Pre GE2025 Wizi na ufisadi wa fedha za serikali uliokithiri katika awamu hii, suluhisho haliko ndani ya CCM wala upinzani kuwa mbadala wa CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mtu mmoja ndio atakuwa mwanzo wa mageuzi. Hata wachina walikuwa naye Mao Ze Dong
 
Nimeipenda hoja yako. Lakini hoja nzuri haihitaji kuwa ndefu hata fupi inatosha. Tatizo ulilolitaja litapungua kwa kiasi kikubwa sana kama tutamuondoa Mungu wa Ikulu anayeishi kwenye Ikulu ya nchi yetu kwa Katiba Mpya na kwa sanduku la kura. Hakuna njia ya mkato.
 
Mpango anaweza
 
Katiba mpya peke yake haiwezi kuwa suluhisho la matatizo kama wizi, inahitaji mtu alieye serious, ambae anaweza kukemea wizi kwa sababu yeye pia haibi
 
Katiba mpya peke yake haiwezi kuwa suluhisho la matatizo kama wizi, inahitaji mtu alieye serious, ambae anaweza kukemea wizi kwa sababu yeye pia haibi
Na huyo mtu SERIOUS akifa itakuwaje? Tunahitaji Katiba Mpya itakayohakikisha kuna taasisi imara na zisizoyumbishwa na mtu yeyote. Taasisi zinakufa? Taasisi imara zitakuwa tayari kumchukulia hatua bila kumuonea mtu yeyote hata Rais wa nchi pindi atakapobainika kuvunja sheria za nchi na Katiba ya nchi. Tusipomuondoa Mungu wa Ikulu pale Ikulu yote yanabaki ni porojo tu.
 
Katiba mpya peke yake haiwezi kuwa suluhisho la matatizo kama wizi, inahitaji mtu alieye serious, ambae anaweza kukemea wizi kwa sababu yeye pia haibi
Kwani JPM hakuwa SERIOUS! Yuko wapi sasa? Huo ni mfano rahisi kuonyesha mtu SERIOUS asivyokuwa na msaada wa muda mrefu. Taasisi imara ndiyo jibu pekee na hiyo itatokana na Katiba Mpya itakayomuondoa Mungu wa Ikulu pale Ikulu.
 
Suluhisho la matatizo kama haya ni Kuweka utaratibu katika nchi ambao Utawala wa nchi husika unajikita kwenye mifumo ya kitaasisi ambazo zipo imara na competent, badala ya kuwa na Serikali inayoendeshwa kwa mtindo kama wa Magenge ambayo yanamilikiwa na mtu binafsi au yanayomilikiwa na kikundi fulani cha Watu kama ilivyo hivi sasa.
 
Nadhani ubora wa mifumo pekee hauwezi kutatua. Kumbuka, mfumo wa kulipa fedha za serikali kupitia control number ulijikita pia kwenye kupunguza rushwa, na kama mfumo ni jambo zuri tu. Tatizo ni tabia za watu ambao wamejenga katika akili yao kwamba ni halali kuiba fedha za serikali. Sasa tumefikia mahali hata jeshi la polisi, sehemu usikotarajia mambo haya kufanyika, hawaridhiki na rushwa wanazotoza watu wanaona nao pia wana fursa ya kuiba kupitia mfumo wa malipo wa serikali.

Angalia kampuni binafsi za parking. Wanaiba kwa kutengezeza parking fee hewa kupitia mfumo wa malipo uliorahisishwa ili watu walipe kwa wakati wao bila kufukuzana na parking attendants. Halamashauri huko ndiko usiseme.

Tatizo sio mifumo - ni uongozi thabiti ambao watu wanajua uko serious katika kuchukia wizi. Hatuna huo uongozi kwa sasa.
 
Kwani JPM hakuwa SERIOUS! Yuko wapi sasa? Huo ni mfano rahisi kuonyesha mtu SERIOUS asivyokuwa na msaada wa muda mrefu. Taasisi imara ndiyo jibu pekee na hiyo itatokana na Katiba Mpya itakayomuondoa Mungu wa Ikulu pale Ikulu.
JPM hakufa kwa sababu alikua serious, labda kama una taarifa iliyo tofauti na kile tunachoambiwa kilimuua
 
Tanzania is among of the failed states, Wala siyo ya kuitolea mfano mzuri kwa chochote kile katikà masuala ya utawala bora.
 
Tanzania is among of the failed states, Wala siyo ya kuitolea mfano mzuri kwa chochote kile katikà masuala ya utawala bora.
Tanzania ina potential kubwa sana, lakini tatizo kwa sasa ni pale juu, ofisi ya raisi. Samia anaendesha nchi kama mwanaume ambae anadhani ili mpenzi wake ampende inabidi amhonge pesa nyingi kila wakati. Ndio mentality anayotumia ndio maana unasikia kelele za Samia katoa hela nyingi, kaahidi mamilioni ya mradi, Samia kaleta fedha ya mkopo nk. Mentality ni kwamba nikimwaga fedha wananchi watanipenda! Samia has never been, and will never be a philosophical president. Nyerere was, Mwinyi was japo kidogo sana, Mkapa was, Kikwete was not, Magufuli was. Samia ni routine president kama alivyokuwa Kikwete.

