Waziri Mkuu: Bandari imepewa DP-World kwa kuwa utendaji wa TICTS ni mdogo
Akielezea suala linaloendelea kuhusu mkataba wa DP-World na Tanzania ametoa sababu kuwa ni utendaji kazi mdogo wa TICTS ambao umesababisha meli nyingi ziwe zinashushia mizigo Lamu, Mombasa au Afrika kusini hali ambayo imepunguza wateja wa Bandari ya Dar es salaam.

Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa amesema utendaji mbovu wa bandari unasababisha meli zitumie muda mwingi bandarini ambapo gharama ya meli kubaki bandarini huingia mfanya biashara hivyo bidhaa kuwa ghali mtaani. Amesema kwa sasa meli hutumia hadi siku saba kwa mzigo kupakuliwa.

Aidha, amesema awali TPA ilitambua utendaji mbovu na kumpa TICTS mkataba kwa miaka 20 lakini hakukuwa na utendaji mzuri ambapo mkataba huo uliisha 2017 na baadae aliomba kuongezewa miaka mitano ambayo imeisha 2022 na bado hakuweza kuleta vifaa vipya vya kuhudumia bandari.

Waziri Mkuu ameonesha suala la mkataba wa DP-World litarahisisha upakuaji wa mizigo.

Watanzania wametaka maelezo baada ya kuwa na utata katika baadhi ya vipengele vya mkataba huo ambao kwa kiasi kikubwa serikali na spika wa bunge wamekuwa wakivitolea maelezo.

Waziri mkui wambie watanganyika kwani hawa nao wamepewa waarabu?
 
Attachments

  • B3B67456-A266-4254-B05E-DEF1144556A7.jpeg
    B3B67456-A266-4254-B05E-DEF1144556A7.jpeg
    23.3 KB · Views: 7
  • 7394C415-7323-4D46-A53C-71E06463F480.jpeg
    7394C415-7323-4D46-A53C-71E06463F480.jpeg
    51.3 KB · Views: 7
  • 10E85B9E-722D-47EB-823B-83B72E0FCEEB.jpeg
    10E85B9E-722D-47EB-823B-83B72E0FCEEB.jpeg
    140.9 KB · Views: 7
  • 60EA54BB-F99D-4343-8F13-AB1324C6B416.jpeg
    60EA54BB-F99D-4343-8F13-AB1324C6B416.jpeg
    66.2 KB · Views: 6
Akielezea suala linaloendelea kuhusu mkataba wa DP-World na Tanzania ametoa sababu kuwa ni utendaji kazi mdogo wa TICTS ambao umesababisha meli nyingi ziwe zinashushia mizigo Lamu, Mombasa au Afrika kusini hali ambayo imepunguza wateja wa Bandari ya Dar es salaam.

Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa amesema utendaji mbovu wa bandari unasababisha meli zitumie muda mwingi bandarini ambapo gharama ya meli kubaki bandarini huingia mfanya biashara hivyo bidhaa kuwa ghali mtaani. Amesema kwa sasa meli hutumia hadi siku saba kwa mzigo kupakuliwa.

Aidha, amesema awali TPA ilitambua utendaji mbovu na kumpa TICTS mkataba kwa miaka 20 lakini hakukuwa na utendaji mzuri ambapo mkataba huo uliisha 2017 na baadae aliomba kuongezewa miaka mitano ambayo imeisha 2022 na bado hakuweza kuleta vifaa vipya vya kuhudumia bandari.

Waziri Mkuu ameonesha suala la mkataba wa DP-World litarahisisha upakuaji wa mizigo.

Watanzania wametaka maelezo baada ya kuwa na utata katika baadhi ya vipengele vya mkataba huo ambao kwa kiasi kikubwa serikali na spika wa bunge wamekuwa wakivitolea maelezo.

Hatuna shida na DPW. Sisi wananchi tuna shida na yaliyomo kwenye mkataba.
 
Waziri mkuu waambie watanganyika kwanini DP world hawakupewa bandari ya Zanzibar ?

