Waziri Jafo abadili gia angani, afuta maamuzi yote ya wasimamizi wa uchaguzi kuwaengua wagombea. Wagombea wote ruksa kushiriki uchaguzi

Hao unaowashauri wadai Tume huru ni Wabunge ambao walishinda mwaka 2015 na kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa Wabunge. Unachokizungumza kinakinzana na hali halisi ya mambo. Kama Tume sio huru wao walipataje nafasi zao?
 
TODAYS, Aliongea Kama kada wa chama tu amri inatakiwa kwa Tume ya Uchaguzi
 
Hatua muhimu kuliko zote

1. Tume huru ya uchaguzi
2. Siasa ziruhusiwe majukwaani kwa mujibu wa katiba
3. Katiba ya Jaji Warioba

Wasikubali kushiriki uchaguzi wowote bila hayo mambo matatu.
 
Kila anayekuja speed na kuonekana anaweza kuwa "fursa" kujijenga lazima abomolewe na adharaulike...
Mwisho wa siku tubaki na msifiwa mmoja tu asiyekosea...
 
mumburya, Halafu mtu mwenye kinywa hichohicho ategemewe kuwa na matendo ya haki!

Mnafiki ni zaidi ya muuaji.
 
Hao unaowashauri wadai Tume huru ni Wabunge ambao walishinda mwaka 2015 na kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa Wabunge. Unachokizungumza kinakinzana na hali halisi ya mambo. Kama Tume sio huru wao walipataje nafasi zao?
Wachache kupata siyo kwamba tume ndio huru. Hivi ni kuulize kuna tume huru?
 
😂 mpaka hapa Kama vyama pinzani vitakuwa imara kwa maslahi ya Demokrasia ninategemea kusikia wataingia katka uchaguzi huu pale tu Kuna tume huru ya uchaguzi hata ya mpito!!! Jaffo na watendaji wake warudi mtaani kunadi wagombea wao.

Vinginevyo hakuna uchaguzi na Dunia imeshajua Kuna uchafuzi tu.
 
Hao unaowashauri wadai Tume huru ni Wabunge ambao walishinda mwaka 2015 na kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa Wabunge. Unachokizungumza kinakinzana na hali halisi ya mambo. Kama Tume sio huru wao walipataje nafasi zao?
Narudia kusema wabunge walioko bungeni walipelekwa na nguvu ya Umma . Muda huo demokrasia bado ilikuwepo kabla hajaja Farao asiye mjua Yusufu. Kwa farao huyu, ambaye watu wamepotea wameuliwa, wanatekwa, wanabambikiziwa kesi, tena serikali yake ikawapa wahalifu jina WASIO JULIKANA.

Wadhubuti kama kwa tume hii kuna mbunge toka upinzani hataingi bunge ni, labda wa CUF NA TLP.

Tunapo badili masuala yake kitaifa MASHAULI tuyajadili kwa lengo la kusaidia na kuleta mustakakali wa taifa.
 
Hao unaowashauri wadai Tume huru ni Wabunge ambao walishinda mwaka 2015 na kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa Wabunge. Unachokizungumza kinakinzana na hali halisi ya mambo. Kama Tume sio huru wao walipataje nafasi zao?

Wakati huo Magufuli hakuwa rais na wakati huo demokrasia ilikuwa ina nafuu kwa mbali.
 
Tarehe 24 wananchi wanachagua wagombea ....yaani ile asilimia 32.
badala ya kuwahamasisha wapige kampeni nyie mko mtandaoni
Kweli JINGALAO 😂 ccm ilishapita bila kupingwa kampeni za Nini kawaapisheni tu.

Hatupigi kura bila tume huru ya uchaguzi.
 
Awamu hii viongozi hawafuati sheria wala katiba,wanafanya vyovyote watakavyo!! wapi Ben Saa8? Wapi Azory?
 
Huyu kijana hana ''future'' tena. Hana kingine cha ku-prove kwamba hafai hata kutajwa
 
Kwenda Unafiki tu huna lolote nyuz zako nyingi ni kujikomba komba tu Hovyo
 
Hili la watendaji kufunga ofisi kuwazuia wa gombea wa upinzani kuchukua fomu na wagombea wa upinzani kukamatwa na kuswekwa gerezani wakati wanakwenda kuchukua fomu na kuwafanya wagombea wengi kushindwa kuchukua fomu, haya yote hayaoni? au anataka kusema kuwa hata wale ambao walikuwa ni wagombea lakini wakashindwa kuchukua fomu kutokana na ofisi kufungwa nao wanahesabiwa kama wagombea watakaopigiwa kura?.
 
Mnaomlaumu Jafo mnamuonea tu. Ifike pahala tuyajue mawaziri mashenzi kama akina Lugola au Mwigulu (enzi zake). Jafo ana hekima sana hata kwa kumtazama lakini bwana yuleee ndiyo remote control.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…