Waziri Mkuu: Bandari imepewa DP-World kwa kuwa utendaji wa TICTS ni mdogo
Sawa,TICTS terms zake ni sawa na hizi?ilibadilishwa sheria?alipewa na Miundo mbinu ya reli?
 
Taja namba ya tangazo la zabuni, acha blah blah za kisiasa. Kila zabuni inayotangazwa hapa nchini lazima inakuwa ina namba yake maalumu ya utambuzi. Aidha, ni lazima pia inakuwa imesajiliwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Manunuzi ya Serikali. Sasa hiyo zabuni ya uendeshaji wa bandari ilitangazwa lini???Imesajiliwa lini??
Narudia tena kukukumbusha kwamba "no research no right to speak".
Jpm aliwahi kutangaza zabuni yoyote? Au mnamuonea mama tu kwa vile kawapa uhuru wa kuongea
 
Jpm aliwahi kutangaza zabuni yoyote? Au mnamuonea mama tu kwa vile kawapa uhuru wa kuongea
Ni kweli JPM alikuwa na mabaya yake, lakini kuuza nchi kwa wageni si miongoni mwa mabaya yake.
Haya eleza, wapi JPM aliwahi kuingia mikataba ya kuuza nchi kwa wageni bila kutangaza zabuni??
 
Ni kweli JPM alikuwa na mabaya yake, lakini kuuza nchi kwa wageni si miongoni mwa mabaya yake.
Haya eleza, wapi JPM aliwahi kuingia mikataba ya kuuza nchi kwa wageni bila kutangaza zabuni??
Kwani mikataba yeneyewe ulikuwa unaijua? Mana hakuna aliyekuwa anaruhisiwa kuliona hata bunge hawakuruhisiwa. It was one man show
 
PM asijivue nguo kujibebesha aibu za wengine, wacha kila mjinga aubebe ujinga wake.

Mkataba usio na ukomo unaompa mwarabu mamlaka ya kujitawala ndani ya ardhi yetu ni matusi, ni matusi mazito sio kwa kizazi chetu pekee, bali hata kizazi kijacho.
Kamwe hicho walichokifanya wakidhani kitakuwa sawa kwa watanzania hakitawezekana milele
 
Kila siku wanazungumza faida za uwekezaji wa DPW, faida hata TICTS wali ahidi, wanakomaa kulazimisha wananchi wakubali its guarantee 100% faida ipo kitu ambacho si kweli, watu wanauliza mkataba sio faida za uwekezaji.
Hivi kwanini wanajitoa ufahamu??
 
Serikali huenda zikibadilika kiufanisi mwaka mmoja baada ya mwingine, serikali yetu inao watendaji wazuri zaidi sasa hivi kuliko waliokuwepo miaka 30 iliyopita, hilo kwanza ulitambue.

Tunapoteza muda mwingi kwenye majadiliano mengi yanayoanzishwa na watu negative wakati DRC na Rwanda wakiwa tayari wameshaingia mkataba na hawa DPW.

Kama tunapenda nchi iwe kama Dubai na tuachane na akili za urasimu na wizi wa bandarini, kwani unatukwamisha na kutupotezea mapato mengi ambayo hutuacha na umaskini ule ule.

Mabadiliko au reforms anazoziendeleza SSH zilianzishwa na hayati JPM, zina maumivu yake lakini ni lazima tuyavumilie ikiwa tunataka kweli kwa vitendo tuwe sehemu ya nchi zilizo katika uchumi wa kati wa juu.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] eti utendaji mzuri[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]. Haki siku zikiachiwa bank statement za mabenki watu wote waone jinsi viongozi wetu wanavyoishi kwa perdiem na allowances na sio mishahara yao basi hii nchi itaingia vitani[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]. Ngoja tuwe wasomaji! Pesa zinatusuliwa juu kwa juu, hakii[emoji1787][emoji1787][emoji1787]. Nipo pale, siku tukikuza uchumi wa Tanzania kuzidi hapa tulipo.
 
