Wengi wanaotaka wake zao wasifanye kazi wana upeo mdogo wa kufikiri halafu ni wabinafsi

Duh! Acha mawazo haya mkuu! mawazo huumba, majanga yakitokea tutajua njia ya kuyatatua lakini tusitandikie godoro matatizo, Ishi leo yako achana na kesho.
Hahaha,
Hapana mimi huwa napenda kuongea uhalisia wa vitu Ninavyoishi navyo.

Yupo mama alimsaidia mume wake alikuwa kitandani hajiwezi, huyu mama alikuwa na kimgahawa chake anapika na anatengeza bites.
Mume aliugua sana mke alikuwa anapanda na kushuka mpaka akaja kupona.

sasa nilikuwa nafikiria sentensi yako ya kwamba pesa ya mwanamke ni ya mwanamke tu na si ya familia.

Mimi na Mke wangu tunasaidiana kulipa ada ya mtoto na hajawahi kuona shida kutoa pesa yake kuhudumia familia
 
Daah hayajakukuta wewe! Tuulize tuliopo huku maofisini ndio tunajua wake za watu wanayofanyiwa!

1. Utajiskiaje kuona mke wako anapapaswa tako na wafanyakazi wenzake?

2. Utajiskiaje mke wako anakwambia ana semina ya wiki tatu mkoa flani? Tena mbaya zaidi anakwambia kaenda na bosi wake..

Kwenye mada hii nakupinga aisee!

Sent from my SM-A515F using JamiiForums mobile app
 
Dhana ya 50/50 wapewe furusa sawa, baada yakupewa furusa hizo Kwa upendeleo hao wanawake angalia impact yake ni nini katika msingi wafamilia ya baba, mama na watoto.
umenena vyema!

sasa tupe takwimu ya unachosema.
Yaani mtu kuomba ajue kusoma na kuandika baada ya miaka mingi mtoto wakike kuwa apelekwi shule unaona anataka kujilinganisha na wewe?

Una tofauti gani na mkoloni aliyewachapa babu zetu fimbo na kuenda kuwauza?

leta takwimu sasa.
 
Yaani uhudumie wazazi wa mkeo na ndugu zake hayo ndiyo majukumu ya mme?

Unawajibika namba 1 kwa familia uliyoianzisha wewe yaani wewe, mkeo na watoto wenu.

Hao wengine ni ziada kama unacho na una moyo unatoa lakini siyo lazima
 
😂
Wake za watu ambao hawapo maofisini huwa hawafanyi hivyo?
Wote wanao- cheat ni wa ofisini tu?
 
Kuoa mke mfanyakazi eti kisa maisha kusaidiana ni woga wa maisha.
Kama una uhakika wa kipato na umewekeza kwenye vitu ambayo unexhausted woga wa maisha unatoka wapi?
Nimefanya kazi huu mwaka wa 9 nakaribia katika ofisi za umma.
Wake zenu wanawazalia watoto ambao si wenu. Kapime DNA halafu uje uandike tena kwa ujasiri hapa
 
Yeyote anayebisha muulize hatamani binti yake aje kuwa Rais, spika, waziri, mkurugenzi kama wanawake walivyoshika hatamu kwenye hii awamu? Anataka binti yake awe goli kipa tu that's it? They must be dumber than bricks 🧱

Watakuita mlamba lips.
Mtu mkewe hata kumhudumia hawezi. Hakumbuki mara ya mwisho kumnunulia nguo ni lini
Nyumbani kwake kunywa maziwa ni anasa wakati inatakiwa iwe sehemu ya mlo wa kawaida. Alafu anajifanya ati yeye ni mwanaume asiyehitaji usaidizi. Uone kama sio mgonjwa wa akili huyo
 
Tafuta hela kijana mwanake kazi yake kulea familia. Ukishaona wewe na mke wako wote mnaamuka saa 11 asubuhi kwenda kupalangana basi wewe huna mke ila una partiner kwenye kuendesha maisha.
Yaani wewe huna uwezo wa kuitunza familia na kwa msingi huo uanaume wako ni wa mashaka. Kimsingi hukupaswa kuoa.
 
