CHARLES2016
JF-Expert Member
- Mar 22, 2016
- 376
- 435
Mkuu, huyu kijana ana asili ya Singida?Bwana mdogo anaenda DODOMA kuwakilisha Jimbo la nyamagana 2020-2025
Ccm walikosa mtu imara nyamagana....
Siku moja ntaandika KUHUSU huyu bwana mdogo....
Kila la kheri John Justin Pambalu
View attachment 1555659
Hapo ndo unapofeli mzee....Yaani kama magufuli ameweza kuwa rais kwa miaka hii mitano, basi nchi hii mtu yoyote anaweza kuwa rais hata Mimi na weweMagufuli yuko sahihi, TL kupewa nafasi ya urais kwa sasa is premature. Sina tatizo na TL kiwa rais but anahitaji kujijenga na kujiandaa kwa nafasi hiyo. Sijwahi kupiga kura, but TL akibadilika comes 2025 nikiwa hai naweza kupiga kura kwa mara ya kwanza na nitampa kura yangu TL. Hata hivyo si jambo kuangalia upepo kwa maandalizi ya 2025
Wanashangilia nini?Huyu mtu anajuwa mpaka anakera
Nimecheki video ya hotuba yake mpaka nimetamani kulia machozi jamaa ameshangiliwa mwanzo wa hotuba mpaka mwisho kwa muda wa karibia dakika 50
Kweli watu wamechoka na wanataka mabadiliko.
Maneno ya kipuuzi ya kujifariji. Hivyo vyote visingekarabatiwa na awamu ya tano huyo huyo Lissu angesema hawa hawafai kuwepo madarakani kwani wamekubali kila kitu kisifanyiwe ukarabati na matokeo yake kipo vile vile kama kilivyoachwa na wakoloni!!.Tundu Lissu Mwanza;
Viwanja vyote vya ndege vilianzishwa na Waingereza isipokuwa KIA, Songwe na Chato.
Reli inayokuja Mwanza ilijengwa na Waingereza.
Reli ya Tanga hadi Arusha ilijengwa na Wajerumani.
Reli ya Kati ilijengwa na Wajerumani.
Reli ya TAZARA ilijengwa na Nyerere kwa msaada wa Wachina.
Bandari ya Mwanza ilianzishwa na Wajerumani.
Bandari ya Kigoma ilianzishwa na Wajerumani.
Bandari zote kubwa za bahari ya hindi zilianzishwa na Wajerumani.
Hata ikulu ya Dar es salaam ilijengwa na Wajerumani na baadae ikaboreshwa na Waingereza.
Kwanini tuliwakataa Waingereza na Wajerumani?
Ni kwa sababu utawala wao haukuwa wa haki.
Oktoba mwaka 1968 Mwalimu Nyerere alichapisha andiko lake liloitwa Uhuru na Maendeleo.
Mwalimu alisema, Uhuru na Maendeleo ni kama Kuku na Yai. Hupati Kuku bila Yai na hupati Yai bila Kuku. Hupati maendeleo bila Uhuru na hupati Uhuru bila maendeleo. Maendeleo lazima yahusishe watu. Vitu kama barabara, majengo makubwa, reli nk sio maendeleo, bali ni nyenzo za kutuletea maendeleo. Hakuna maana kama tunajenga mabarabara halafu raia wanakamatwa hovyo kwa sababu ya kumuudhi mtu mwenye madaraka.
Lissu akaendelea.
Sikatai kuwa ujenzi wa barabara ni jambo zuri. Sikatai ujenzi wa reli ni jambo zuri.
Lakini utawala wa haki ni muhimu kuliko hayo yote.
------------------------------------------------------------------------------------------------------
Rais wa Marekani, Ronald Reagan aliwahi kusema maneno kama hayo. Akaongeza kuwa Raia wa Marekani ana thamani kubwa kuliko mabarabara ya ghorofa na silaha za Nyuklia. Kwa sababu hayo yote yapo kwa faida ya Raia wa Marekani, na sio kwamba Raia wa Marekani yupo kwa faida ya hivyo vitu.
Theodore Roosevelt naye alisema; haki za Mali na haki za binadamu zinakwenda sawa. Lakini ikitokea haki hizi zinapihana basi haki za binadamu zipewe kipaumbele. Kwa sababu Mali zipo ili zimnufaishe binadamu, sio binadamu azinufaishe mali.
