Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Tumefikia mahali ambapo hali ya wizi na ufisadi wa fedha za serikali inatisha. Si Tamisemi tu, bali hata vyombo vya usalama na taasisi za serikali ugonjwa ni huo huo. Udanganyifu katika mifumo ya malipo imekuwa ndio habari ya mjini, kuanzia tozo za kupaki magari, fine za trafiki, miamara ya serikali za mitaa na serikali kuu, mashirika ya umma nk, ni wizi, wizi, wizi tu!
Watu siku hizi hawana uoga tena. Kwa wale waliompenda Magufuli na ambao hawakumpenda, wote lazima tukiri kwamba katika uongozi wake watu waliogopa kufanya wizi kama huu unaofanyika sasa.
Sasa tujiulize, kwa nini watu hawana uoga tena wa kufanya ufisadi na wizi hadi kufikia kiwango hiki?
Bila aibu wala upendeleo, twapaswa kukiri kwamba kuongezeka sana kwa wizi na ufisadi chini ya Raisi Samia kunachangiwa na watu kuona kwamba (perception) kuanzia ofisi ya Raisi mwenyewe, mawaziri nk, kumekuwa na viongozi na hata mawaziri wapigaji wengi tu. Kama hatutaoneana aibu, basi lazima tuseme uongozi wa Raisi Samia ndio tatizo na ndio unafanya watumishi wa serikali, mashirika na hata vyombo vya usalama kuwa na udiriki wa kuiba kwa kiwango hiki, jambo ambalo tunakiri wasingethubutu kufanya wakati wa Magufuli.
Wengi wetu tunaona kwamba Raisi Samia mwenyewe alihalalisha wizi wa fedha za serikali pale alipotoa kauli kwamba kila mtu atakula kwa urefu wa kamba yake, kauli ambayo japo anajua imeleta utata, hajawahi kuirekebisha. Raisi Samia anapaswa aelewe kichocheo kikubwa cha wizi uliopo ni perception kwamba kama Raisi amekuwa akitoa fursa nyingi za kutajirisha ndugu zake wa karibu na mbali (nepotism), na sasa hata mawaziri wake na watu wengine kwenye mashirika na serikali kuu na za mitaa wanaona ni halai kujitajirisha kwa kuiba fedha za serikali. Hivi inafikia wakati wowote Raisi Samia anajiuliza utajiri wa kasi wa mtoto wake Abdul unavyotazamwa na Watanzania, kuanzia mawaziri hadi watu wa serikali za mitaa na kwingineko, na unakuwa na athari gani kwa uaminifu wa viongozi na watu walio na fursa za kuiba fedha za serikali? Kwa nini watu wawe waaminifu wakiwa na perception kwamba hata Ofisi ya Raisi nchini haya mambo yanafanyika?
Watanzania wote wamesikia juu ya yale Makonda aliyofunua kule Arusha, na Watanzania wote wanatambua aliyofunua Makonda ni tone dogo sana katika bahari ya wizi wa fedha za serikali unaofanyika nchini kwa sasa. Leo mpeleke Makonda Morogoro, Mbeya, Iringa, Tanga nk, atakutana na yale yale anayoibua Arusha - wizi, wizi, wizi!
Sasa ni wakati wa kikiri kwamba tatizo la wizi nchini ni tatizo linalotokana na udhaifuu wa Ofisi ya Raisi katika kusimamia nidhamu ya fedha na uongozi nchini, na imefikia mahali hakuna mtu anaemuogopa Raisi Samia katika kufanya ufisadi na kuiba. Jambo mojawapo la kisaikolojia, ni kwamba inawezekana watu hawana uoga na kuiba chini ya uongozi wa Raisi Samia kwa sababu hawamwogopi raisi mwanamke, au labda wameona hana ukali au weupe wa kukemea wizi wa fedha za serikali, au kwa sababu tu ya perception kwamba hata Ofisi ya Raisi kuna hizi tabia za kujinufaisha kibinafsi na fedha za serikali.
Sasa je, suluhisho ni nini? Je, suluhisho liko ndani ya CCM au labda chama cha upinzani kuiondoa CCM madarakani?
Ukiniuliza maoni yangu binafsi, nitakuambia sioni ndani ya CCM kiongozi ambae anaweza kuwa mbadala wa Raisi Samia na kuweza kurudisha nidhamu ya fedha za serikali. Niambie, nani? Wale wote wanaotamani kushika nafasi ya uraisi, wote ukiwaangalia unaona kabisa huyu hawezi, na wala yule hawezi. Sioni mtu ndani ya CCM mwenye uwezo wa kurekebisha hali tuliyofikia Tanzania. Nani, Mpango? Makamba? Mwigulu? Majaliwa? Biteko? Jafo? Bashungwa? Hakuna hata mmoja, wote wameshaambukizwa kirusi cha kutoweza na kuweka maslahi ya chama na ukada mbele ya maslahi ya Tanzania.
Basi je, suluhisho liko nje ya CCM kwenye vyama vya upinzani? Tundu Lissu? Zitto Kabwe nk? Inawezekana, lakini ni jambo ambalo haliwezekani kusema Lissu au Ziito kwa mfano, wachukue nafasi ya Uraisi na nchi iwe chini ya uongozi wa vyama vyao. Hilo halitatupeleka popote.
Maoni yangu ni kwamba imefikia wakati tufikirie kuuna serikali ya mseto ambayo itajumuisha vyama vyote vya upinzani, ili tujipange upya. CCM peke yake, au Chadema peke yake, au ACT wazalendo peke yake, hawezi kututoa hapa tulipo. Lazima tutafute namna ya uwajibikaji wa serikali kwa kuwa na serikali ya mseto ambayo hivi vyama vya siasa nchini vitalazimika kufanya kazi pamoja kwa maslahi ya Tanzania, hapo tunaweza kufanikiwa.