Sio mda mrefu uliopita wakati vikao vya bunge vikiendelea tulishuhudia na tulisikia vilio vya wadau mbali mbali kuhusu madeni ya Serikali, hususan ukopaji wa Serikali na Ulipaji wa mikopo hiyo.

Walipohojiwa Tuliambiwa, tusiwe na wasiwasi, Serikali ipo makini-mikopo ni ya lazima kutekeleza miradi mikubwa, mikopo ni lazima na inasaidia Ujengwaji wa Barabara, madaraja, zahanati, mahospitali n.k kwa kifupi, ati ni kwaajili ya miundombinu...Wananchi hawakuridhika wakahoji tena ni kwanini tunaendelea kukopa wakati tunaona madeni yanakuwa makubwa tu na hata kulirudisha sakata lililomstaafisha Spika mstaafu J. Ndugai ambalo alisema tuna hatari ya kupigwa mnada na Serikali ikajibu Tusiwe na wasiwasi Rais SSH yupo makini yaani Serikali ipo makini, Benki kuu ipo makini na wataalamu wetu na Benki kuu na hata Taasisi au mashirika makubwa ya Kifedha na Uchumi Duniani vimewahakikishia kuwa bado tunakopeka na vilevile uwezo wetu wa kulipa madeni bado upo vizuri. Ikapita....wadau wakaja humu jamvini, wachumi wakatokea kwenye vyombo vya habari na kwingineko na kila utakayemsikia anasema kamavile "unajua wale wenzetu" wakiashiria Taasisi kubwa kama WB, IMF 'wakishasema tuna uwezo-kukopa na kulipa huwa hawakosei' tusijifanye wajuaji Watanzania kwani hata wenye mauchumi makubwa wanafanya hivyo.....fasti fowadi mwezi mmoja uliopita Taasisi na mashirika makubwa ya kifedha na uchumi, wakatoa kongole wakasema Bandari yetu Salama ipo Salama....yaani kuna Ufanisi wa hali ya Juu na tunazipiku hata zile nchi za Jirani....Ripoti ilisema

Sekta ya bandari nchini imefurahia kipindi cha ukuaji thabiti katika suala la maendeleo ya miundombinu na upatikanaji wa vifaa na teknolojia za kisasa kutokana na uwekezaji mkubwa unaofanywa na serikali ya awamu ya sita katika kuboresha sekta hiyo ambayo ni uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania.~WB
Tukirejea ya alichosema Waziri Mkuu ambaye ndiye Serikali ni..... kwanini wana kinzana na Taasisi na Mashirika ya Kifedha na Kiuchumia Duniani?

Sawa, huwa wanatudanganya, wana yao n.k sasa ni kwanini katika suala la Madeni na Ukopaji walishikilia ya Wataalam wetu, Benki kuu na hata "Waliondelea" "Wenzetu wale" "Walio na Uchumi mkubwa" kutuondolea mashaka na sintofahamu zake?

La Bandari tena:

Kwanini katika suali hili la Bandari wasituambie yale yale ya Walioendelea?? Kwamba Ufanisi upo, Uwekezaji Upo, Utendaji upo??

Nini kikubwa cha DPW kilichowafanya kukataa ripoti nzuri tu inayowaondolea TICTs uwalakini wanaodai umetokea?

Je, gawio lilikuwa dogo?(utajijiju) Wataalamu wetu wameamka? Mbona hawakuwasikiliza wale waliokataa Mikopo n.k?

Rejea alichosema Mbarawa akihitimisha uwasilishwaji wa hoja yake Bungeni kabla ya Upigaji kura na Hili la Waziri Mkuu kama linatoa mashaka au Kuoana!

Kifupi, Waziri Mkuu ameongezea changa la macho na kunaonekana kuwa kuna nuka Rushwa.

Kamata haaaaaoooo, Shika haaaao
 
PM asijivue nguo kujibebesha aibu za wengine, wacha kila mjinga aubebe ujinga wake.

