Wazazi wenye wanafunzi waliofutiwa matokeo ya Darasa la Saba 2022 tukutane hapa tutiane moyo

Wazazi wenye wanafunzi waliofutiwa matokeo ya Darasa la Saba 2022 tukutane hapa tutiane moyo

Waziri gani huyo?
Ajira kupitia digrii hutaipata bila kuonesha
Cheti Cha la Saba.
Form four.
Form six
Na mwisho cheti Cha digrii

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
Nitajie ajira serikalini ambapo viambanisho ni pamoja na cheti cha std 7... Mimi kwenye faili langu la ajira hakuna hicho cheti.
 
NECTA mwaka huu hawajarank shule,nadhani Ili kupunguza udanganyifu,Yale mabango kuwa shule imekuwa ya kwanza yatapungua
Ni mfumo mzuri sana, ranking inaharibu Elimu. Waende mbali zaidi ya hapo,
 
Duh!!
Kwahiyo unataka kuniambia walipata mitihani kabla wakawapa majibu watoto...
Hili haliwezekani mkuu
Watu wanapewa mtihani kabisa.

Tofauti na hapo ni kuwa watu hufundishwa kujibu hayo maswali, kwa huu mfumo ni ngumu necta kujua uibiaji
 
hahahhhahaha shauri ako mkuuu ningekupa mifano ya shule chache ila ntazichafua zaidi mana hii nayo ni biashara.
We zitaje zijulikane, kama mtu anafanya uharibifu hata akichafuka hakuna ubaya
 
Ndugu zangu, usiku wa leo sijalala vizuri, nimefadhaishwa sana na kitendo cha mwanangu wa darasa la saba aliyekuwa anasoma shule ya St Anne Marie academy ya jijini Dar es Salaam kufutiwa matokeo. Yaani nina hasira kali sana kiasi sijajua nichukue hatua gani dhidi ya uongozi wa shule.

Naombeni tushauriane, kama wewe siyo mhanga wa jambo hili unaweza pita kimya kimya tu maana kwa sasa sihitaji kejeli, nahitaji faraja na ushauri.

Hivi mtoto ataenda private? Je, haiwezi kuwa na athari kwenye mitihani ya form four?

Naomba kuwasilisha.
Taifa kama Taifa la kesho.
Wizara ya Elimu ijitafakari! Ni wakati muafaka kuweka mitaala ya Elimu kuwa na muelekeo wa kuwasaidia Hawa wanafunzi na pia wazazi wanaojitoa sana kutafuta Ada. Uweke mwisho wa siku uje kufuta matokeo?
Inakuwa umeuza mioyo ya wengi sana.
Mwanafunzi awe anatahiniwa kuanzia miaka miwili ya mwisho na pale anapoonekana kurudi Nyuma, mwalimu, mzazi na mwanafunzi wakutanishwe kuona jinsi gani ya kumrejesha kwenye mstari ili mtihani wa mwisho usijekuwa mzigo.
 
Kwanza kumpeleka Private sio tatizo ila lazima afanye mtihani wa STD 7. Huwezi kufanya mtihani wa Form 2 kama hukufanya mtihani wa STD 7, kwakuwa wamefutiwa matokeo maana yake ni kama hajafanya mtihani sasa.
Mfumo wa sasa hivi mtoto akimaliza STD 7 kuna namba anapewa na ili asajiliwe kufanya mtihani wa Form 2 lazima namba ile utumike, kinyume chake hawezi kamwe.
Wanaokuambia mpeleke tu, wakuambie mwakani wakat anaendelea na huko Secondary basi sharti arudie mtihani wa la Saba, hakuna kona hapo.
Naomba kuuliza kma nakupata vizuri, Inamaana kwa mwaka 2023 anaweza kuanza kidato cha kwanza na ikifika muda wa kufanya mtihani wa darasa la saba anafanya ili aipate hiyo Prem namba? Je hiyo Prem namba ya mwaka huo wa 2023 itamruhusu kufanya mtihani wa kidato cha pili kwa 2024?
 
