Pre GE2025 Wizi na ufisadi wa fedha za serikali uliokithiri katika awamu hii, suluhisho haliko ndani ya CCM wala upinzani kuwa mbadala wa CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Basi unarudi kwenye kichwa cha thread hii - si CCM wala chama mbadala wa CCM wanaweza kututoa kwenye tope tulipo, tunahitaji uongozi wa mseto kama transition ya kipindi kisichopungua miaka mitano ili turekebishe mambo
Uongozi wa mseto kwa kutumia Katiba gani?
 
Transition period. Zanzibar walipoanza uongozi wa mseto walitumia katiba gani? Kenya je? Huhitaji ku-complicate haya mambo.
Tz is a failed state, kwa hiyo siyo nchi nzuri au Bora ya kuitolea mifano kwenye masuala ya utawala Bora.
Je, hauoni kwamba Mgogoro wa Kiutawala bado haujamalizika au bado upo pale pale huko Zanzibar???Je, Ni kweli kwamba haujui uwepo wa tatizo hili huko Zanzibar?????
 
Najua uwepo wa tatizo Zanzibar, ambalo sio tatizo lililopo serikali ya muungano,lakini tatizo la serikali ya muungano linaweza kuwa linachangia tatizo lililopo Zanzibar!
 
Najua uwepo wa tatizo Zanzibar, ambalo sio tatizo lililopo serikali ya muungano,lakini tatizo la serikali ya muungano linaweza kuwa linachangia tatizo lililopo Zanzibar!
Mbona Serikali ya mseto ipo Zanzibar, Sasa kwa Nini tatizo bado lipo huko ikiwa Serikali ya mseto ndio suluhisho kwa matatizo ya Kiutawala kama hayo??
 
Mbona Serikali ya mseto ipo Zanzibar, Sasa kwa Nini tatizo bado lipo huko ikiwa Serikali ya mseto ndio suluhisho kwa matatizo ya Kiutawala kama hayo??
Tatizo ni objectives za serikali ya mseto unayounda. Serikali ya mseto ya Zanzibar ipo kwa ajili ya kunyamazisha na kutuliza upinzani sio kutafuta way forward ya kudumu. Wapinzani wameridhika na kupewa nafasi fulani ili wanyamaze. Ile ya mseto ya Tanzania itakuwa ya muda lengo kubwa ikiwa ni kuleta katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi. Baada ya hapo haihitajiki tena.

Angalia hii thread

Mfumo aliozungumzia mchangiaji ni tofauti na wewe unachokizungumzia. Wewe unazungumzia Financial Software au Financial Applications yeye anazungumzia Administrative and Management Systems ambazo zinahusisha vyote ulivyovitaja. Ila nakubaliana na wewe kuhusu kutokuwepo na uongozi thabiti wa kusimamia hayo kwa pamoja ili vyote vilete matunda tunayotarajia. Hii ni changamoto ya kuwa na uongozi wa mtu mmoja ambaye kila mtu anamuogopa badala ya kuogopa sheria na taratibu za kazi. Hata mifumo ya kuwajibisha watumishi wezi imekuwa corrupted!
 
JPM hakufa kwa sababu alikua serious, labda kama una taarifa iliyo tofauti na kile tunachoambiwa kilimuua
Wewe umeelewa vibaya kaka. Maana yangu ni kuwa hata uwe SERIOUS kiasi gani kwa kuwa unakuwa peke yako ukiondoka kila kitu ulichokisimamia kinakwama. Kinachotakiwa ni Taasisi imara siyo mtu mmoja SERIOUS peke yake.
 
Okay, shukurani kwa ufafanuzi. Hivi tatizo ni uoga au kulinda maslahi? Maana ingekuwa ni uoga watu wasingekuwa wanaiba. Tatizo ni kwamba watu wanaona uozo na wanajua ni uozo, lakini hawasemi ili wasiondolewe katika nafasi zao na wengine wakapewa ikiwa watasema ukweli. Watu waoga ni kama wale wa Putin, wanamwogopa Putin japo hawafaidiki na nafasi walizonazo. Hawa wa hapa kwetu sio uoga wa nanma hiyo, ni suala la wao kujifanya hawaoni uozo ili waendelee kukaa katika neema walizonazo. Si ulimsikia yule aliyesema nilipoona Magufuli atanitumbua na mie nasomesha watoto niliamua kupendekeza tubadili awamu za uongozi ziwe za miaka saba badala ya mitano ili kumfurahisha!
 
