Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Mbarawa azungumza kuhusu uwekezaji wa Bandari

Hamza ni mzanzibar anadhana na wabara ni kama wazanzibar ni wavivu kusoma
 
Tatizo haliko kwenye mwekezaji, tatizo liko kwenye utata wa mkataba. Kwa muda gani? Bandari zote Tanganyika,au baadhi ya bandari? Kwa Nini iwe bandari za Tanganyika tu na kuziengua za Zanzibar? Waziri afafanue utata wa mkataba, wawekezaji tunawataka.
 
Hamza:Mkataba haukupelekwa kimwendokasi,ulifuata utaratibu
 
Hamza:Serikali inaamini Mkataba/makubaliano yapo sahihi,
 
Lugha ya Kiswahili inatupa ukakasi kwani haitoi tafsiri sahihi ya huu Mkataba/makubaliano
Treaty v Contract!?
 
Watu wamegoma kuwaachia,,Watz wamekuwa ruba,,,Wamekuwa wakali na vya kwao na si dhambi wanastahili sana kuvipagania kwa nguvu na kwa juhudi zote,,,,Viongozi wetu ni vizuri wangekuwa wanasoma alama za nyakati,,Kuishi kwa kujali na kuthamini nyakati ni jambo moja Bora Sana na la msingi mnoo katika kuishi na kuyajenga maisha Yaliyo Bora!!
 
Uharaka kwa kukimbilia bungeni ili Bunge kutoa Azimio tarehe 10 June 2023 bila kutoa nafasi wananchi na wadau kujadili suala la bandari



TOKA MAKTABA barua ya Mwaliko kwa wadau

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE LA TANZANIA
Simu: +255 026 23222761-5
Fax No. +255 026 2322624
E-mail: cna@bunge.go.tz
TAARIFA KWA UMMA
Ofisi ya Bunge,
S.L.P. 941,
DODOMA.

Kamati ya Pamoja (Joint Committee) ya Bunge ya Miundombinu na ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) inawaalika wadau kutoa maoni kuhusu Azimio la Bunge kuhusu Mapendekezo ya Kuridhia Makubaliano kati ya Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai
kuhusu Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii kwa ajili ya Uendelezaji na Uboreshaji wa Utendaji Kazi wa Bandari Tanzania la Mwaka 2023(Intergovernmental Agreement – IGA , between the United Republic of Tanzania and the Emirate of Dubai concerning Economic and Social Partnership for the Development and Improving Performance of Ports in Tanzania).

Mkutano wa kupokea na kusikiliza maoni ya wadau (Public Hearing) utafanyika siku ya Jumanne tarehe 06, Juni saa 7:30 mchana katika Ukumbi wa Msekwa ‘D’, Ofisi ya Bunge, Jijini Dodoma.

Kamati inawaalika watu wote wenye maoni kuhusu Azimio hilo kufika na kuwasilisha maoni yao kabla haujapelekwa katika hatua nyingine.

Vilevile Kamati itapokea maoni kwa njia ya Posta au Barua pepe kwa anuani ifuatayo:-

Katibu wa Bunge, Ofisi ya Bunge,
10 Barabara ya Morogoro
S.L.P. 941,
40490 Tambukareli
DODOMA.
Baruapepe: cna@bunge.go.tz na kamati@bunge.go.tz

Azimio hilo linaweza pia kupakuliwa katika tovuti ya Bunge,
www.bunge.go.tz. Aidha, unashauriwa kuwasilisha jina lako kupitia barua pepe tajwa endapo utapenda kuwasilisha maoni yako kwa kuzungumza kwa ajili ya
hatua za kiutawala.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa,
Ofisi ya Bunge,
S.L.P 941,
DODOMA
 
Watanzania wamechafukwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…