1. Je, kuwapa hao DPW ndio suluhisho la kudumu la tatizo hilo??
2.Katika miaka yote hii ya Uhuru, Je, Serikali yenyewe imefanya juhudi gani za makusudi katika kuwawezesha Watanzania wazawa ili waweze kuendesha Bandari hiyo?? Kwa nini haikuunda Kampuni yake yenyewe ambayo ni strong and competent katika kufanya shughuli za Badari??
3. Je, kuuza au kubinafsisha wa wageni kila taasisi ya Serikali iliyoshindwa kujiendesha ndio suluhisho sahihi l a matatizo yetu??
4. Je, kampuni ya kitanzania yenye uwezo wa kufanya kazi za bandari ni TICTS tu peke yake??Zingine mbadala hakuna hadi wapewe DPW??
5. Kama utendaji usioridhisha wa Kampuni ya TICTS ndio kigezo kilichosababisha bandari kuuzwa kwa wageni, mbona kuna taasisi nyingi hapa nchini ( taasisi binafsi na taasisi za Serikali) ikiwamo na Ofisi yake ya Waziri Mkuu na Ikulu ya Rais pia, taasisi ambazo nazo utendaji wake si wa kuridhisha.Je, taasisi hizo (Ikulu na OWM nazo sasa tunatakiwa tuzibinafsishe kwa raia wa kigeni eti kisa zina utendaji usioridhisha???? Ndio anataka kutuambia hivi Watanzania??
6.Je, TPA itakuwa na Jukumu gani basi baada ya bandari zote kubinafsishwa hapa Tz???
7.Ni kwa nini Serikali isifikirie kuivunja Mamlaka ya Bandari (TPA), kuivunja TASAC pamoja na taasisi zingine zote zinazohusika na masuala ya Bandari hapa nchini ili kuunda kampuni moja kubwa itakayoshirikiana au kuingia ubia na taasisi binafsi za ndani ya nchi kama vile TICTS ili kufanya kazi za bandari kwa ufanisi zaidi badala ya kufikiria kubinafsisha bandari zote kwa kampuni ya kigeni ya DPW kwa Mkataba wa maisha/milele????????????