Waziri mkuu waambie watanganyika kwanini mwanasheria mkuu wa serikali hakusaini mkataba wa DP world?

Waziri mkuu waambie watanganyika wabunge 30 na waandishi wa habari kibao walikwenda kufanya nini Dubai na walikwenda huko kwa gharama za nani?

Waziri mkuu soma ujumbe huu ili ujue watanganyika hawakuamini👇
 
Attachments

  • 658B4AA4-5F41-4CF1-9E0E-DFB907268572.jpeg
    658B4AA4-5F41-4CF1-9E0E-DFB907268572.jpeg
    37.4 KB · Views: 8
Majibu rahisi kwa hoja zenye msingi pale unaposema walifanya bila ya ufanisi kwani hakuna aliyekuwa anawasimamia hao TICTS katika mkataba wao wa awali hadi wafanye watakayo bila ya kuleta mitambo ya kutosha ya kupakulia mizigo toka kwenye meli. Kipi kiliwafanya muwaongezee mkataba wa miaka 5 tena na ikiwa hiyo miaka 20 walikuwa nje ya ufanisi . Hawa DP WORLD mmejipanga vipi kuwasimamia au mnataka mkiwa kaburini wajukuu zenu waje kuwasema kwa kushindwa kuweka wazi namna ya kuwasimamia hawa pia maana mfano tumeona kwa TICTS for 25 years with poor supervisory finally lead to blah blah , Tunangojea kuona BIDHAA zikishuka? . PM TUAMBIE FAIDA ZA MKATABA NA DP WORLD KWA MASLAHI YA TANZANIA YETU NA SI KWA HOJA DHAIFU HIZO.
 
Ni kweli TICS wamekuwa na utendaji mdogo tumewatoa, je hewa DPW na wenyewe wakiwa na utendaji mbovu tunaweza kuwatoa na kuweka wengine?
Waziri mkuu alipita bila kupingwa kinyume na katiba ya nchi sasa anasimamia kuuzwa kwa bandari na kila kitu.
Mwenye ile hukumu ya kukataliwa kwa kupita bila kupingwa tafadhali aiweke hapa
 
Hajajibu hoja zinazotiliwa shaka na wananchi.

Kwa ni wamepewa mkaba usio na Kikomo

Kwa nini wamepewa Bandari zoote, Anga, Reli na Barabara milele na milele.

Waziri Mkuu na yeye ni kama hajui kama sisi tu.

Mkataba upi? Mkataba bado
 
Kwanini hawakupewa maeneo waliyopewa ticts badala yake wamepewa bandari zote za Tanganyika, kama ticts walipewa miaka 20 na baadae miaka 5 wakashindwa huyu akishindwa ataondolowaje wakati mkataba hauna kikomo
 
Hili limeelezwa sana ila wapigaji pale bandarini ni wengi vishoka hawawezi kukubali mabadiliko kwa haraka tonge linadondoka.
 
Uzuri wake tumebakiza mwaka 1 kuingia kwenye Uchaguzi ujao hapo 2025.

Na kwa taarifa za ndani ile nguvu ya Ukawa ya 2015 itakuwa mara mbili zaidi maana ushawishi wa Chama Tawala upande wa Kanda ya ziwa umeshuka zaidi baada ya kifo cha JPM
 
Ila hii nchi ina mambo ya ajabu!! Mtu mmempa mkataba wa miaka 20 akavurunda vibaya bado mnamuongezea wa miaka mitano!!!! No wonder huu mkataba mwingine umekaa ndivyo sivyo🙆🙆🙆
 
Akielezea suala linaloendelea kuhusu mkataba wa DP-World na Tanzania ametoa sababu kuwa ni utendaji kazi mdogo wa TICTS ambao umesababisha meli nyingi ziwe zinashushia mizigo Lamu, Mombasa au Afrika kusini hali ambayo imepunguza wateja wa Bandari ya Dar es salaam.

Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa amesema utendaji mbovu wa bandari unasababisha meli zitumie muda mwingi bandarini ambapo gharama ya meli kubaki bandarini huingia mfanya biashara hivyo bidhaa kuwa ghali mtaani. Amesema kwa sasa meli hutumia hadi siku saba kwa mzigo kupakuliwa.

Aidha, amesema awali TPA ilitambua utendaji mbovu na kumpa TICTS mkataba kwa miaka 20 lakini hakukuwa na utendaji mzuri ambapo mkataba huo uliisha 2017 na baadae aliomba kuongezewa miaka mitano ambayo imeisha 2022 na bado hakuweza kuleta vifaa vipya vya kuhudumia bandari.

Waziri Mkuu ameonesha suala la mkataba wa DP-World litarahisisha upakuaji wa mizigo.

Watanzania wametaka maelezo baada ya kuwa na utata katika baadhi ya vipengele vya mkataba huo ambao kwa kiasi kikubwa serikali na spika wa bunge wamekuwa wakivitolea maelezo.

Kwahiyo tayari DPW walishapewa?!!

Kwanini haikutangazwa tenda kama ilivyo taratibu?

Kwanini wananchi walidharauliwa kuchukuliwa mawazo yao kwanza kabla hawajaenda kwenye makubaliano?

Hii sio SAWA
 
1. Je, kuwapa hao DPW ndio suluhisho la kudumu la tatizo hilo??
2.Katika miaka yote hii ya Uhuru, Je, Serikali yenyewe imefanya juhudi gani za makusudi katika kuwawezesha Watanzania wazawa ili waweze kuendesha Bandari hiyo?? Kwa nini haikuunda Kampuni yake yenyewe ambayo ni strong and competent katika kufanya shughuli za Badari??
3. Je, kuuza au kubinafsisha wa wageni kila taasisi ya Serikali iliyoshindwa kujiendesha ndio suluhisho sahihi l a matatizo yetu??
4. Je, kampuni ya kitanzania yenye uwezo wa kufanya kazi za bandari ni TICTS tu peke yake??Zingine mbadala hakuna hadi wapewe DPW??
5. Kama utendaji usioridhisha wa Kampuni ya TICTS ndio kigezo kilichosababisha bandari kuuzwa kwa wageni, mbona kuna taasisi nyingi hapa nchini ( taasisi binafsi na taasisi za Serikali) ikiwamo na Ofisi yake ya Waziri Mkuu na Ikulu ya Rais pia, taasisi ambazo nazo utendaji wake si wa kuridhisha.Je, taasisi hizo (Ikulu na OWM nazo sasa tunatakiwa tuzibinafsishe kwa raia wa kigeni eti kisa zina utendaji usioridhisha???? Ndio anataka kutuambia hivi Watanzania??
6.Je, TPA itakuwa na Jukumu gani basi baada ya bandari zote kubinafsishwa hapa Tz???
7.Ni kwa nini Serikali isifikirie kuivunja Mamlaka ya Bandari (TPA), kuivunja TASAC pamoja na taasisi zingine zote zinazohusika na masuala ya Bandari hapa nchini ili kuunda kampuni moja kubwa itakayoshirikiana au kuingia ubia na taasisi binafsi za ndani ya nchi kama vile TICTS ili kufanya kazi za bandari kwa ufanisi zaidi badala ya kufikiria kubinafsisha bandari zote kwa kampuni ya kigeni ya DPW kwa Mkataba wa maisha/milele????????????
Maswali yote uliyouliza yana jibu moja tu ni kwamba DP WORLD anakidhi sifa miongoni mwa makampuni yote katika uendeshaji wa bandari.
 
Hajajibu hoja zinazotiliwa shaka na wananchi.

Kwa ni wamepewa mkaba usio na Kikomo

Kwa nini wamepewa Bandari zoote, Anga, Reli na Barabara milele na milele.

Waziri Mkuu na yeye ni kama hajui kama sisi tu.
Nyie siyo kwamba hamjui ila mmeamua kukaza shingo kwa sababu mnazozijua hasa za kibiashara mnaona maslahi yenu yapo hatarini.
 
Back
Top Bottom