Waziri Mkuu: Bandari imepewa DP-World kwa kuwa utendaji wa TICTS ni mdogo
Wametangaza sana toka mwaka Jana lakini hujapeleka mtu wako ashindanishwe
1.Je, hiyo Zabuni unayodai "imetangazwa sana" ilikuwa ni namba ngapi???
2.Ilitangazwa lini, yaani tarehe ngapi na katika chombo/vyombo gani vya habari???
3.Hao waarabu wa DPW unaowatetea sana walipata tuzo ya hiyo kazi kwa Zabuni gani?Ilitangazwa lini hiyo Zabuni?Tathmini ya hiyo Zabuni ya DPW ilifanyika lini?Je wajumbe wa Kamati ya Tathmini walikuwa ni akina nani???
Ningependa kukukumbusha kwamba, "No research no right to speak": By Mao Tse Dong
 
Sawa mkuu, vipi kuhusu kikomo cha mkataba, je? Ni kweli pia bandari zote hadi za maziwa zitakuwa chini ya DPW? Naomba msaada wako maana mimi nasikia sikia tu.
Wapi imesemwa bandari zote zitakuwa chini yao?
 
B
1.Je, hiyo Zabuni unayodai "imetangazwa sana" ilikuwa ni namba ngapi???
2.Ilitangazwa lini, yaani tarehe ngapi na katika chombo/vyombo gani vya habari???
3.Hao waarabu wa DPW unaowatetea sana walipata tuzo ya hiyo kazi kwa Zabuni gani?Ilitangazwa lini hiyo Zabuni?Tathmini ya hiyo Zabuni ya DPW ilifanyika lini?Je wajumbe wa Kamati ya Tathmini walikuwa ni akina nani???
Ningependa kukukumbusha kwamba, "No research no right to speak": By Mao Tse Dong
Fatilia news kila siku ukitaka haya mambo. Kwa mfano Leo hii serikali wametangaza kuuza Treasury bills, unajua na umefatilia? Msibishe tu ili mueleweke mmebisha. Bora huyu mama angalau anatangaza, enzi zile za giza za yule mwendawazimu kila tenda ilikuwa inaenda kwa ndugu na jamaa zake tu Wala hamna kutangaza popote na vyombo vya habari vilikuwa vimezimwa.
 
Taja namba ya tangazo la zabuni, acha blah blah za kisiasa. Kila zabuni inayotangazwa hapa nchini lazima inakuwa ina namba yake maalumu ya utambuzi. Aidha, ni lazima pia inakuwa imesajiliwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Manunuzi ya Serikali. Sasa hiyo zabuni ya uendeshaji wa bandari ilitangazwa lini???Imesajiliwa lini??
Narudia tena kukukumbusha kwamba "no research no right to speak".
 
Akielezea suala linaloendelea kuhusu mkataba wa DP-World na Tanzania ametoa sababu kuwa ni utendaji kazi mdogo wa TICTS ambao umesababisha meli nyingi ziwe zinashushia mizigo Lamu, Mombasa au Afrika kusini hali ambayo imepunguza wateja wa Bandari ya Dar es salaam.

Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa amesema utendaji mbovu wa bandari unasababisha meli zitumie muda mwingi bandarini ambapo gharama ya meli kubaki bandarini huingia mfanya biashara hivyo bidhaa kuwa ghali mtaani. Amesema kwa sasa meli hutumia hadi siku saba kwa mzigo kupakuliwa.

Aidha, amesema awali TPA ilitambua utendaji mbovu na kumpa TICTS mkataba kwa miaka 20 lakini hakukuwa na utendaji mzuri ambapo mkataba huo uliisha 2017 na baadae aliomba kuongezewa miaka mitano ambayo imeisha 2022 na bado hakuweza kuleta vifaa vipya vya kuhudumia bandari.

Waziri Mkuu ameonesha suala la mkataba wa DP-World litarahisisha upakuaji wa mizigo.

Watanzania wametaka maelezo baada ya kuwa na utata katika baadhi ya vipengele vya mkataba huo ambao kwa kiasi kikubwa serikali na spika wa bunge wamekuwa wakivitolea maelezo.

Maelezo ya waziri mkuu yamejitosheleza. Ameongea kama mtu mwenye dhamana ya kukagua kazi za bandarini mara kwa mara. Ameongea kama mtu mwenye mamlaka anayoyastahili.

Wengi humu JF tunapiga kelele za kishabiki zile ambazo hazina uzalendo wa aina yoyote ile.

