Uchaguzi 2020 Yaliyojiri katika Kampeni za Tundu Lissu Jijini Mwanza

Mgombea Urais wa Chadema Tundu Lissu leo anatarajiwa kuitikisa jiji la Mwanza katika mkutano mkubwa wa Hadhara katika viwanja vya Furahisha.

Tayari maandalizi yamekamilika na maandamano makubwa ya kumlaki yanasubiriwa kuanza wakati wowote kutoka sasa

Tayari mgombea huyo ameshafanya mikutano minne ya kampeni ambapo mitatu ilikuwa jijini DSM na mmoja ulikuwa jijini Arusha hapo Jana.
Tundu Lissu akitaka Kura, anachopaswa kufanya ni kuzungumzia vizuri issue ya Maji. Mwanza tunapata tabu Sana ya Maji. Maji shida Sana na wakati ziwa lipo karibu tu mita chache.
 
Ficha upumbavu wako wewe, si lazima kila jambo ulizungumzie! Malaria ipo Tabora na Singida itakosa Mwanza? Eti Mwanza wana afya! Sogea hapo Bugando uone wasukuma wanavyotaabika.

Kuna mwanadamu wa leo asiyehitaji bima? Kujua umuhimu wa bima kunahitaji hata elimu ya chekechea? Uvyama usitutoe akili. Tumia nafasi yako kuwashauri wakubwa wa chama chako kutambua na kuboresha huduma muhimu za kijamii kwa wananchi pale mnapopata fursa ya kuongoza, si kuwafanya wananchi mazuzu.
Tatizo Lisu kwa kuwa anaumwa andhani kila mtu hitaji lake Ni kuwa na bima ya kutibiwa.Nenda mijini watu kibao hawana bima na hawana mpango nayo hata ukisema wakachukue Bure anakwambia ya nini? Mimi sijaugua miaka Saba sasa malaria niitake ya Nini ? Nikiumwa naenda duka la dawa nanunua Panadol Mia tano biashara imeisha

Hitaji kuu la watanzania sio bima ya afya hasa wa kawaida mijini na vijijini kwenye nchi zetu za kiafrika

Lisu anahangaika kuifanyia marketing lakini Ni concept inayoweza eleweka zaidi kwa middle class wanaoumwa ambao kutwa Ni wao ba hospital hospital na wao
 
Bugando na sekou toure kumefurika wagonjwa tele, hospital ya Butimba, vituo vya afya Kama vile buzuruga, nk watu wamefurika, unadhani hizo ni kumbi za harusi na hao watu wako harusini?!
Wanatoka mikoa mingine sio wenyeji wa Mwanza. Nenda Bugando hapo kahakiki.Msukuma wa Mwanza kumkuta anaumwa sio rahisi

Wana miiki ya chuma hao watu
 
Anaenda tu kukamikilisha ratiba Mwanza kule huwaambii kitu kuhusu Magufuli
Na kwa kuwa Lisu amekuwa akiponda ujenzi wa reli ya mwendokasi kwenda Mwanza atapata jibu Leo wengi hawataenda mkutanoni

Tena Mwanza mjini linashushwa daraja la nguvu Busisi
Endelea kuwa hewani, utapata jibu baadae..
 
Baadaye wapi? Mkutano umedoda huo Enzi za Lowasa huo uwanja ulikuwa tayari umejaa kuanzia saa moja asubuhi .Huo wenu wa kusubiri Giza liingie Halafu mnaleta picha za 2015 mkiwa mumme edit zikiwa na Giza Giza Mkutano gani huo?

Picha hazipigwi toka juu .Za video mnaunga mnachukua video ya 2015 mnaweka na ya Lisu ya Leo !!!

Pigeni za drone Kama kipindi Cha Lowasa
 
Tatizo Lisu kwa kuwa anaumwa andhani kila mtu hitaji lake Ni kuwa na bima ya kutibiwa.Nenda mijini watu kibao hawana bima na hawana mpango nayo hata ukisema wakachukue Bure anakwambia ya nini? Mimi sijaugua miaka Saba sasa malaria niitake ya Nini ? Nikiumwa naenda duka la dawa nanunua Panadol Mia tano biashara imeisha

Hitaji kuu la watanzania sio bima ya afya hasa wa kawaida mijini na vijijini kwenye nchi zetu za kiafrika

Lisu anahangaika kuifanyia marketing lakini Ni concept inayoweza eleweka zaidi kwa middle class wanaoumwa ambao kutwa Ni wao ba hospital hospital na wao
Kama umeamua kuwa kada wa chama chochote socialize vya kutosha kwanza ili ujue maisha ya watanzania ambao ndio mtaji wako. Sasa jamaa unapigia chapuo chama kitatue shida za wananchi kumbe hata shida zao huzijui!

Acha kujifungia ndani na kuhudhuria shughuli za ccm pekee ndipo utazungumza vitu vya kueleweka, otherwise unaonekana kituko!!! Naamini asili yako si mjini, tembelea hata ndugu zako vijijini ujue changamoto zao ndipo uje kuzungumza. Acha upumbavu!

