Wengi wanaotaka wake zao wasifanye kazi wana upeo mdogo wa kufikiri halafu ni wabinafsi

Ndio nakuuliza unaweza kujenga Ukweni na kimshahara chako ambacho hata wewe mwenyewe hakikutoshi?
Kwa nini ujipendekeze kujenga ukweni, huku mama mkwe wako anawatoto wakiume aliowazaa kama wewe?.

Mambo mengine niyaziada hayatakiwi kuyatilia maanani, au Dada yako, mdogo wako wakike akiolewa ungependa shemeji yako ndio amjengee mama/Baba yako?.
 
Kwa nini ujipendekeze kujenga ukweni, huku mama mkwe wako anawatoto wakiume aliowazaa kama wewe?.

Unaona sasa ulivyo mbinafsi.
Mtoto ni mtoto awe wakike au wakiume.
Na wote wanahaki sawa kwa mzazi.

Wewe ukizaa watoto wakike wote hawataki wa na wajibu wa kukutunza?
 
Hukutakiwa kuongelea habari za ndoa kama hujui majukumu ya mume.

Majukumu ya mume na mke ni yaleyale kwa sababu wao ni mwili mmoja. Au wewe unazungumzia wale wanawake mnaowanunua na kuwaita mke huku mkiwageuza vijakazi na misukule yenu.
 
Unaona sasa ulivyo mbinafsi.
Mtoto ni mtoto awe wakike au wakiume.
Na wote wanahaki sawa kwa mzazi.

Wewe ukizaa watoto wakike wote hawataki wa na wajibu wa kukutunza?
Mwanamke akiolewa ukoo automatically umepungua, na mwanaume akioa basi ukoo umeongezeka. Ukishatambua Hilo mambo mengine hayatokusumbua.

Nawakifanya hivyo nijambo laziada ambalo kwangu hatawasipofanya sintowalaumu.
 
Dunia inabadilika inabidi majukumu yatafakariwe upya.

Mfano tu uwepo wa vitu kama mashine za kufulia, kuoshea vyombo kunarahisisha mambo

Mtasema ni ghali lakini hizi mashine zitakuja kuwa kawaida kama tv na pasi zilivyo sasa tofauti na zamani

Narudia tena, dunia inabadilika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…