Mtanzania kweli mwenye uzalendo na mwenye kutambua shida ya bandarini hauwezi kupoteza muda kupinga uwekezaji unaokwenda kuongeza tija ya bandari kwa ujumla.

Mtu mwenye kujielewa vyema kichwani hauwezi kupinga ufanisi wa kazi unaokwenda kupunguza foleni ya meli ambayo inaongeza bei za bidhaa humu mitaani.

Unaweza kueleweka ukiwa unafanya kazi ya siri ya TICTS ambaye kashindwa kuendana na mahitaji ya bandari ya muda huu lakini iwapo haupo huko halafu unaopinga kwa nguvu zote hiki kinachotaka kufanywa na awamu ya sita, basi unalo tatizo kubwa sana lenye kuweza kutatuliwa na madaktari mabingwa wa matatizo ya akili pale Muhimbili.
 
Majibu rahisi kwa hoja zenye msingi pale unaposema walifanya bila ya ufanisi kwani hakuna aliyekuwa anawasimamia hao TICTS katika mkataba wao wa awali hadi wafanye watakayo bila ya kuleta mitambo ya kutosha ya kupakulia mizigo toka kwenye meli. Kipi kiliwafanya muwaongezee mkataba wa miaka 5 tena na ikiwa hiyo miaka 20 walikuwa nje ya ufanisi . Hawa DP WORLD mmejipanga vipi kuwasimamia au mnataka mkiwa kaburini wajukuu zenu waje kuwasema kwa kushindwa kuweka wazi namna ya kuwasimamia hawa pia maana mfano tumeona kwa TICTS for 25 years with poor supervisory finally lead to blah blah , Tunangojea kuona BIDHAA zikishuka? . PM TUAMBIE FAIDA ZA MKATABA NA DP WORLD KWA MASLAHI YA TANZANIA YETU NA SI KWA HOJA DHAIFU HIZO.
Faida za mkataba ni kuongezeka kwa ufanisi pale bandarini.

Faida za mkataba ni kupungua kwa muda wa meli zinazokaa foleni baharini zikisubiri kushushwa mizigo.

Faida za mkataba kuokoa muda ambao unakwenda kutumiwa na meli hiyo kwa ajili ya kuondoka na kwenda kuzalisha sehemu nyingine.

Faida za mkataba ni kuondoa gharama zote za meli kukaa nangani ikisubiri kuhudumiwa, kumbuka hizo ni gharama zinaozoingiwa aidha na mteja anayesubiri bidhaa yake au bandari yenyewe.

Hizi zako ni hoja za mtu ambaye pengine hajawahi hata kutumia bandari maskini ya Mungu, hana bidhaa inayokwama katika kuitoa au kuipakia pale bandarini.

Ni hoja za mtu kakaa kwenye kiti chake pengine Mwanza au Morogoro anaongea kishabiki tu!.
 
Akielezea suala linaloendelea kuhusu mkataba wa DP-World na Tanzania ametoa sababu kuwa ni utendaji kazi mdogo wa TICTS ambao umesababisha meli nyingi ziwe zinashushia mizigo Lamu, Mombasa au Afrika kusini hali ambayo imepunguza wateja wa Bandari ya Dar es salaam.

Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa amesema utendaji mbovu wa bandari unasababisha meli zitumie muda mwingi bandarini ambapo gharama ya meli kubaki bandarini huingia mfanya biashara hivyo bidhaa kuwa ghali mtaani. Amesema kwa sasa meli hutumia hadi siku saba kwa mzigo kupakuliwa.

Aidha, amesema awali TPA ilitambua utendaji mbovu na kumpa TICTS mkataba kwa miaka 20 lakini hakukuwa na utendaji mzuri ambapo mkataba huo uliisha 2017 na baadae aliomba kuongezewa miaka mitano ambayo imeisha 2022 na bado hakuweza kuleta vifaa vipya vya kuhudumia bandari.

Waziri Mkuu ameonesha suala la mkataba wa DP-World litarahisisha upakuaji wa mizigo.

Watanzania wametaka maelezo baada ya kuwa na utata katika baadhi ya vipengele vya mkataba huo ambao kwa kiasi kikubwa serikali na spika wa bunge wamekuwa wakivitolea maelezo.

