Wizi wa catalytic converter kwenye magari 'Masega'

Safi sana..
lakini bado ninaendelea kudodosa kama kuna mtu akiyewahi kutoa cat converter kwenye toyota au nissan atumegee uzoefu kidogo ni nini kilitokea baada ya kutoa...
Nimezungumzia nissan na toyota coz naona ni kampuni mbili ambazo mifumo yake inashabihiana sana.

Je baada ya kutoa gari iliongeza nguvu na kumaintain fuel consumption nzuri au gari ilileta matatizo mengine kibao??
 
Hembu dhibitisha kauli yako kwa mifano na hoja za kitaalam ukiachana na maneno ya kijiweni..na huo mzigo unatoka wapi?? Na usije ukajiongopea kuna gari ukitoa hayo ujue ndio umeharibu gari linakuwa guta
Dhibitisha [emoji808]

Thibitisha[emoji818]
 
Mkuu labda mm nikwambie tuu kinachotokea ni hiki unapotoa cut converter kwa gari nyingi hasa tuzitumiazo bongo lazima utaona ina gain au ongeza power na ulaji wa mafuta kuimalika kwa kiasi fulani kwa sababi..

Gari zinazokuja bongo ni used so inamaana cut converter ishaamza kuchoka ndio maana gari nyingi za bongo zikiagizwa used huwezi pata ile fuel consumption inayotakiwa so ww utakapo toa lazima gari itakuwa na mabadiliko flani..lkn kwa gari za kisasa ukitoa mara nyingi huwa ni shida zaidi ikiwa kupunguza perfomance ya gari na kuongeza ulaji wa mafuta
 
Point noted..
Nitqjaribu kutoa kwa uangalifu mkubwa...nikiona kuna mdhara narudishia.
 
Mkuu unaweza nipa kazi ya SCR (Selective Catalytic Reduction)
 
Yes uko sahihi ndugu. DPF iko kwenye hizi common rail diesels.
 
Mkuu unaweza nipa kazi ya SCR (Selective Catalytic Reduction)
Ndio lakini sio kitaalam sana kwa kukutajia majina ya chemical na gasi zilizopo kwenye hewa na vipi vipi DEF ina convert nn kuwa nn but kwa kiwango ambacho na elewa na nn scr inafanya..


Mkuu SCR huu ni mfumo kama wa DPF na catalic converter lengo kubwa ni kupunguza uchafuzi wa mazingira unaotokana na moshi wa gari baada ya disel kuunguzwa na engine..lkn mfumo huo wenyewe huwa unatumia liquid flani ambayo huwa inakwenda kwenye catalic converter na kufanya reaction ya kubadili hewa ya nitrogen oxide na kuwa hewa ya nitrogen water na kiwango kidogo cha carbon dioxide..

Mfumo huu upo sana kwenye viwanda au kwenye majenereta makubwa makubwa yale ya viwandani kwenye meri n.k na kwenye magari makubwa..

Ila yote au lengo ni kupunguza uchafuzi wa mazingira. Kuna kitu inaitwa addblue mifumo yote hiyo lengo lake ni moja..

Nadhani mkuu utakuwa umenielewa..

So unapoiondoa mifumo hii kienyeji enyeji huwa na madhara .na kuna baadhi ya gari haziwezi kuwaka kabisa au kujiweka kwenye SAFE MODE..ili iwe salama zaidi lazima kuna mambo mawili moja wapo ulifanye au kufunga emulator ili uweze kuidanganya control box kwamba mfumo uko kamili na sahihi au uifanyie program control box..kuna vitu vinaitwa dpf ,egr,adblue,scr and lamda sensor off or remove.
Na hili kwa bongo bado nigeni kidogo ndio maana badala ya kutengeneza magari tunaishia kuihalibu zaidi kutokana na kutofaham..

Wenye gari za disel toyota na nissan like navara or prado hilux and land cruiser humo ndio kuna dpf kwa sana na mwishowe wengi huishia kusema turbo sijui engine majanga.

Na huwa kunakuwa na batani/switch yenyewe kazi yake nikusafisha mfumo wa dpf huwa wanaita dpf regenerate./regeneration kuna warning light ikikuwakia tuu basi unafanya hicho kitu au watumia mashine kufanya hivyo hapo unasafisha kabisa mfumo wa exhaust na kama hutofanya hivyo matokeo yake dpf huziba kabisa na gari kukosa nguvu na inaweza kuua engine kabisa.
 
kweli kabisa
 
yapo kwenye gari zip na zip...na yanatumika kufanyia nini kwa hao wanunuzi...maana gari kibao zimekufa magarage nikatoe niuze kama ni mchongo
 
Taa ya Engine inawaka, Ulaji wa mafuta unaongezeka na mlio wa gari unabadirika. Ukitaka kufahamu hapo hapo ni Taa ya engine kuwaka.. Ahsante
Kuondoa yale manyama kwenye Catalytic convertor hakuongezi unywaji wa mafuta, bali kunaipa uwezo engine ku breath vizuri sana, na in terms of power, unagain lakini not noticebale at all. The reason hayo madude yameekwa ni ku silence mvumo wa gari na mambo ya mazingira. Vile vile Check engine light haiwaki kwa sababu hayo manyama yametolewa. Kwenye hio mitungi kunakuwa na sensors, kazi ya hizi sensor ni kupima hewa iliyotoka kwenye engine (Oxygen) na kuitaarifu ECU mafuta yanayohitajika kwenye engine. Sensor ikiwa mbovu ndio check engine itakuwakia. Ila kama ni nzima, ina solve hio ishu wenyewe na kuadjust tu.

Jambo jengine, Tukijaalia kuwa sensor ni mbovu, pia Check engine light haiwaki hapo hapo. Kawaida ukichomoa betru ya gari, error zote zina ji reset. Hivo ukiwasha gari, check engine haiwaki hata kama kuna tatizo, ila ukishatembea kwa masafa machache au gari ikiwa imenguruma kwa muda fulani ndipo utaiona kuwa inawaka.

Njia pekee na ya haraka kujua kama wameyatoa, isikilize exhaust yako inavotoa sauti ukiona tofauti na mwanzo yaani mvumo umekuwa mkubwa basi tupia jicho chini au waulize tu mafundi kunani....
 
Msaada jaman,
Gearbox ya gar yang aina ya corollar 4E 111 imezingua ikatafuna baadh ya meno hasa pinion, fundi wang anasema Automatic gearbox haitengenezeki. Je n kwel swez kuitengeneza?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wakuu..

Kuna hii biashara naona ipo kasi sana kuhusu haya madini yanayopatikana kwenye muffler ya gari, yapo kwenye kimtungi wao wanayaita mazega kama sikosei.

Swali langu ni haya mazega (mineral in catalyst converter) wanayafanyia nini? Pia bei yake kwa kilo?

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…