Waziri Jafo abadili gia angani, afuta maamuzi yote ya wasimamizi wa uchaguzi kuwaengua wagombea. Wagombea wote ruksa kushiriki uchaguzi

Waziri Jafo abadili gia angani, afuta maamuzi yote ya wasimamizi wa uchaguzi kuwaengua wagombea. Wagombea wote ruksa kushiriki uchaguzi

Watanzania tutabaki gizani hadi pale mwana wa Israel atakapokuja kutimiza wajibu wake,hainiingii akilini Watanzania wote tumeridhia uchaguzi usimamiwe na serikali iliyopo madarakani ambapo na wao ni sehemu ya washindani,hovyo kabisa
Uchaguzi wa serikali za mitaa umenajisiwa,hausafishiki kwa matangazo ya kwenye vyombo vya habari.
Ufutwe kabisa,Serikali ikae na vyama vya siasa kuona njia sahihi ya kufanya chaguzi hizi,lakini hii ya kusema wagombea waliofutwa wamerejeshwa si kweli,chaguzi hizi haziwezi kuwa huru asilani
 
[emoji30][emoji30][emoji30]
masoudkipanya_B4o0u68j7Kl.jpeg
 
Hata anapofanya mabadiliko ya maamuzi ambayo yamaefanywa na wasaidizi wake, amewawajibisha hao wasaidizi? Anasumbua tu kwa kosa ambalo hakufanya yeye. Yeye angefanya maamuzi magumu ya kujiuzulu au kuwawajibisha walioko chini yake walioharibu mchakato wa uchaguzi makusudi kabisa.

Waliowaengua wagombea wa vyama vingine ni Marais wa kata , Jaffo n wewe Urais?
 
Eti anasema kama jina lilikatwa alafu ukaenda kushtaki eti jibu likitoka kuwa umeshinda basi jina lako litakuwa kwenye form ya wagombea..
Sasa najiuliza mtu ameshakatwa alafu chama chake kishajivua alafu jina mkaliweke kwenye form ya wagombea ina maana huyo mgombea atakuwa binafsi au??

Umesema point! Siasa za Tanzania zinadhaminiwa na chama na kama chama kimeshajitoa, mgombea hana tena udhamini wa chama cha siasa. Anaweza kuwa mgombea binafsi lakini si katika fomu ambazo zilishakataliwa.

Sasa ndio kuna sababu nzuri ya kugomea uchaguzi kwa vyama vya siasa. Kama kweli wagombea hawakukidhi vigezo halali - uhalali wa kuwarejesha kupitia tamko uko wapi? Sasa ni dhahiri maamuzi mengi yalifanywa kwa hila!
 
Leo mchana waziri wa tamisemi katangaza uchaguzi mpya na kubatilisha matokeo hasa kwa maeneo waliopita bila kupingwa kwa chama chake.

Nauliza Jafo anamamlaka ya kumvua mtu ushindi?

Yaani mwanachama wa ccm kapewa mamlaka ya kutengua ushindi bila idhiniya mahakama?
Uchaguzi umefanyika tayari? Kuna form za kujaza kukubali matokeo. Sio kaa uchaguzi wa monita wa darasa la pili.
 
Tena hao viongozi wa dini sio wa kuwasikiliza kabisa, maana mambo ya dhuluma za wazi zinafanyika wako kimya. Nadhani ni vyema vyama vyote vilivyosusia vijitoe kabisa kwenye chaguzi zote mpaka tuwe na tume huru ya uchaguzi. Huu uhuni umekuwa wazi kabisa, na kama sio pressure ya mitandao huu uhuni ungeendelea. Hatuwezi kuendelea kufanya chaguzi ambazo box la kura haliheshimiwi. Nadhani hapa hapa ndio sehemu sahihi ya kudai katiba mpya itakayoleta tume huru ya uchaguzi.

Yap. This was serious miscalculation on the part of ccm. Bila shaka kitakachofuata kutoka kwa washindani ni kutoshiriki uchaguzi wowote utakaosimamia na watendaji wa kata/vijiji au Wakurugenzi waliokula kiapo.
 
mbowe atupe ukweli chadema imesimamisha wagombea wangapi?
Mbowe anahusika vipi kwenye tamko la Jafo?

Unaweza ukawa unapenda kuigiza kuwa mtu mpumba.vu, lakini usichokijua, ukifanya mara nyingi baadaye utakuwa mpum.bavu halisia.

Hapa watu wanajadili hoja ya msingi maana ni suala kikatiba na sheria pia. Je, kisheria waziri ana uwezo wa kumvua mtu aliyetangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi wa serikali za mitaa? Sheria inasemaje? Hii ni hoja nzito, na inaweka precedence kwa siku za mbeleni. Kama hujui, kaa kimya ili ueleweshwe na wenye ufahamu.

Usiwe mtu wa kuropoka ropoka. Upu.mbavu siyo kitu cha kukifanyia mazoezi. Ukijizoesha baadaye utakuja kushtuka tayari ukiwa mpumb.avu kamili.
 
Jafo na genge lake wanataka tu wasaidiwe kubariki haramu. Lazima sheria ichukue mkondo wake kuepuka similar unfortunate incidents happening again siku za usoni
 
Back
Top Bottom