Hapa hakuna waziri mkuu ni chenga tu,sasa aliyeshindwa kuwasimamia hao ticks ni nani na je hizo mashine zinazofanya kazi vzr bandari za Dubai zilijipeleka zenyewe pale,Hivi kwa nn Viongozi wetu ni wafupi sana kiakili,waziri mkuu unapelekwa pelekwa tu kama remote.Watanganyika wenye akili lzm washtuke kwa sababu wenye authority ya serikali yetu ni wazanzibar na hawajainclude bandari za zanzibar kwenye mkataba kwa nn,muungano uko wapi hapo.CCM mnachekesha sana na Watanganyika wanaccm waliopo Bungeni ni sawa sawa na kenge tu mnashindwa kuelewa mchezo uliopo,mnaiweka bandari yenu rehani,Kila mtanzania anajua Bunge halina upinzani,sasa keshokutwa mtasema nani aliwakwamisha kutumia AKILI zetu mlizopewa na MUNGU MWENYEZI,Vichwa tulipewa na MUNGU kwa ajili ya kufikiri na si kufuga nywele.
 
Akielezea suala linaloendelea kuhusu mkataba wa DP-World na Tanzania ametoa sababu kuwa ni utendaji kazi mdogo wa TICTS ambao umesababisha meli nyingi ziwe zinashushia mizigo Lamu, Mombasa au Afrika kusini hali ambayo imepunguza wateja wa Bandari ya Dar es salaam.

Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa amesema utendaji mbovu wa bandari unasababisha meli zitumie muda mwingi bandarini ambapo gharama ya meli kubaki bandarini huingia mfanya biashara hivyo bidhaa kuwa ghali mtaani. Amesema kwa sasa meli hutumia hadi siku saba kwa mzigo kupakuliwa.

Aidha, amesema awali TPA ilitambua utendaji mbovu na kumpa TICTS mkataba kwa miaka 20 lakini hakukuwa na utendaji mzuri ambapo mkataba huo uliisha 2017 na baadae aliomba kuongezewa miaka mitano ambayo imeisha 2022 na bado hakuweza kuleta vifaa vipya vya kuhudumia bandari.

Waziri Mkuu ameonesha suala la mkataba wa DP-World litarahisisha upakuaji wa mizigo.

Watanzania wametaka maelezo baada ya kuwa na utata katika baadhi ya vipengele vya mkataba huo ambao kwa kiasi kikubwa serikali na spika wa bunge wamekuwa wakivitolea maelezo.

Waziri mkuu baada ya kukaa kimya kwa wiki mbili, leo ameamua kuja kisanii sana. Ametoa majibu ya kisiasa na kisanii sana.
 
Faida za mkataba ni kuongezeka kwa ufanisi pale bandarini.

Faida za mkataba ni kupungua kwa muda wa meli zinazokaa foleni baharini zikisubiri kushushwa mizigo.

Faida za mkataba kuokoa muda ambao unakwenda kutumiwa na meli hiyo kwa ajili ya kuondoka na kwenda kuzalisha sehemu nyingine.

Faida za mkataba ni kuondoa gharama zote za meli kukaa nangani ikisubiri kuhudumiwa, kumbuka hizo ni gharama zinaozoingiwa aidha na mteja anayesubiri bidhaa yake au bandari yenyewe.

Hizi zako ni hoja za mtu ambaye pengine hajawahi hata kutumia bandari maskini ya Mungu, hana bidhaa inayokwama katika kuitoa au kuipakia pale bandarini.

Ni hoja za mtu kakaa kwenye kiti chake pengine Mwanza au Morogoro anaongea kishabiki tu!.
Hayo yote TICTS wameshindwa yafanya kwa miaka 25 wakiwa chini ya usimamizi wa serikali na unaamini wataweza hawa DP WORLD chini ya usimamizi wa serikali ile ile . Watanzania wote ni watumiaji wa bandari kwakuwa asilimia nyingi za bidhaa zinatoka nje kama si malighafi basi ni bidhaa kamili hivyo acha UJINGA wa kuhisi anayeagiza au kutuma mzigo kupitia bandari ndiye mwenye hati miliki ya kuhoji ufanisi wa bandari na mustakabali wake bali ni jukumu la kila mwananchi kwa nafasi yake.
Bado unaongea kwa ushabiki kama unaowaita mashabiki pia , chukua taarifa kamili ili uje kutupasha hapa ya kwamba ule mkataba ni wa miaka 10, 20 au 30 kisha faida zake ni hizi na masharti ya uendeshaji ni haya na haya hapo sasa utakuwa umejibu minong'ono kwa hoja nzuri na nzito.
Hoya sisi tunapenda hii nchi iwe zaidi ya DUBAI ulipo sema misingi ya uwazi ndiyo tunaitaka na DP WORLD they are smart in terms of capital regardles historia za nchi walizowekeza na kesi zao huku nyuma, tambua mimi sipingi hilo la uwekezaji kwakuwa sisi tumeshindwa kufika mahali pazuri hivyo kusaidiwa ni jambo zuri tena sana.
 
