Jafo hajawahi kufanya kazi kwenye Halmashauri, anaposema vilivyosusia ni vyama sio wagombea ,ana maanisha wagombea wataendelea kupigiwa kura, hajui madhara yake ukiwa watachaguliwa, hawatashiriki shughuri zozote za maendeleo ikiwa watapita. Ikitokea hivyo shughuri nyingi za kwenye hizi LGAs zinategemea sana hawa viongozi na sio madiwani. Watapelekewa vifaa vya viwandani kwenye miradi wataviweka ndani, shughuri nyingi za wananchi zitakwama.
Mimi nafikiri utafutwe muafaka , Jafo ana mamlaka ya kuwarudisha wagombea wote waliotolewa, kwa sababu makosa yao ni madogodogo tu ya ujazaji wa fomu sio ya jinai.
Lazima ifike mahari tukubali hatukufikiria wakati tunapanga kuwaondoa xhadema na ACT, ilibidi pia tupandikize wahombea toka kwenye vyama vingine 11,ili hawa wakigoma hao wengine wanabakizwa kwa ajiri ya justification, sasa hawajasimamisha wagombea halafu wanaambiwa waende mbele ya waandisha wa habari wakatoe tamko la kuendelea na uchaguzi, wakati tumeshachelewa