwa ajili ya kuwateka wateja...
Mimi nachoweza kusema we muangalie huyo mtoto kwa jicho la huruma n mwanao achana na hao washenzi kikubwa fanya mpango arudi kufanya mtihani wa darasa la Saba ili ndoto yake ya kupata elimu Bora isife....
Kila la kheri mkuu na hamna hatari yyt ile
NECTA mwaka huu hawajarank shule,nadhani Ili kupunguza udanganyifu,Yale mabango kuwa shule imekuwa ya kwanza yatapungua
 
udanganyifu hifanywa na vishule vyetu hivi.... wizi wanafanya giants na wana hadi mawakala wa hizo kazi kuanzia mwanzo (maandalizi) ya mtihani hadi mwisho wanajua....
Duh!!
Kwahiyo unataka kuniambia walipata mitihani kabla wakawapa majibu watoto...
Hili haliwezekani mkuu
 
Duh!!
Kwahiyo unataka kuniambia walipata mitihani kabla wakawapa majibu watoto...
Hili haliwezekani mkuu
hahahhhahaha shauri ako mkuuu ningekupa mifano ya shule chache ila ntazichafua zaidi mana hii nayo ni biashara.
 
Naungana na serekali kufungia matokeo baadhi ya shule serekali ipo sahihi kabisa uhuni wa shule za binafsi haukubaliki kabisa, maana haiwezekani ndani ya darasa moja, swali la kwanza wanafunzi wote wajaze B, swali la pili wanafunzi wote wajaze C swali la tatu darasa ZIMA wakose, swali la nne wanafunzi wote wapate, alkadhalika hivyo hivyo kwa maswali yote 25. This is evils.
Hili tatizo pia linasababishwa na baraza la mitihani. Haiwezekani kabisa utunge mtihani wote maswali yawe ni multiple choices... Ilitakiwa mtihani kama una sections 3 basi multiple choice iwe ni only one section na sections nyingine ziwe ni za kujaza majibu...
 
Back
Top Bottom