Hao unaowaita middle class unafahamu ni watu wangapi? Unafikiri Lissu anategemea apate kura zote 100%? Unaelewa maana na malengo ya kampeni? Mshauri jiwe ndo huwa anaamini akifanya jambo moja basi ametatua kero za makundi yote kisha anataka kura zao zote kwa lazima!

By the way, kama mawaziri na ukwasi wao wote bado wanahitaji bima, hao matajiri wa Mwanza wasiohitaji bima unaweza kutupa takwimu zao? Unavyoielezea Mwanza kama peponi vile, huenda hata hujawahi kufika.
 
Wanatoka mikoa mingine sio wenyeji wa Mwanza. Nenda Bugando hapo kahakiki.Msukuma wa Mwanza kumkuta anaumwa sio rahisi

Wana miiki ya chuma hao watu
Mtu atoke mkoa mwingine aje kutibiwa sekou toure, Butimba ama buzuruga?! Kwa bugando sawa sababu ni hospital ya rufaa ya kikanda, lakin hospital za mkoa na wilaya ziko kila mkoa na kila wilaya, haya vipi hao waliofurika sekou toure, butimba, buzuruga na igoma?!
 
Amekuwa akiponda ununuzi wa Ndege jibu atalipata mwanza Ndege ukiuliza wauza samaki mitaani watakuambia jinsi abiria wa Ndege wanavyobeba samaki kwa wingi
Hapo akienda na porojo zake za kupinga ununuzi wa Ndege aone wavuvi na wauza samaki watakavyoguna hata Kama Ni Chadema

Ndege nyingi hufurika Mwanza kubeba samaki kupeleka nje ya Nchi kibao akiponda ununuzi wa Ndege Mwanza hata mtu wa mtaani atamzomea sababu wanajua umuhimu wa Ndege kwenye biashara yao ya samaki
Mwache aiingie kwenye 18 aone! Asifikiri Mwanza ni Arusha au Moshi. Amuulize Lowassa atamsimlia vizuri.
 
Anaenda tu kukamikilisha ratiba Mwanza kule huwaambii kitu kuhusu Magufuli
Na kwa kuwa Lisu amekuwa akiponda ujenzi wa reli ya mwendokasi kwenda Mwanza atapata jibu Leo wengi hawataenda mkutanoni

Tena Mwanza mjini linashushwa daraja la nguvu Busisi
Busisi ipo Mwanza mjini? Wewe ni wa kupuuzwa tu.
 
Ha
Amekuwa akiponda ununuzi wa Ndege jibu atalipata mwanza Ndege ukiuliza wauza samaki mitaani watakuambia jinsi abiria wa Ndege wanavyobeba samaki kwa wingi
Hapo akienda na porojo zake za kupinga ununuzi wa Ndege aone wavuvi na wauza samaki watakavyoguna hata Kama Ni Chadema

Ndege nyingi hufurika Mwanza kubeba samaki kupeleka nje ya Nchi kibao akiponda ununuzi wa Ndege Mwanza hata mtu wa mtaani atamzomea sababu wanajua umuhimu wa Ndege kwenye biashara yao ya samaki
Hizi ndege zinachukua minofu na kutuachia mifupa - mapanki. Uwiiiiiii!
 
Anaenda tu kukamikilisha ratiba Mwanza kule huwaambii kitu kuhusu Magufuli
Na kwa kuwa Lisu amekuwa akiponda ujenzi wa reli ya mwendokasi kwenda Mwanza atapata jibu Leo wengi hawataenda mkutanoni

Tena Mwanza mjini linashushwa daraja la nguvu Busisi
Mimi ni mkazi wa kijiji cha Kahumlo - Busisi. Kura yangu kwa Lissu anayeniahidi uhuru, haki, na maendeleo yangu.
 
Baadaye wapi? Mkutano umedoda huo Enzi za Lowasa huo uwanja ulikuwa tayari umejaa kuanzia saa moja asubuhi .Huo wenu wa kusubiri Giza liingie Halafu mnaleta picha za 2015 mkiwa mumme edit zikiwa na Giza Giza Mkutano gani huo?

Picha hazipigwi toka juu .Za video mnaunga mnachukua video ya 2015 mnaweka na ya Lisu ya Leo !!!

Pigeni za drone Kama kipindi Cha Lowasa
Tumepiga za Drone,imepatikana hii.
JamiiForums-879927817_641x534.jpg
 
Mgombea Urais wa Chadema Tundu Lissu leo anatarajiwa kuitikisa jiji la Mwanza katika mkutano mkubwa wa Hadhara katika viwanja vya Furahisha.

Tayari maandalizi yamekamilika na maandamano makubwa ya kumlaki yanasubiriwa kuanza wakati wowote kutoka sasa

Tayari mgombea huyo ameshafanya mikutano minne ya kampeni ambapo mitatu ilikuwa jijini DSM na mmoja ulikuwa jijini Arusha hapo Jana.

Chadema katika uchaguzi mkuu huu inatumia kauli Mbiu ya Uhuru,Haki na Maendeleo ya watu.

#UhuruHakiNaMaendeleoyawatu#
#Niyeye2020#
Hongera zenu. Naomba huko kannda ya ziwa mkutano mmoja uwe Chato tena ikiwezekana iwe pale pale nyumbani kwa Nduli Idd Amin
 
Back
Top Bottom