Mkataba usio na ukomo unaompa mwarabu mamlaka ya kujitawala ndani ya ardhi yetu ni matusi, ni matusi mazito sio kwa kizazi chetu pekee, bali hata kizazi kijacho.
Kuna kipengele kwenye Mkataba ule unaowapa Kampuni hadhi ya Kiserikali, inaipa nguvu hata kampuni au watu ambao hawapo kuwa na nguvu za Kiserikali. Yaani hata makampuni ambayo hayajasajiliwa na watu ambao hawajazaliwa!

Wakoloni wametumia udhaifu wa Mwafrika na Imani zake, wamejipatia Tunnel if I may, kuja kututawala tena. Yaani Ikitokea Mwingereza, au Mmarekani au yeyote yule kufikia dau kubwa la kuinunua DPW basi atakuwa ameinunua na kushikilia mapumu serikali mbuyetu.

Hapana. Warudi kikangaoni wakaange tena. Hili walisitishe. Bunge Lina uwezo huo. CCM ina Uwezo huo.

Wako wapi walinda Katiba?
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] eti utendaji mzuri[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]. Haki siku zikiachiwa bank statement za mabenki watu wote waone jinsi viongozi wetu wanavyoishi kwa perdiem na allowances na sio mishahara yao basi hii nchi itaingia vitani[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]. Ngoja tuwe wasomaji! Pesa zinatusuliwa juu kwa juu, hakii[emoji1787][emoji1787][emoji1787]. Nipo pale, siku tukikuza uchumi wa Tanzania kuzidi hapa tulipo.
Hii ni vita kubwa sana. Inajumuisha TICTS na GSM, hao wote wawili ni matajiri waliotajirikia ineffeciency ya bandari yetu, hawawezi kukubali mfumo mpya wa uendeshaji utumike mahali pale.

Wanamwaga pesa kwa wabunge, wanamwaga pesa kwa wanasheria kina Mwabukusi, wanamwaga pesa kwa wana mitandao wa humu JF, wanamwaga pesa kila mahali wanapoweza kufika ilimradi DPW asiweze kuleta mabadiliko pale bandarini.

Wanajua huo utakuwa mwisho wao wa kupata pesa kwa njia haramu za utakatishaji.

Hii ni vita nzito lakini maji ukiyavulia nguo huna budi kuyaoga.
 
ANAANDIKA BABA ASKOFU BAGONZA (PhD)

BANDARI: Tumefikaje? Tutatokaje?

Mjadala wa “kuuzwa”, “Kubinafsishwa”, “Kukodishwa” au vyovyote ilivyofanywa, umeonyesha nyufa za hatari katika nyumba yetu TANZANIA. Nitaje kadhaa:

1. Rushwa

Rushwa bandarini ndiyo imesababisha bandari ifanywe inachofanyiwa. Wakiishapeana rushwa, serikali inakosa mapato, mizigo inachelewa, inapotea, na bandari limekuwa pango la majizi.
Swali ni je, kila penye rushwa tuuze? Tubinafsishe? Tukabidhi sekta binafsi? Je rushwa ikishika kichwani na moyoni? Tujadili ufa huu bila jazba. Rushwa itavuruga wawekezaji wapya.

2. Umoja na Utaifa

Mjadala umeonyesha, wanaodai wanaujenga/kuutetea umoja na utaifa, ndio wanaubomoa. Wanaoonekana kuubomoa, ndio wanaujenga. Bandari imeujeruhi umoja na utaifa wetu. Hii ina gharama mbeleni. Tumejuana, tuishi kwa tahadhari.

3. Udini na Siasa Zetu

Viongozi wetu wana dini zao. Sitamani kuchagua kiongozi asiye na dini. Tatizo tunalo viongozi wa dini. Tunawakosoa viongozi wa dini ileee na kupongeza wa dini zetu. Au tunanyamaza mpaka tupigwe sindano ya kupongeza badala ya kushauri. Inapendeza kumkosoa na kumshauri kiongozi wa dini yako japo haizuiwi kumkosoa wa dini isiyo yako.