Wewe umeelewa vibaya kaka. Maana yangu ni kuwa hata uwe SERIOUS kiasi gani kwa kuwa unakuwa peke yako ukiondoka kila kitu ulichokisimamia kinakwama. Kinachotakiwa ni Taasisi imara siyo mtu mmoja SERIOUS peke yake.
Nadhani tuko pamoja. Taasisi imara bila mtu imara haitasaidia kama vile tu kuwa na mtu imara bila taasisi imara
 
Kipindi cha jpm ndo wizi ikithiri ukiongozwa na jpm mwenyewe ila hakuna chombo cha habari chochote kilichokuwa na ubavu wa kulipoti kama sas ambapo mengine ni uonvo lla vimeachwa vyote vikue bwana mwenye shamba atakuja kuchambua magugu na ngano. Viva samia kupro.otd freedom of speech
 
Alisema mtanikumbuka na kauli yake inaakisi ukweli

Raisi alifeli aliposema kila mtu atakula kwa urefu wa kamba yake,,,shida ilianzia pale

..kwa ubaguzi na ukatili.

..ni mhuni tu ndiye anayeweza kuwaambia walipakodi sitawaletea barabara kwasababu mmechagua mpinzani.
 
Kwenye watu wengi huwezi kukomesha wizi unacho weza ni kudhibiti
 
Nadhani tuko pamoja. Taasisi imara bila mtu imara haitasaidia kama vile tu kuwa na mtu imara bila taasisi imara

..tumejaribu mambo mengi lakini bado hatujatengeneza taasisi na mifumo imara.

..hebu tujaribu kuandika Katiba Mpya bora itakayolinda maslahi ya wananchi, na vilevile kuwalinda wanaozingatia maadili na utawala bora.

..katiba ya sasa hivi imetengeneza Raisi-mungu-mtu. Na inalinda wezi wa rasilimali zetu.
 
Nadhani tuko pamoja. Taasisi imara bila mtu imara haitasaidia kama vile tu kuwa na mtu imara bila taasisi imara
Ukiwa na taasisi imara kila mtu anafanya kazi kulingana na taratibu za kazi. Hata taasisi za kusimamia nidhamu zinakuwa vibrant. Na ile kauli ya "Pengo lako haliwezi kuzibika" inakuwa haina uhalali wowote pindi mtu mmoja (imara) akiondoka.
 
Sahihi kabisa.
 
Leo naapa kueleza ukweli.Unataka nieleze ukweli?
 
Unajua JPM hakuwa mwizi wa kiasili. JPM alitaka kuwa na fedha ambazo angezitumia anavyotaka yeye bila mambo ya bajeti ya Bunge. Kwa hiyo alikuwa anachukua fedha kutoka taasisi mbalimbali kama Bandari, na kuziweka ambako haijulikani. Ndio zile trilioni 15 CAG alisema hajui zilienda wapi.

Kuna wakati hata alitoa maagizo barabara zijengwe bila bajeti ya Bunge, akisema fedha nitatoa, kwa sababu alikuwa nazo. Hata kitengo cha wasiojulikana kiliendeshwa kwa hizo fedha ambazo zilikuwa hazina hata accountability.

Ndio maana alipokufa, watu wachache waliojua ziko wapi walianza kuzihamishia account zao, Samia akatoa amri kwa benki zote wasimamishe transaction kubwa zote za ndani kwa miezi mitatu. Walikuwa wakizitafuta hizo fedha, na sijui kama walizipata.

Sasa huo ndio ulikuwa wizi wa Magufuli
Ukiwa na taasisi imara kila mtu anafanya kazi kulingana na taratibu za kazi. Hata taasisi za kusimamia nidhamu zinakuwa vibrant. Na ile kauli ya "Pengo lako haliwezi kuzibika" inakuwa haina uhalali wowote pindi mtu mmoja (imara) akiondoka.
Nchi kama South Africa, Zimbabwe, wana utaratibu mzuri sana wa kitaasisi. Lakini unaona madudu yanayofanyika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…