Waziri Katambi apiga marufuku mikutano ya siasa kwa vyama vyote
Imagine watu wa lobbying wakutane na hiki! Huko kwa wazungu wanasema hiki huku ndani linatoka tamko hili. Kwa ufupi hawa watu wanajipa kazi ngumu sana. Naogopa isijekuwa hizi lobbying ni michongo watu wanaharibu makusudi waombe mafungu ya kwenda nje kupoza! Watu watanyongwa huko mbele kama alivyosema Polepole! Naona kabisa nini kitatokea huko mbele
 
Mnataka siasa zifanyike kipindi cha uchaguzi tu.

Kwani kazi za vyama vya siasa ni nini?, nyie Ccm mtaweza kutekeleza hilo?...

JPM alitangaza hilo zuio pia, ila tulishuhudia chama chake pekee kikifanya siasa huku wengine wakipigwa 'stop', naona mmeamua kurudia hilo.
Waziri amefanya vizuri mkafanye kazi
Kuna mtu unamlisha humu, ukifanya wewe inatosha,
 
Leo bungeni Waziri wa Mambo ya Ndani, Patrobas Katamb ameagiza Jeshi la Polisi kusitisha vibali vya mikutano ya siasa kwa kipindi kisichojulikana.

Moto umekuwa mkali na uwanja umeinama kwa upande wa CCM hadi kuomba tena Msaada wa jeshi la polisi , ingawa wananchi tuliwaonya CCM kuwa vita hii ya kubishana na CHADEMA mtaangukia pua lkn walibisha.


Waziri wa Mambo ya ndani, akiwa bungeni amesema

''Kwa sababu ya taharuki hizi ambazo zimekuwa zikiendelea, nitatumia fursa hii pia, Mheshimiwa Spika, kwa sababu tumekuwa tukisikia majibizano ya hapa na pale, kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ambayo ni custodian wa peace, order, and tranquility, kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ambayo tumepewa instrument na dhamana ya kusimamia amani, ulinzi na usalama, na kwa sababu chochezi wa mambo haya umeonekana zaidi kwenye maeneo ya kisiasa.

Ameongeza, kupitia Bunge lako tukufu, namuelekeza IGP Wambura asitoe vibali kwa kazi zozote zitakazokuwa zinahusiana na kufanya mikutano ya hadhara katika kipindi hiki kwa chama chochote, iwe Chama cha Mapinduzi, iwe chama chochote kile kwa kipindi hiki.

Amemalizia kwa kushauri 'Ni vizuri turudi katika kuwaruhusu wananchi wajenge uchumi wa nchi yao. Ni katika kipindi ambacho tunahitaji kufanya kazi kwa ajili ya kuhakikisha kila Mtanzania, wafanyabiashara, wawekezaji, wanafanya kazi yao kwa amani na utulivu. Nafanya hivi, Mheshimiwa Spika, kwa sababu katika mazingira haya, tutakapokuwa tunawatafuta wahalifu, ni ngumu kuchambua wahalifu kwenye mkusanyiko ya watu wengi."

Pia soma
 
Baadae utakasikia kale katibu mwenezi wa Ccm kako kametembelea USA-River mkoani Arusha, utakasikia "Ccm Oyee, Ccm tunaendelea kutekeleza Ilani yetu.. Chadema muwapuuze, hawana jipya..."

Hapo ccm wao hawaoni kama ni Siasa, ila Chadema wakiitisha tu mkutano. Polisi ndani ya dakika sifuri washawahi na mappumbu yao..
 
Back
Top Bottom