4. Ujuzi wa Sheria na Uchumi.

AJABU: Wanasheria walioongea tukaelewa ni wachache sana. Walio wengi ujanja wao unaishia Kisutu.
Wanauchumi wetu ujanja wao unaishia Kariakoo. Mkataba huu hawauelewi na wakiuelewa hawatuelezi tukaelewa. Huu ni ufa wa hatari.

5. Bunge

Hili lingebinafsishwa kabla ya bandari. Walichoongea bungeni sicho wanachoongea mitaani na kwenye baa. Wanamdanganya rais kuwa wanamuunga mkono wakati wamebeba mishale ya kumwangamiza. Mjadala wa Bandari umefanywa mgumu na bunge letu.

6. Serikali

Mjadala na tabia za watu vimeonyesha serikali hii si ya rais Samia hata kama kaiteua yeye. Hii ni mchanganyiko wa serikali zilizopita. Ina utii uliogawanyika - kiapo kimoja Chamwino na vingine huko makaburini, Msufini, na Butiama. Serikali bila “Uwajibikaji wa pamoja” ni sawa na genge la wasela. Ufa huu unadai tuanze upya.

7. Rushwa part 2.

Katika Mjadala wa Bandari tumesikia malalamiko ya rushwa za aina tatu: Wanaonufaika na uzembe wa bandari wakikazana kukwamisha mkataba; DP World wakikazana mkataba upite; na wanaoitwa wazalendo wasio wa taka DP World wala wazembe wa bandari LAKINI bila kutoa suluhisho. Ufa huu ni mgumu kuushughulikia bila kuchelewesha mkataba na kusikilizana kwanza.

8. Rais Wetu

Rais SSH ni wetu sote. Ni muhimu kama taifa kumkinga na mipasuko inayotokana na mjadala huu. Kuna maisha baada ya mjadala wa bandari. Yeye analo jukumu la kutuongoza sote na makundi yote mpaka tuvuke. Subira itatufundisha kuliko haraka. Ufa huu unazibwa kwa kusikiliza na kuchukua hatua.

9. Miafaka yetu

Mjadala huu umejeruhi miafaka yetu na kufukua baadhi ya makaburi. Baadhi ya makaburi tumekuta marehemu hawajaoza.
Katiba, maridhiano, Muungano, maelewano ya kidini, uhuru wa maoni na mamlaka ya wananchi bila bunge ni mambo muhimu sana katika kuziba nyufa zilizojitokeza.

10. Upinzani wetu

Mjadala unaonyesha aina mpya ya upinzani. Ndani ya chama tawala na serikali kuna upinzani mkali dhidi ya suala la bandari. Hii ni afya kwa nchi lakini hatari kwa utawala. Vyombo vyetu vijifunze kutotumia nguvu kupambana na maoni. Bora upinzani wa hadharani kuliko wa moyoni.

Nawashukuru wooote wanaochangia kwa hoja na kutuelimisha tulio wajinga wa sheria, uchumi, mikataba ya kimataifa na katiba yetu.
 
Akielezea suala linaloendelea kuhusu mkataba wa DP-World na Tanzania ametoa sababu kuwa ni utendaji kazi mdogo wa TICTS ambao umesababisha meli nyingi ziwe zinashushia mizigo Lamu, Mombasa au Afrika kusini hali ambayo imepunguza wateja wa Bandari ya Dar es salaam.

Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa amesema utendaji mbovu wa bandari unasababisha meli zitumie muda mwingi bandarini ambapo gharama ya meli kubaki bandarini huingia mfanya biashara hivyo bidhaa kuwa ghali mtaani. Amesema kwa sasa meli hutumia hadi siku saba kwa mzigo kupakuliwa.

Aidha, amesema awali TPA ilitambua utendaji mbovu na kumpa TICTS mkataba kwa miaka 20 lakini hakukuwa na utendaji mzuri ambapo mkataba huo uliisha 2017 na baadae aliomba kuongezewa miaka mitano ambayo imeisha 2022 na bado hakuweza kuleta vifaa vipya vya kuhudumia bandari.

Waziri Mkuu ameonesha suala la mkataba wa DP-World litarahisisha upakuaji wa mizigo.

