Uchaguzi 2020 Yaliyojiri katika Kampeni za Tundu Lissu Jijini Mwanza

Uchaguzi 2020 Yaliyojiri katika Kampeni za Tundu Lissu Jijini Mwanza

Haha unaota subirini mwenye Mwanza yake afike mtajificha uvunguni siku hiyo.ccm ni mwanza na mwanza ni ccm, shinyanga, Geita simiyu na Kagera kote chadema andikeni maumivu ya kifua kikuu.Huko ndiyo kuna kura 12 million za Magu labda muokoze za ziada.
Nasikitika kutokuwepo Mwanza. Sisi wa Mwanza hatuna habari na Jiwe.

Hata 2015, CCM hawakushinda Mwanza. Wizi mkubwa wa kura ulifanyika. Kura za wizi zilipigwa usiku kucha siku ya tarehe 14 kuamkia 15 Oktoba kwenye ukumbi wa shule ya Sekondari ya Alliance, walimu walilazimishwa kuweka alama ya V kwa Jiwe na Mabula wawili. Mkuu wa shule ambaye ni Mkenya alikataa. Kilichompata, anakijua yeye, Mungu wake, ubalozi wa Kenya na watu wake wa karibu.

Pamoja na huo wizi, jimbo la Nyamagana, bado kwenye ubunge CCM waliachwa kwa mbali. Wakalazimisha, wakamtangaza Mabula!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwezi kuua kirahisi rahisi kilichomo ndani ya mioyo ya Watanzania KAMWE haiwezekani endeleeni kujidanganya tu.

 
Ametisha. Wakoloni walijenga reli, barabara, shule, vyuo, hospitality, elimu bure, matibabu bure, maji bure, lakini tulikosa kitu kikubwa kuliko vyote,...UHURU
Mkuu pole kama ndiyo historia uliyofundishwa na ukaamini.

Hakuna kipindi kilikuwa kigumu kuishi hapa Afrka kama kipindi cha ukoloni.

Hakuna kilichokuwa bure, elimu ilikuwa sio elimu bali minyororo ya utumwa wa fikra, mkuu kwenye suala la afya ndio panatia simanzi, tukaingizwa kwenye utegemezi wa kiafya mpaka leo - kwenye corona tumejifunza kwamba mkoloni hafai, kwenye maji haikuwa huduma safi kama anayofanikisha JPM.

kiufupi ndugu yangu, yeyote anayesifia mkoloni muogope kama ukoma.

Sent from my SM-J105F using JamiiForums mobile app
 
Kwani Magufuli anafanya kampeni moja kwa siku? Thubutuuu!!!
Leo aliyoyaongea huko Ikungi - Singida ni ishara tosha kuwa "amekamatika" haswa.
Kwahiyo Lisu kashajihakikishia ushindi ndio maana anafanya mkutano mmoja kwa siku?
 
Ccm kwa sasa hivi wamehamia kwenye kushindanisha umahiri wa kucheza SINGELI baada ya mgombea wao kuwaruka kwenye sera na kujikuta anaongelea kugongana bila kinga.
 
Mliambiwa kuwa hamtavunjiwa nyumba kwa sababu mnaipenda CCM. Kwa usaliti mlionyesha leo tunakuja kuvunja nyumba zenu zote mlizojenga holela.

Uthibitisho ni hii picha. Haya mahaba mliyoonyesha kwa mgombea wa CHADEMA mwenyekiti hawezi kuvumilia.
IMG_20200901_173252_513.JPG


Sent from my Infinix Zero 3 using JamiiForums mobile app
 
Magufuli amewaambia watz wazaliane Kwa wingi kwakuwa kanunua ndege, kajenga sgr, anajenga bwawa la stiegler,
 
Tundu Lissu Mwanza;
Viwanja vyote vya ndege vilianzishwa na Waingereza isipokuwa KIA, Songwe na Chato.
Reli inayokuja Mwanza ilijengwa na Waingereza.
Reli ya Tanga hadi Arusha ilijengwa na Wajerumani.
Reli ya Kati ilijengwa na Wajerumani.
Reli ya TAZARA ilijengwa na Nyerere kwa msaada wa Wachina.

Bandari ya Mwanza ilianzishwa na Wajerumani.
Bandari ya Kigoma ilianzishwa na Wajerumani.
Bandari zote kubwa za bahari ya hindi zilianzishwa na Wajerumani.

Hata ikulu ya Dar es salaam ilijengwa na Wajerumani na baadae ikaboreshwa na Waingereza.

Kwanini tuliwakataa Waingereza na Wajerumani?
Ni kwa sababu utawala wao haukuwa wa haki.

Oktoba mwaka 1968 Mwalimu Nyerere alichapisha andiko lake liloitwa Uhuru na Maendeleo.

Mwalimu alisema, Uhuru na Maendeleo ni kama Kuku na Yai. Hupati Kuku bila Yai na hupati Yai bila Kuku. Hupati maendeleo bila Uhuru na hupati Uhuru bila maendeleo. Maendeleo lazima yahusishe watu. Vitu kama barabara, majengo makubwa, reli nk sio maendeleo, bali ni nyenzo za kutuletea maendeleo. Hakuna maana kama tunajenga mabarabara halafu raia wanakamatwa hovyo kwa sababu ya kumuudhi mtu mwenye madaraka.

Lissu akaendelea.
Sikatai kuwa ujenzi wa barabara ni jambo zuri. Sikatai ujenzi wa reli ni jambo zuri.
Lakini utawala wa haki ni muhimu kuliko hayo yote.
------------------------------------------------------------------------------------------------------

Rais wa Marekani, Ronald Reagan aliwahi kusema maneno kama hayo. Akaongeza kuwa Raia wa Marekani ana thamani kubwa kuliko mabarabara ya ghorofa na silaha za Nyuklia. Kwa sababu hayo yote yapo kwa faida ya Raia wa Marekani, na sio kwamba Raia wa Marekani yupo kwa faida ya hivyo vitu.
Theodore Roosevelt naye alisema; haki za Mali na haki za binadamu zinakwenda sawa. Lakini ikitokea haki hizi zinapihana basi haki za binadamu zipewe kipaumbele. Kwa sababu Mali zipo ili zimnufaishe binadamu, sio binadamu azinufaishe mali.

Kwa lugha nyepesi ili mswahili wa kawiada aelewe; ni kwamba, Kujenga miundombinu ya mikubwa huku wananchi wakitegemea mlo mmoja, huku raia wana hofu ya kutoa maoni yao, bado watu wanatekwa, kupotezwa na kuuawa bila uchunguzi, huku miili ya watu inaokotwa halafu serikali inaizika bila uchunguzi...

Asante Mwanza, Asante Tanzania.
FB_IMG_1598974790572.jpeg
FB_IMG_1598974788139.jpeg
 
Back
Top Bottom