Waziri Mkuu: Bandari imepewa DP-World kwa kuwa utendaji wa TICTS ni mdogo
Uzuri wake tumebakiza mwaka 1 kuingia kwenye Uchaguzi ujao hapo 2025.

Na kwa taarifa za ndani ile nguvu ya Ukawa ya 2015 itakuwa mara mbili zaidi maana ushawishi wa Chama Tawala upande wa Kanda ya ziwa umeshuka zaidi baada ya kifo cha JPM
 
Attachments

  • 0FA3BCD7-19E3-4EB1-A1D3-BCF8F2351826.jpeg
    0FA3BCD7-19E3-4EB1-A1D3-BCF8F2351826.jpeg
    39.6 KB · Views: 6
Akielezea suala linaloendelea kuhusu mkataba wa DP-World na Tanzania ametoa sababu kuwa ni utendaji kazi mdogo wa TICTS ambao umesababisha meli nyingi ziwe zinashushia mizigo Lamu, Mombasa au Afrika kusini hali ambayo imepunguza wateja wa Bandari ya Dar es salaam.

Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa amesema utendaji mbovu wa bandari unasababisha meli zitumie muda mwingi bandarini ambapo gharama ya meli kubaki bandarini huingia mfanya biashara hivyo bidhaa kuwa ghali mtaani. Amesema kwa sasa meli hutumia hadi siku saba kwa mzigo kupakuliwa.

Aidha, amesema awali TPA ilitambua utendaji mbovu na kumpa TICTS mkataba kwa miaka 20 lakini hakukuwa na utendaji mzuri ambapo mkataba huo uliisha 2017 na baadae aliomba kuongezewa miaka mitano ambayo imeisha 2022 na bado hakuweza kuleta vifaa vipya vya kuhudumia bandari.

Waziri Mkuu ameonesha suala la mkataba wa DP-World litarahisisha upakuaji wa mizigo.

Watanzania wametaka maelezo baada ya kuwa na utata katika baadhi ya vipengele vya mkataba huo ambao kwa kiasi kikubwa serikali na spika wa bunge wamekuwa wakivitolea maelezo.

Hawa jamaa hoja za msingi wanazikwepa.., yaani hakuna hata mmoja anayejibu kwa ufasaha nikuzunguka mbuyu tu. Kama vp wawe wanatangaza tenda then wawekezaji wanaomba halafu tunaangalia anayetufaa.
 
Akielezea suala linaloendelea kuhusu mkataba wa DP-World na Tanzania ametoa sababu kuwa ni utendaji kazi mdogo wa TICTS ambao umesababisha meli nyingi ziwe zinashushia mizigo Lamu, Mombasa au Afrika kusini hali ambayo imepunguza wateja wa Bandari ya Dar es salaam.

Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa amesema utendaji mbovu wa bandari unasababisha meli zitumie muda mwingi bandarini ambapo gharama ya meli kubaki bandarini huingia mfanya biashara hivyo bidhaa kuwa ghali mtaani. Amesema kwa sasa meli hutumia hadi siku saba kwa mzigo kupakuliwa.

Aidha, amesema awali TPA ilitambua utendaji mbovu na kumpa TICTS mkataba kwa miaka 20 lakini hakukuwa na utendaji mzuri ambapo mkataba huo uliisha 2017 na baadae aliomba kuongezewa miaka mitano ambayo imeisha 2022 na bado hakuweza kuleta vifaa vipya vya kuhudumia bandari.

Waziri Mkuu ameonesha suala la mkataba wa DP-World litarahisisha upakuaji wa mizigo.

Watanzania wametaka maelezo baada ya kuwa na utata katika baadhi ya vipengele vya mkataba huo ambao kwa kiasi kikubwa serikali na spika wa bunge wamekuwa wakivitolea maelezo.

Nchi ina matatizo mengine hata huwezi kuyaelezea...
 
Hayo yatasemwa kwenye HGA
Tatizo mkataba mama tumishaukubai na kuwa sheria kwa sababu umshapitishwa na bunge
Hayo mengine yote yanayokuja yanajengwa na mataba mama ambao tumeishaukubali. Hizo polojo za waziri mkuu ni usanii tuu.

Kama kulikuwa na makubaliano mengine kwanini wasingojee kwanza kabla ya mkataba mama kuridhiwa na bunge?? Hivi unajua usudi la kupelekwa bungeni na kuridhiwa?

Mkuu hapo tukubali tu tumeshapigwa. Sasahivi hata tufany nini hatuwezi kujitoa ktk haya mkubaliano, hata kitokee nini hatutaweza kujitoa maana tumeshalikubali hilo ktk mkataba mama
 
Kwani mkataba uliopelekwa Bungeni una shida gani? Kuna Bandari yeyote mwekezaji kapewa kwenye huo mkataba?
 
Mkuu wewe umeelewa nini kuhusu liliojadiliwa na bunge na kupitisha kuwa sheria?

Kwa kukusaidia, yale makubaliano yaliopitishwa na bunge ndio unakuwa sheria na mkataba mama. Mambo yote mengine tutakayokubaliana hapo mbele, yatazingatia tulichokubaliana ktk mkataba mama. Na ukizingtia tulichokubaliana ktk mkataba mama ni upotolo mtupu
 
Mkuu wewe umeelewa nini kuhusu liliojadiliwa na bunge na kupitisha kuwa sheria?
Makubaliano ya Tanzania na Dubai kuhusu ushirikiano katika masuala ya uwekezaji na Bandari

Then ndo tunaenda kuingia mikataba kuhusu bandari au sehemu ya Bandari tunayofikiri tunaweza kushirikiana nao kwenye HGA

Shida iko wapi?
 
Shida ipo tulipokubaii kuwa hatutaweza kujitoa ktk mkataba huo hata kitokee nini na tumeshalikubali hilo. Wewe huoni kama hapo pana shida?
 
Makubaliano ya Tanzania na Dubai kuhusu ushirikiano katika masuala ya uwekezaji na Bandari

Then ndo tunaenda kuingia mikataba kuhusu bandari au sehemu ya Bandari tunayofikiri tunaweza kushirikiana nao kwenye HGA

Shida iko wapi?
Makubaliano kuhusu ushirikiano kuhusu masuala ya bandari. Haya yamepelekwa bungeni na kuwa sheria. Hiyo kwako ia sound vipi?
 
Kama unapinga bandari afu haukuandamana we ni mnafiki
 
Hakuna mtanzania anayepinga uwekezaji ktk bandari. Tunachopinga ni kuingia mikataba ya kisenge. Ningekuwepo nchini tz wakati wa hayo maandamano, ningeshiriki
 
Back
Top Bottom