Ngoja waje pingapinga fc
Wewe bushlawyer unayewaza kwa kutumia tumbo lako! Jifunze mujibu hoja Kama mtaalam wa Sheria Basi eeh! Mbona umegeuka kituko humu? Siamini Kama kweli una elimu ya Sheria. Watu weledi wanawaelimisha wengine juu ya ubaya na uzuri wa mikataba wewe unaleta maujinga yako! Acha kuia ugoro!
 
Hayo yote TICTS wameshindwa yafanya kwa miaka 25 wakiwa chini ya usimamizi wa serikali na unaamini wataweza hawa DP WORLD chini ya usimamizi wa serikali ile ile . Watanzania wote ni watumiaji wa bandari kwakuwa asilimia nyingi za bidhaa zinatoka nje kama si malighafi basi ni bidhaa kamili hivyo acha UJINGA wa kuhisi anayeagiza au kutuma mzigo kupitia bandari ndiye mwenye hati miliki ya kuhoji ufanisi wa bandari na mustakabali wake bali ni jukumu la kila mwananchi kwa nafasi yake.
Bado unaongea kwa ushabiki kama unaowaita mashabiki pia , chukua taarifa kamili ili uje kutupasha hapa ya kwamba ule mkataba ni wa miaka 10, 20 au 30 kisha faida zake ni hizi na masharti ya uendeshaji ni haya na haya hapo sasa utakuwa umejibu minong'ono kwa hoja nzuri na nzito.
Hoya sisi tunapenda hii nchi iwe zaidi ya DUBAI ulipo sema misingi ya uwazi ndiyo tunaitaka na DP WORLD they are smart in terms of capital regardles historia za nchi walizowekeza na kesi zao huku nyuma, tambua mimi sipingi hilo la uwekezaji kwakuwa sisi tumeshindwa kufika mahali pazuri hivyo kusaidiwa ni jambo zuri tena sana.
Serikali huenda zikibadilika kiufanisi mwaka mmoja baada ya mwingine, serikali yetu inao watendaji wazuri zaidi sasa hivi kuliko waliokuwepo miaka 30 iliyopita, hilo kwanza ulitambue.

Tunapoteza muda mwingi kwenye majadiliano mengi yanayoanzishwa na watu negative wakati DRC na Rwanda wakiwa tayari wameshaingia mkataba na hawa DPW.

Kama tunapenda nchi iwe kama Dubai na tuachane na akili za urasimu na wizi wa bandarini, kwani unatukwamisha na kutupotezea mapato mengi ambayo hutuacha na umaskini ule ule.

Mabadiliko au reforms anazoziendeleza SSH zilianzishwa na hayati JPM, zina maumivu yake lakini ni lazima tuyavumilie ikiwa tunataka kweli kwa vitendo tuwe sehemu ya nchi zilizo katika uchumi wa kati wa juu.
 
Kama hamjamuelewa na huyu aliye ongea kwa kiswahili chepesi kabisa basi mnyamaze msubiri matokeo mazuri.
Kaongea kipi Cha maana? Yeye Kama mtendaji mkuu wa serikali alishawahi kuwaita ticts ofisini kwake kuwakemea? Alishawahi kwenda bandarini kuwaonya wafanyakazi wezi na wazembe wasiowajibika? Alishawahi kumsimamisha mtendaji yeyote wa bandari kwa utendaji mbovu? Akubali tu kuwa yeye na serikali anayoisi.amia imeshindwa kufanya kazi yenye matokeo chanya kwa wananchi.
Kwani akimbilie kuuza badala ya kutafuta na kuinunua hiyo teknolojia ya dpw pamoja na kusomesha vijana wazalendo? Hajajibu lolote zaidi ya kukazia bandari iuzwe.
 
Maana yake , yeye kama waziri mkuu na mtendanji wa serikali- HATOSHI- kama utendaji kazi mdogo, kwa ni nini wasiongeze ufanisi kwa sisi wenyewe. kama utendaji kazi mdogo, chanzoi ne yeye. Longo longo tupu na kuzunguka mbuyu.
Yeye na mwanaye Wana kampuni yao ya kutoa mizigo hapo bandarini na ni wakwepa Kodi wazuri tu!
 
Kwani jpm aliwahi kutangaza tenda hata moja au mnamuonea Samia tu kwa sababu amewapa uhuru wa kuongea
Uwe na hofu ya Mungu. TPA haijawahi kutangaza tenda yoyote na Kama naongopq weka copy ya tangazo Hilo hapa!
 
Back
Top Bottom