Pre GE2025 Wizi na ufisadi wa fedha za serikali uliokithiri katika awamu hii, suluhisho haliko ndani ya CCM wala upinzani kuwa mbadala wa CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ila nadhani wanaotisha kwa ujambazi bila aibu. Unakuta polisi trafiki kapaki prado yupo hapo barabarani, hahahaha unajiuliza ila ene way kila mtu urefu wa rope
Hapa kuna ukweli. Kwa mshahara wa laki sita utawezaje kununua Prado? Wanasingizia tumekopa saccos, lakini utakuta mtu mwenyewe ana miaka 5 kazini, kwa kiwango hicho na muda huo hawezi kukopa pesa inayotosha kununua Prado. Kamba yao wameikita barabarani na ina urefu wa kutosha.
 
Mtazunguka sana kutafuta wa kumsukumia jumba bovu hili

Lakini ukweli unabaki ni mmoja tu ni lazima apatikane mtu mwenye elements za Udikteta na alindwe sana na atawale kwa muda usiopungua miaka 20 🙄👁

Hapo ndipo Nchi itakaa kwenye mstari ulionyooka 🙄👁

Magufuli alishaonyesha kuwa Inawezekana 😳🙄🙄👁
 
. Kuzuia kitu kinachoitwa Rushwa inahitajika mlolongo mrefu sana ulio na sheria kali za nchi... Kuanzia wananchi wenyewe mpaka serikali kwa ujumla.

. Wizi wa mali za umma hauji hivi hivi, lazima huwa kuna chazo.
1. Gape la ajira kwa wananchi
2. Sheria mbovu
3. Nchi kukosa plan ya maendeleo
 
Punguza unafiki. Nani ana muda wakumuongelea marehemu. Mtu kafa miaka mitatu iliyopita, wewe unailaumu kwanini haongelewi
 
Tunamshukuru Mungu kwa kutuondolea yule kiongozi muovu bila damu kumwagika. Uchu wake wa madaraka ndio uliochangia kwa kiasi kikubwa kuua checks and balances ndani ya nchi hii. Kama sio yeye aliua demokrasia ya watu kuhoji, Leo hii wenye nguvu ya kuhoji Bado wangekuwepo. Ametuwekea bunge la chama kimoja ili alitumie kuiweka madarakani zaidi ya miaka 10. Alikuja kuparalize mifumo na kutuletea habari za one man show.
 
Chumvi ikiharibika haina dawa.
Huwezi kuinusuru nchi kwa kuendelea kuikumbatia hiyo ccm iliyokwisha haribika. Matendo ya ccm ndiyo yametufikisha kwenye mkwamo sugu. Lazima tutafute na kukubali mbadala
 
Ccm lazima iondoke kwanza ili nchi ianze upya.Lakini pia ili tutoke hapo kwenye mkwamo lazima tuondokane na tabia yakutegemea mtu mmoja kama mwamuzi wa kila kitu.Wenzetu walishaondoka uko wako kwenye kujenga mifumo thabiti inayojisimamia ndo maana wanaendelea ila sisi bado tunawaza mtu mmoja sahihi ambaye ata ukimpata anaweza kufa au kubadilika muda wowote.
 
Chumvi ikiharibika haina dawa.
Huwezi kuinusuru nchi kwa kuendelea kuikumbatia hiyo ccm iliyokwisha haribika. Matendo ya ccm ndiyo yametufikisha kwenye mkwamo sugu. Lazima tutafute na kukubali mbadala
Mbadala bila CCM maana yake ni muungano wa vyama au chama cha upinzani kimoja, na kuondoa(purging) wale wote walio tainted na CCM. Tunaweza kuharibu hata zaidi, kwa sababu ukifanya hivyo kunakuwa na tendency ya kuleta watendaji wapya wasio na uzoefu katika mifumo ya serikali. Kosa hili walifanya Zimbawe na South Africa na kuharibu sana uimara wa serikali na hata uchumi. Ndio maana nikasema suluhisho ni serikali ya mseto
 
Serekali ya majimbo. MTU akivuruga jimboni kwake anapambana na watu wake. Na hii italeta ushindani katika maendeleo.
Hii nayo ni point nzuri sana, ila tatizo ni kwamba kutakuwa na majimbo ambayo yana nafasi kidogo sana za kiuchumi, kwa mfano kusini mwa Tanzania nk. Itabidi umakini ufanyike kusawazisha. Lakini kubadili mfumo uliopo na wa central government kuingia mfumo wa majimbo, decentralization, inarahisisha sana kusimamia serikali katika dimension ndogo kwa ufanisi zaidi.
 
Umeongea vitu vya maana sana. Serekali imemshinda huyu mama. Apumzike TU!
Nadhani kuna tatizo kubwa zaidi ya huyu mama; serikali imewashinda CCM, hawana la kufanya tena kwa sababu ya cancer iliyo ndani yao katika mazingira ambayo wananchi wasio na upevu wa kisiasa wanaona hakuna mbadala wa CCM. Leo CCM hata wakiuza Mlima Kilimanjaro kwa Kenya, bado kuna watu watasifia huo uamuzi na wanaweza kushinda uchaguzi mkuu.
 
Watu wapo ila wamemezwa na mfumo wa kishetani. Huwezi kuwa kwenye kundi la mafisadi 20 halafu ukaanza kuleta ideology za kizalendo watakumaliza mapema mno.

Ratio ya wazalendo versus wasaka tonge tunaweza weka assumption ya 10:90 na ukiangalia hapo nguvu ya hao 90 iko kwa wenye madaraka. Unafanyaje mwisho wa siku, hata hao 10% wataishi maisha ambayo nafsi zinawauma ila hawana jinsi.
 
Andiko lina ukweli mwingi! Suluhisho ndilo bado la kufikiria!
Anko Magu ninaamini aliharibiwa na haya majambazi ama kwa uchawi au kifitina tu! Ninaungana na chalamila kuwa msaidizi namba moja wa Anko magu alihusika kwenye kifo chake!
Hayo ni dhahiri haiwezekani mtu aseme anaponya nchi huku akiiuza na kuifisidi kwa kasi ya ndege!
Suluhisho ni moja!
Tunahitaji Ibrahim Traore mmoja tu ayashughulikie haya majambazi kwa nguvu zote na kujenga hofu na nidhamu! Baasi Utawala wa kiraia uje baadaye! basi kwa sababu hata anko magu mbona aliipeleka nchi kijeshi kabla hayo majizi hayajafitinisha?
 
Kwa kweli Tanzania inahitaji Traole wake, huo ni ukweli usiopingika. Huenda yupo tu huko kwa wajeda, anaangalia tu kinachoendelea
 
Hao wau wako wapi, lazima wapatikane katika mfumo unaoonekana, la sivyo hawawezi kutusaidia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…