Halafu mie siku zote nimesema wazi, sifa za kumchagua mgombea mwenza wa uraisi sio kwamba ni mtu ambaye atakuwa raisi bora ikiwa raisi aliyepo madarakani akifa. Tanzania imewahi kuwa na mgombea mwenza mmoja tu ambaye alichaguliwa kutokana na umahili wake - Dr. Omar Juma. Na hili lilitukia kwa sababu Nyerere ndie alilisimamia. Kabla ya hapo makamu wa raisi alikuwa raisi wa Zanzibar - ambapo utaratibu huo ulitoa makamu wa raisi makini.

Samia hakuchaguliwa kuwa mgombea mwenza wa Magufuli kwa sababu ya sifa za kuwa kiongozi shupavu anaeweza kuwa raisi bora. Hakuna aliewaza kwamba Magufuli angeweza kufa kabla hajamaliza awamu yake. Hata Mpango hajachaguliwa kuwa makamu wa raisi kwa sababu za umahili wake katika kuwa kiongozi. Samia asingechagua makamu wa raisi ambaye angeonekana mahili zaidi yake kwa sababu angemfunika - kwa hiyo Mpango alionekana kufaa!

Na siku zote kuna kuwa na agenda iliyofichika kwamba achaguliwe mgombea mwenza ambae hawezi kumfunika raisi. Kwa hiyo raisi Samia ametokea kuwa raisi wa Tanzania si kwa sababu alikuwa na sifa za kuwa raisi. Hivyo anaposhindwa kusimamia mambo kama udhibiti wa fedha za serikali au uwekezaji toka nje hatupaswi kushangaa.
 
Rais Samia unamuonea tu katikà suala hili.
Tatizo siyo Rais Samia bali tatizo ni KATIBA MBAYA ILIYOPO HIVI SASA HAPA TANZANIA.
 
KATIBA MPYA ndio suluhisho la matatizo yetu hata kama sio kwa 100% lakini tukianzia hapo tutafaulu.
 
KATIBA MPYA ndio suluhisho la matatizo yetu hata kama sio kwa 100% lakini tukianzia hapo tutafaulu.
Yes, point nzuri, kuanza na Katiba mpya, ambapo jambo moja la msingi iwe kwamba Raisi akifa akiwa madarakani, makamu wa raisi atakuwa raisi ili kuongoza nchi kwenda kwenye uchaguzi mpya ndani ya mwaka mmoja toka kifo cha raisi kutokea, na yeye kama raisi wa mpito hataruhusiwa kugombea uraisi, ili asije akasimamia uchaguzi kwa namna ya kujipendelea, au kutumia kipindi cha maandalizi ya uchaguzi kwa namna ya kujitengenezea mazingira ya yeye kushinda uchaguzi wa raisi.
 
Magu alikuwa vzr sana, shida ni ile utekataji na watu wasiojulikana ndio walimuharibia sifa yake.!!
Mi nammiss sana daddie na ile tumbua tumbua. Kuna watu ss hivi wamevizoea vyeo nao wana vibesi.
 
Rais Samia unamuonea tu katikà suala hili.
Tatizo siyo Rais Samia bali tatizo ni KATIBA MBAYA ILIYOPO HIVI SASA HAPA TANZANIA.
Halafu ndio tatizo tulilonalo sasa hivi. Kuna watu mnaona kumkosoa Samia ni kumuonea, wakati mnajua wazi kuna madudu yanafanyika nchini. Tatizo sijui kwa kuwa ni mwanamke, kwa hiyo naturally mnataka kumkinga? Mnahitaji kumwona Samia kama raisi wa nchi, sio kama raisi mwanamke.
 
Hayo madudu yanayofanyika Yana baraka zake kutoka kwenye Katiba ya nchi, hata Rais Samia peke yake hawezi kuyazuia. Endapo kama Katiba ya nchi iliyopo ingekuwa nzuri na kuweka mifumo imara ya Utawala wa nchi, basi Watu (watawala) wasingeweza kupata nafasi ya kufanya hayo madudu, aidha wangeshindwa kabisa kuyafanya au wangeweza kuwajibishwa (kusulubiwa msalabani) endapo kama wangekuwa wakaidi na kufanya hayo madudu ambayo yamekatazwa na Sheria (Katiba).
Wala hatumtetei Rais Samia kama unavyodhani.
 
Basi unarudi kwenye kichwa cha thread hii - si CCM wala chama mbadala wa CCM wanaweza kututoa kwenye tope tulipo, tunahitaji uongozi wa mseto kama transition ya kipindi kisichopungua miaka mitano ili turekebishe mambo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…