Watanzania wametaka maelezo baada ya kuwa na utata katika baadhi ya vipengele vya mkataba huo ambao kwa kiasi kikubwa serikali na spika wa bunge wamekuwa wakivitolea maelezo.

Mheshimiwa Waziri Mkuu kikulacho ki ungoni mwako. Maadui mnao karibu kabisa na serikali, ni hao hao wanaotoa pesa za michango za kujenga misikiti na makanisa.

Hao hao kina GSM, ndio wabaya wenu wakubwa. Wanajaza watu humu wanaoshinda wakianzisha mada za kuwatusi, kuwakejeli na hata zile zenye mtazamo wa kuvunja nchi.
 
Akielezea suala linaloendelea kuhusu mkataba wa DP-World na Tanzania ametoa sababu kuwa ni utendaji kazi mdogo wa TICTS ambao umesababisha meli nyingi ziwe zinashushia mizigo Lamu, Mombasa au Afrika kusini hali ambayo imepunguza wateja wa Bandari ya Dar es salaam.

Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa amesema utendaji mbovu wa bandari unasababisha meli zitumie muda mwingi bandarini ambapo gharama ya meli kubaki bandarini huingia mfanya biashara hivyo bidhaa kuwa ghali mtaani. Amesema kwa sasa meli hutumia hadi siku saba kwa mzigo kupakuliwa.

Aidha, amesema awali TPA ilitambua utendaji mbovu na kumpa TICTS mkataba kwa miaka 20 lakini hakukuwa na utendaji mzuri ambapo mkataba huo uliisha 2017 na baadae aliomba kuongezewa miaka mitano ambayo imeisha 2022 na bado hakuweza kuleta vifaa vipya vya kuhudumia bandari.

Waziri Mkuu ameonesha suala la mkataba wa DP-World litarahisisha upakuaji wa mizigo.

Watanzania wametaka maelezo baada ya kuwa na utata katika baadhi ya vipengele vya mkataba huo ambao kwa kiasi kikubwa serikali na spika wa bunge wamekuwa wakivitolea maelezo.


Hivi Kwa upande wa TICTS hakuna ripoti inayoonesha sababu why walishindwa kufikia ufanisi
 
Hivi Kwa upande wa TICTS hakuna ripoti inayoonesha sababu why walishindwa kufikia ufanisi
Hakuna cha Ufanisi wala cha Utendaji. Ukifuatilia linki za hapo juu lazima ujiulize, kulikuwa na sababu gani zingine? Nchi imetumia karibia ya Trillioni 2.2 TShs katika maboresho ya Bandari karibia zote Tanzania na fedha nyingi ni mikopo ambayo marejesho ya uwekezaji huo anaanza kufaidi DPW wakati sie Watanzania tunaenda kulipa madeni hayo kila kukicha....inaendlea taarifa hiyo na kisema....👇

Hatua hizi zote zimeongeza kwa kiasi kikubwa ufanisi wa utunzaji wa mizigo katika bandari za TPA ambazo zinaendelea kuvutia idadi kubwa ya wateja ambao huchagua kusafirisha mizigo yao kupitia bandari za Tanzania.

Yaani miezi miwili mitatu baadae ndio hakuna Ufanisi? Hakuna Utendaji?


 
Hata Serikali yenyewe ya CCM haina ufanisi aka ufanisi mdogo ni vyema nayo ingeuzwa tu kwa waMarekani.

Kama suala ni ufanisi, Mh PM lini CCM ilikuwa na ufanisi? mbona hamkuwahi kufikiria kuibinafsisha au kuiuza kabisa CCM yenyewe?
 
Ukisikiliza speech na utetezi alioandikiwa na wanasheria wa serikali.

Kama washauri wenyewe kile walichompa ndio best defence. Unapata picha kwanini kwenye mikataba ya manunuzi yenye variable consideration kama order ya ndege tunaishia kuwekewa vipengele vya kulipa ziada, halafu baada ya wanatafuta mbuzi wa kafara ndani ya serikali.

What a pity
 
Back
Top Bottom