Waziri Jafo abadili gia angani, afuta maamuzi yote ya wasimamizi wa uchaguzi kuwaengua wagombea. Wagombea wote ruksa kushiriki uchaguzi

Waziri Jafo abadili gia angani, afuta maamuzi yote ya wasimamizi wa uchaguzi kuwaengua wagombea. Wagombea wote ruksa kushiriki uchaguzi

Namuona akitolewa kafara kwa kufukuzwa uwaziri na aliyemtuma kuchezea uchaguzi.

Ccm inaonyesha ata nyie hamjui mnasimamia nini juzi wataruhusiwa kukata rufaa, jana majina yote yamerudishwa leo hakuna mtu atakayerudishwa walioteuliwa ndio hao hao kauli tatu kutoka kwa mtu mmoja ndani ya wiki moja.
 
Mambo ya kusimamia mchakato na uchaguzi wenyewe yanataka watu wenye akili,maarifa na uwezo wa hali ya juu kusimamia.

Hapa kwetu wapo watu wanaotumia nguvu nyingi na akili kiduchu kusimamia chaguzi zetu,matokeo yake ni vurugu tu.

Awamu hii tutaona mengi
 
SOMENI HIYO TAARIFA VIZURI NYINYI WANA JF, HIYO TAARIFA INASEMA KWAMBA WATAKAORUHUSIWA KUGOMBEA NI WALE WALIOPITISHWA KUGOMBEA TU,
YAANI KIUFUPI JAFO KAGEUKA TENA, KAPIGA U-TURN UPYA, KAIKANA TAARIFA YAKE YA JANA ALIYOITOA MBELE YA VYOMBO VYA HABARI ALIYOSEMA KUWA WOTE WALIOOMBA KUGOMBEA WATARUHUSIWA KUGOMBEA!!
 
Nzi wa kijani mnabadilika Kama kinyonga😜😜😜😜...litakuja tamko jingine mtafata Tena na kukana kauli zenu,ndo maana mnaonekana haziwatoshi.
 
Wewe ndo hujamuelewa Jafo, Kiufupi ni kwamba kwa mujibu wa hilo tangazo, Jafo kafanya U-Turn tena, kama jina lako halijapitishwa kugombea hugombei. Soma namba 1 moja vizuri hapo kwenye hiyo taarifa.

Maana yake ni kwamba waliokatwa wameshakatwa tayari hawaruhusiwi kugombea

Soma vizuri
Hata mimi nimeelewa hivyo yaani hakuna suluhu au kwa kifupi kapingilia msumari au kwa lugha nyepesi kabariki walioenguliwa wasishiriki kabisa uchaguzi
 
Jafo kashindwa kutaja sheria au kanuni aliyoitumia kiwarudisha 96% ya wapinzani walio enguliwa kurudishwa bali anatoa maneno ya kufikirika.

Hapa ndio tujue nchi haifati sheria wala kanuni ni matakwa ya mtu atakavyoamka
View attachment 1260746
Huyu bwana haeleweki. Tangazo lake la jana la kusema kila aliyegombea ataruhusiwa kusimama kwenye uchaguzi amelikana tena. Hawa watu hawaaminiki katika lolote.
 
Nimemsikiliza vizuri sana Jana jumapili alipofanya '"press" conference na maagizo au maelekezo aliyoyatoa kuhusu sakata la wagombea kuenguliwa katika mchakato wa kuwapata viongozi wa serikali za mitaa. Rejea maelekezo haya.
tapatalk_1573392682011.jpeg


Ghafla leo tena namsikia akitoa maelekezo mapya kwa wasimamizi wa uchaguzi huko mawilayani.kiukweli naona kama huyu mtu anachanganyikiwa hebu mlio karibu nae jaribuni kukaa nae nahisi kuna kitu kinamtesa katika roho/nafsi yake asije akachukua maamuzi magumu.

Ni hayo tuu..
 
Wewe ndo hujamuelewa Jafo, Kiufupi ni kwamba kwa mujibu wa hilo tangazo, Jafo kafanya U-Turn tena, kama jina lako halijapitishwa kugombea hugombei. Soma namba 1 moja vizuri hapo kwenye hiyo taarifa.

Maana yake ni kwamba waliokatwa wameshakatwa tayari hawaruhusiwi kugombea

Soma vizuri
Jafo anahitaji kusaidiwa kwa sasa akili siyo yake tena.Jana alisema amefuta maamuzi yote ya wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi leo amewataka wasimamizi wa uchaguzi kuendelea na utekelezaji kwakifupi jafo ameshachanganyikiwa
 
Back
Top Bottom