Kwa lugha nyepesi ili mswahili wa kawiada aelewe; ni kwamba, Kujenga miundombinu ya mikubwa huku wananchi wakitegemea mlo mmoja, huku raia wana hofu ya kutoa maoni yao, bado watu wanatekwa, kupotezwa na kuuawa bila uchunguzi, huku miili ya watu inaokotwa halafu serikali inaizika bila uchunguzi...
Asante Mwanza, Asante Tanzania.View attachment 1555631View attachment 1555632
Matajiri hawaingii JF. Wote humu kajamba nani ila isikupe presha kijana wa Lissu wa moja hawezi kuwa mbili. Lissu hana hoja anaokoteza tuUnahofia MB mbona tupo uchumi wa kati.
Unajifanya kushupaza shingo kumtetea huyo dikteta wako kumbe una njaa Kali kiasi kwamba ku 'view' clip ya sec 5 tano tu unalia na Megabytes.
Inashangaza!
Unataka Rais akufanyie nini ? Au unaona uhuru ni immaterial? Rais hamfanyii mtu kitu watu wanatoa kodi zao ili serikali ifanye kile inachotakiwa kukifanya kutokana na mipango ya nchi...., haya mambo ya mtu kuamua ya kufanya ndio utawala wenyewe huo...Kwahiyo hitimisho kasema atawafanyia nini watu wa Mwanza?
Hahaa nilitamani iwe hivyo lakini naogopa kuja kuumia moyoni. Baada ya Mavu kuapishwa tena.
We nae mgumu kuelewa... ndo maana anakwambia kina nyerere waliamua kuunganisha nguvu kumkataa coz hivo ulovitaja vilileta mushkel
Bwasheee umepagawa na mambo ya mwanzaAcha kukariri bwashee!
kweli uelewa upo tofauti..., visingefanyika kwanini asiseme...Maneno ya kipuuzi ya kujifariji. Hivyo vyote visingekarabatiwa na awamu ya tano huyo huyo Lissu angesema hawa hawafai kuwepo madarakani kwani wamekubali kila kitu kisifanyiwe ukarabati na matokeo yake kipo vile vile kama kilivyoachwa na wakoloni!!.
Uzuri ni kwamba hao maelfu ya watu ni wenye akili timamu na wenye kupima mchele ni upi na pumba ni zipi.
Hao wasanii hawapigi kura? kwa nini hawajajitolea kumnadi wenu? ujue uchaguzi huu hakuna msanii anayelipwa na chama, wote wamejitolea kutokana na mapenzi yao kwa JPM.
Kwa kuongeza waliojenga ni Watanzania tena bure bila malipo stahiki. TL huu ndio mwisho wake hawezi kuwadhihaki Watanzania kiasi hiki. Yeye aende akatulie huko Belgium apumuliwe vizuri kisogoni.Kumjibu kifupi Lisu Ni kuwa Kodi zote na faida za miundo mbinu zilienda kujenga Ulaya sio Tanzania ndio masna tulamkimbiza mkoloni pamoja na kujenga miundo mbinu
Leo faida za miundo mbinu yetu inabaki nchini .Lisu hajui hata historia
Walijenga reli,barabara sawa lakini faida haikubaki nchini!!!
Hotuba yake hopeless
Tulidai Uhuru faida ibaki nchini isiende kujenga ujerumani na uingereza kwa wakoloni
Msukuma huyoMkuu, huyu kijana ana asili ya Singida?
Kwani kujaa kwa watu kwenye mkutano ni ishara ya kumpa kura ? Wengine wameenda kushangaa aliyepigwa risasi bado yupo hai? .... Huwajui wasukuma wewe tuulize sisi msukuma anapelekwa pilisi ukimuuliza vipi anakujibu ndoho tabu , yaani hakuna shida ..... Wasukuma wepesi wa kukubali juuu juu ila subiri kwenye vitendo ndio utachoka ngome ya ccm ni kanda ya ziwa subiri october utaamini haya ninayokwambia hata leo nilikuwepo Mwanza yaliyotokea ni ya kawaida sana ni jmati tu kama wa mkutano wa injili wa mwl mwakasege ... october sio mbali utaona