Tundu Lissu Mwanza;
Viwanja vyote vya ndege vilianzishwa na Waingereza isipokuwa KIA, Songwe na Chato.
Reli inayokuja Mwanza ilijengwa na Waingereza.
Reli ya Tanga hadi Arusha ilijengwa na Wajerumani.
Reli ya Kati ilijengwa na Wajerumani.
Reli ya TAZARA ilijengwa na Nyerere kwa msaada wa Wachina.
Bandari ya Mwanza ilianzishwa na Wajerumani.
Bandari ya Kigoma ilianzishwa na Wajerumani.
Bandari zote kubwa za bahari ya hindi zilianzishwa na Wajerumani.
Hata ikulu ya Dar es salaam ilijengwa na Wajerumani na baadae ikaboreshwa na Waingereza.
Kwanini tuliwakataa Waingereza na Wajerumani?
Ni kwa sababu utawala wao haukuwa wa haki.
Oktoba mwaka 1968 Mwalimu Nyerere alichapisha andiko lake liloitwa Uhuru na Maendeleo.
Mwalimu alisema, Uhuru na Maendeleo ni kama Kuku na Yai. Hupati Kuku bila Yai na hupati Yai bila Kuku. Hupati maendeleo bila Uhuru na hupati Uhuru bila maendeleo. Maendeleo lazima yahusishe watu. Vitu kama barabara, majengo makubwa, reli nk sio maendeleo, bali ni nyenzo za kutuletea maendeleo. Hakuna maana kama tunajenga mabarabara halafu raia wanakamatwa hovyo kwa sababu ya kumuudhi mtu mwenye madaraka.
Lissu akaendelea.
Sikatai kuwa ujenzi wa barabara ni jambo zuri. Sikatai ujenzi wa reli ni jambo zuri.
Lakini utawala wa haki ni muhimu kuliko hayo yote.
------------------------------------------------------------------------------------------------------
Rais wa Marekani, Ronald Reagan aliwahi kusema maneno kama hayo. Akaongeza kuwa Raia wa Marekani ana thamani kubwa kuliko mabarabara ya ghorofa na silaha za Nyuklia. Kwa sababu hayo yote yapo kwa faida ya Raia wa Marekani, na sio kwamba Raia wa Marekani yupo kwa faida ya hivyo vitu.
Theodore Roosevelt naye alisema; haki za Mali na haki za binadamu zinakwenda sawa. Lakini ikitokea haki hizi zinapihana basi haki za binadamu zipewe kipaumbele. Kwa sababu Mali zipo ili zimnufaishe binadamu, sio binadamu azinufaishe mali.
Kwa lugha nyepesi ili mswahili wa kawiada aelewe; ni kwamba, Kujenga miundombinu ya mikubwa huku wananchi wakitegemea mlo mmoja, huku raia wana hofu ya kutoa maoni yao, bado watu wanatekwa, kupotezwa na kuuawa bila uchunguzi, huku miili ya watu inaokotwa halafu serikali inaizika bila uchunguzi...
Asante Mwanza, Asante Tanzania.