Wezi wa mitihani shule nyingi za private zinaiba mitihani halafu wanalipishwa hela nyingi kisa kuongea kingereza ujinga mtupu
 
Naomba kuuliza kma nakupata vizuri, Inamaana kwa mwaka 2023 anaweza kuanza kidato cha kwanza na ikifika muda wa kufanya mtihani wa darasa la saba anafanya ili aipate hiyo Prem namba? Je hiyo Prem namba ya mwaka huo wa 2023 itamruhusu kufanya mtihani wa kidato cha pili kwa 2024?
Anaruhusiwa kuanza kidato cha kwanza vizur tu, kwa maana mtu anaweza kufanya From 1 and 2 kwa mwaka kama uwezo anao kama ilivyo kwa QT tu
 
Pole sanaa...ila amini kuna mwenye maumivu zaid ya kwako...waka jana kuna shule inaitwa sijui ndo Nyamuge..ipo ilemela kama sikosei...ilifutiwa matokeo...watoto wakahamishiwa vituo vingine....sasa wapo wazaz waliwapeleka watoto wao shule kama Musabe iliyopo Buhongwa napo mwaka huu imefutia matokeo...ebu jaribu kuvaa viatu vya hao wazazI ambao watt wao wamefutiwa matokeo kwa mara ya pil
 
Yaani mwaka jana walifanya mitihani darasa la saba wakafutiwa na mwaka huu napo wamefanya wakafutiwa? Yaani mtoto mmoja kafutiwa Mara mbili ndani ya miaka miwili?
 
Ndugu zangu, usiku wa leo sijalala vizuri, nimefadhaishwa sana na kitendo cha mwanangu wa darasa la saba aliyekuwa anasoma shule ya St Anne Marie academy ya jijini Dar es Salaam kufutiwa matokeo. Yaani nina hasira kali sana kiasi sijajua nichukue hatua gani dhidi ya uongozi wa shule.

Naombeni tushauriane, kama wewe siyo mhanga wa jambo hili unaweza pita kimya kimya tu maana kwa sasa sihitaji kejeli, nahitaji faraja na ushauri.

Hivi mtoto ataenda private? Je, haiwezi kuwa na athari kwenye mitihani ya form four?

Naomba kuwasilisha.

Kuna ufumbuzi mahakamani kwenye hili. Hakuna makosa ya jumuiya. Nini makosa ya watoto hawa au wazazi wao?

Wakawakamate wahalifu siyo kuwabambikizia kesi wahalifu.

Kwanini kamani haki bin hakikama wanadhani wanahoja wasiwape mitihani mingine watoto hawa badala ya kuwapa msongo wa mawazo kwenye umri mdogo huu?
 
sijasema aangalie mtandaoni lama atakuta *W kwa sababu kituo kimefungiwa

mzazi nenda baraza matokeo ya mwanao yapo tena kwa ukamilifu wake kulingana na alichopata......

humu utapigiwa kelele tu... FATILIA MATOKEO YA MWANAO BARAZA...
Wamefungia shule kwa sababu ya udanganyifu wa mwanafunz kweny mtihani...hapa unamshaur aende baraza kuangalia matokeo ya mwanae...iv inamake sense kwel?kwamba baraza watafanya ku asume kwamba mwanae hakufanya udanganifu?
 
Yaani mwaka jana walifanya mitihani darasa la saba wakafutiwa na mwaka huu napo wamefanya wakafutiwa? Yaani mtoto mmoja kafutiwa Mara mbili ndani ya miaka miwili?
Inauma sanaa aysee....kuna mmoja mwaka jana kafutiwa nyamuge...kahamishiwa musabe napo wamepiga pini
 
K
Ni mfumo mzuri sana, ranking inaharibu Elimu. Waende mbali zaidi ya hapo,
Kabxaa...kuna shule ilikuwa ya 9 kitaifa mwaka juzi...magari yote ya shule yaliweka mabango yaliyosomeka 9 kitaifa...mwaka uliofuata kaangukia pua....wizi ni mwingi.sanaa kweny hizi private..hasa za watu binafsi..atleast za kanisa kidogo kuna uhalisia
 
Saana na inawasumbua sana watoto ... naona wameingizwa kwenye mchezo mchafu kwa manufaa ya wenye shule ...
Hao watoto kisheria ni kama walibakwa na hao wenye shule. Kumshirikisha mtoto kwenye uhalifu ni kosa sababu hakufanya kwa ridhaa yake. Serikali ishughulike na hao wenye shule kwa kosa la "kubaka" hao watoto.
 
Back
Top Bottom