Uyu ajakua ngoja yamkute kapata kidemu Cha chuo washapanga mipango wajenge kwa pesa ya mwanamke
Anaona Me yeyote aoaye Mke wa nyumbani ni mshamba bila kujua ni muda tu utafika atapigwa tukio hadi aache ujuaji wa hivi viumbe.

Ubinadamu ni kazi/Humanity is a work.
 
Ktk jamii yoyote classes are inevitable. These cases of gender equality and equity put them aside. Human beings cannot live homogeneous, never ever, suala la kuendesha maisha ktk ndoa ni utaratibu wa mtu na mke wake siyo kufuata mkumbo au kushauriwa, "because what is good to you cannot be good to all". Tatizo vijana wengi hasa hawa wasomi uchwara wanaotembea na vibegi mgongoni na kuvaa visuruali na vishati vya kubana wameathiriwa na Beijing agenda. Pole sn.
 

Wewe mkeo ambaye yupo nyumbani pima watoto DNA alafu uje utoe ripoti hapa.
Mnashindwa Kuelewa maamuzi na tabia ya mtu ni tofauti na kazi.

Mwananmke anaweza akafungwa jela na akapata Mimba
 
Yeyote anayebisha muulize hatamani binti yake aje kuwa Rais, spika, waziri, mkurugenzi kama wanawake walivyoshika hatamu kwenye hii awamu? Anataka binti yake awe goli kipa tu that's it? They must be dumber than bricks 🧱
Chukua idadi ya wanaweke hao waliopo kwenye hizo nafasi kisha gawanya Kwa idadi ya wanawake wenye vigezo vyakupewa hizo nafasi kisha zidisha 100%, Kisha uone binti yako anaasilimia ngapi zakupata hiyo chance, kisha mpiganie. Kama wewe watamani hivyo, waulize waume zao hao wenye hizo nafasi wanajivunia wake zao kushika hizo nafasi?.

Kisha baada yahapo pia utambue msingi wa mada tunazingumzia mke wako/wangu. Na sio binti yangu/wako.
 

Walipata uraias, uspika kutokea nyumbani?

Unajua Samia kaanza siasa lini? Unajua background yake? Unajua background ya Tulia? Unadhani walifika Hapo bila kazi zingine?

Wake za marais kuacha kazi ni protocal tu, wanapewa majukumu ya kinchi na ndo maana wanalipwa mishahara na sheria imepitishwa ya kulipwa mafao as well.

Wafungieni watoto wenu ndani muone kama watafika popote wataishia kutumika tu.
 

Ndio ujibu hoja.
Unaweza kukarabati na kujenga Ukweni?au kusomesha ndugu za mkeo?
Kama unaweza kutimiza majukumu ya mkeo ikiwemo kuhudumia wazazi wake basi unahaki ya kumzuia asifanye kazi.

Lakini elewa kuwa hakuna mtu aliyefanokiwa hata mmoja duniani ambaye mkewe ni mama wa nyumbani asiyefanya kazi ya uzalishaji
 
Tulishakubaliana wazazi wahudumiwe wakifikisha miaka 60, sasa haya ya kujenga ukweni yanatoka wapi?

Ndio wakifika hiyo 6o unaweza kuwahudumia na kuwajengea au kukarabati makazi yao ikiwa tuu mahitaji ya nyumbani kwako yamakushinda na pesa ya maziwa tuu unaona ni kazi?
 
Mada nimke wako/wangu kaka Robert nasio Binti yangu/wako. Wewe kama mzazi unatamani Binti Yako awe raisi/waziri/mkurungezi nisawa Sasa muulize mume wake anafuraha nabinti yako kuwa na hivyo vyeo ndio msingi wahoja ulipo katika ngazi yafamilia ya baba/mama na watoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…