Waziri Jafo abadili gia angani, afuta maamuzi yote ya wasimamizi wa uchaguzi kuwaengua wagombea. Wagombea wote ruksa kushiriki uchaguzi

Swali muhimu: Je waziri ana haki kubatilisha maamuzi ya wasimamizi na kamati za rufaa za chaguzi hizi za serikali za mitaa? Ni kanuni zipi zinampa haki ya maamuzi aliyoyafanya? Au wanataka tu kuhalalisha batili? Unawezaje kuhakikisha wagombea kuwa waliowaengua watawatendea haki katika uchaguzi huo? CCM wanaonekana kukosa busara ya kimkakati waliyojisifia na 'kusifiwa' kuwa nayo hiko nyuma
 
Safi sana.Jambo hili lilitukarahisha sana hata sisi wanachama wa CCM.People must be ruled by consent,not by force.
 
Mnaomlaumu Jafo mnamuonea tu. Ifike pahala tuyajue mawaziri mashenzi kama akina Lugola au Mwigulu (enzi zake). Jafo ana hekima sana hata kwa kumtazama lakini bwana yuleee ndiyo remote control.
Hekima ni pamoja na kudimamia unayoyaamini. Ukishindwa hayo una matatizo kama walivyo unaowasema.
 
We have lost sense and wisdom. We need to start afresh.
You are correct.That is why I admire our President,he has realized that we need to start afresh,and he is tying to do just that despite the resistance.
 
You are correct.That is why I admire our President,he has realized that we need to start afresh,and he is tying to do just that despite the resistance.
He probably is not doing it right. Those decisions are being done under his watch and with his concert. He should take responsibility and own both bad and good concequencies of the decidions taken and carrief out by his government. Nyerere did so when his ujamaa vilkage undertaking did not bear the expected results.
 
Hapa patamu sana sasa, mbowe, zitto, maalim seif leteni sera hawa jamaa wamesoma alama za nyakati
 
sasa wakati watendaji wanakata mbuga , hawakai ofisini ulifikiri walipewa likizo?.
wakati wanaandamana kutaka kujua kwa wakurugenzi watachukua hatua gani ilikuwa ni maigizo? ..
wakati waliotoa form zao copy na kisha ile original kukutwa imebadilishwa , sivyo ilivyoandikwa ilikuwa maigizo?
.... wakati TV zote zinaeleza sakata hili la watendaji kukimbia ofisi , wengine ni ndugu zetu wanavunjika na miguu kuwakimbia chadema ilikuwa ni maigizo?......

biblia yangu inaniambia ..mithali 25:21 ... adui yako akiwa na njaa mpe chakula ; tena akiwa na kiu mpe ,mpe maji ya kunywa.

chadema ni kusudi la Mungu , wametekeleza mapenzi ya Mungu ... kwa kuwapa chakula chao ccm , ambao wao wanaona wanastahili kushinda tu .wengine hawastahili.

zaburi 51:17 ....dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika .Moyo uliyovunjika na kupondeka eeh Mungu hutaudharau.

chadema sasa hivi mioyo imevunjika na kupondeka kwa ajili ya amani ya tanzania ... Mungu hawezi kuwaacha , maono haya lazima yatimie tu.. kikubwa kwa chadema ni kutulia . kwa sababu , biblia imesema ni laazima chadema mtulie ndiyo mnapopata nguvu msiyumbushe na wanachama wenu wakorofi .....isaya 30:15.

Mungu ni mwema sana kwa upande wa chadema .
 
I concur with you.There is obvious hesitation on the part of the President in taking prompt and right decisions.Jafos' decision is however the right step in the right direction,inspite of the fact that damage to the image of the government and CCM has already been done.
 
Hao unaowashauri wadai Tume huru ni Wabunge ambao walishinda mwaka 2015 na kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa Wabunge. Unachokizungumza kinakinzana na hali halisi ya mambo. Kama Tume sio huru wao walipataje nafasi zao?
Swali la kijinga sana, sasa embu niambie mwaka 2015 mikutano ya siasa ilikuwa imezuiwa? Na wabunge walikuwa wanafutwa na wengine kupigwa risasi mchana kweupe. ..
Au unazungumzia Tume hii hii yenye maelekezo yote kutoka kwa Chair wa CCM
 
Kuna haja gani ya kuwa na sheria za uchaguzi kama mtu mmoja anayejiita Waziri wa TAMISEMI anaamua kubadili mambo jinsi anavyotaka?
 
Hata kama mtu ameshachaguliwa, chama kilichomdhamini kikimfutia udhamini, anapoteza sifa ya kuwa kiongozi na hivyo hufanyika uchaguzi mpya kujaza nafasi hiyo; Je mheshimiwa huoni kuwa vyama vilivyotangaza kujitoa si vimefuta udhamini kwa wagombea wao? Mimi naona kama chama kimejitoa na hata baada ya kauli yako hii ya kuwarudisha wote, bado wanaendelea kujtoa, wasilazimishwe maana tukifanya hivyo wananchi wanaweza kuwachagua watu wasio na udhamini wa vyama na baadae tukalazimika kuingia kwenye gharama kubwa za uchaguzi mwingine
 
Unafikiri Jafo kafanya hayo kwa maamuzi yake yeye binafsi au kaelekezwa baada ya kuona mambo si sahihi? Kinachotafutwa hapa ni kuhalalisha najisi...kisha tutaona maajabu zaidi kipindi kinachofuata. Very unfortunate.
 
Kinachotafutwa si uchaguzi bali kuhalalisha matokeo yaliyokwishapangwa. Msikilize Jafo kwa makini utagundua hili.
 
Wakati wa kurudisha fomu hawako ofisini kama ilivyotakiwa na maamuzi yao mmeyabariki kwa kuwapitisha wenzenu bila kupingwa

wale waliobahatika kurudisha mmewakata sasa hivi mnajifanya kuwarudisha kwenye gemu kuficha aibu yenu

Watanzania siyo wajinga na endeleeni kuwabagua wazungu wengine mkiwaita mabeberu na wengine mkiwaita marafiki zenu

Kwa maoni yangu sasa ifike wakati wa mtu kutopitishwa bila kupinga ili chama kimoja kikimpitisha mpumbavu asiwe kiongozi wa wananchi kwa lazima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…