Mkuu Jp Omuga,
Ukiangalia thamani ya mijadala inayoendelea ndani ya jukwaa hili siku hizi utajuwa tulipofika kama nchi.
Ndiyo maana utaona hata mabadiliko ya wachangiaji wengi katika mada ni za kusifu au kukashifu tu; hakuna majadiliano ya kina juu ya hoja zinazoelimisha na kushauri.
JF sana sana, sasa hivi imebaki na sifa za jina tu basi, hakuna mijadala mizito.
Ukiona hata watu makini wanapoingia humu na kuchangia chochote, hawatumii ule umakini uliokuwepo hapo zamani; umakini wa kutafuta taarifa sahihi na kuziwasilisha kimpangilio.
Baada ya kuandika haya, hoja yako juu ya katiba ni nzuri sana, lakini sioni jinsi inavyoweza kujadiliwa humu kwa mtindo wa mijadala ilivyo siku hizi.
Sijui kama mada 'serious' kama hiyo itapata wachangiaji ndani ya jukwaa hili kwa jinsi lilivyokaa siku hizi.
Kazi iliyopo siku hizi kwa wachangiaji ni kurashiarashia tu kwenye uandishi bila kujali uzito wa yanayotakiwa kuwasilishwa.
Sijui, labda Maxence anajuwa jinsi ya kutengeneza pawepo na umakini unaotakiwa kwenye mada ya aina hiyo.