Ana ID tatuBia yetu kabadili ID anajiita kamanda
1.Bia yetu
2.Kawe allumn
3.Kamanda
Nili mblock Bia yetu na Kawe alumin naona tena kaanzisha nyingine na mblock na hiyo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ana ID tatuBia yetu kabadili ID anajiita kamanda
Haya nitakujibu mimi tu , ni mepesi sana !Ndugu Lissu, tupe majibu ya maswali haya kabla ya tarehe 28/10/2020.
====
Nawashukuru Jamiiforum.com kwa kutoa furusa hii ya kuuliza maswali. Nina imani mlengwa atayatendea haki maswali yetu kwa kuyajibu kwa ufasaha na kwa staha.
Maswali yangu ni haya kwa kuanzia.
1. Miaka kadhaa iliyopitia, Mtanzania mwenzetu ndugu Lissu, ukiwa bado mbunge ulinukuliwa ukiitakia mabaya Tanzania na watanzania wote hasa wale wenye uwezo mdogo kiuchumi. Ndugu Lissu ulinukuliwa ukisema kuwaunaitaka dunia/ ulimwengu iifungie/ iwekee vikwazo vya kiuchumi, kidiplomasia, kisiasa, kijamii na mengine kama hayo, yaani dunia itemee mate Tanzania. Kwa uhalisia vikwazo hivi vilipotumika kwenye nchi nyingine mfano Zimbabwe, Iran, hata Venezuela uathiri wananchi wenye vipato vya chini na kati, ambao kwa hapa Tanzania ndio walio walio wengi.
Je, Katika mazingira kama haya Watanzania hawa, sisi, tulio wengi tutapa sababu gani za kukuamini kuwa unaweza kuwa kiongozi wa nchi yetu na kujali maslahi ya nchi hii na watu wake wakati kwa vikwazo ulivyotuombea sisi vitupate vina lenga kukuimarisha wewe binafsi mbele ya wale ambao hawatutakii mema sisi watanzania na nchi yetu kwa ujumla wake!?
2. Siku kadhaa zilizopita ukiwa Mkoani Kilimanjaro, ulinukuliwa kupitia vyombo vya habari ikiwemo televisheni ya ITV ukisema kuwa utarudisha madaraka kwa wananchi kama ilivyokuwa wakati wa Ukoloni. Tulio wengi tunajua wakati wa ukoloni watanzani/wananchi walifanywa manamba na wengine kuuzwa nje kama watumwa.
Je, Kwa kauli hii sisi watanzania tutaachaje kuamini kuwa kipindi tu Ndugu Yetu Lissu utakapopata madaraka ya nchi hii utatuuza watanzania kwa mafungu kama bidhaa sawa na kipindi cha Ukoloni na hivyo ni halali tukunyime kura!?
3. Vyombo kadhaa vya kimataifa na baadhi vya humu nchini vimeandika habari kuwa unasimamiwa na mwansheria wa kimataifa ambaye si mtanzania. Pia wakati wamchakato wako wakupat nafasi ya kugombea inasemwa ulishawishi wajumbe wa mkutano kuvuruga wimbo wa Taifa kwa kuongeza maneno ambayo hayapo. Je, Kwa mambo yote mawili yaliyotajwa sisi watanzania tunakosaje haki ya kukunyima kura kwa kuonyesha unatudharau watanzania na pia unadharau mambo yanayotambulisha utanzania wetu!?
Karibu kwa majibu.
Source:Uchaguzi 2020 - EXCLUSIVE: Maswali kwa Mgombea Urais wa JMT, Tundu Lissu kutoka kwa Watanzania watumiao mitandao ya kijamii
====
Huku siku zikiyoyoma kuelekea siku ya Uchaguzi Mkuu, mgombea Urais anayependwa na wengi na ambaye anatarajiwa kushinda kiti hicho kwa zaidi ya 70% Tundu Lissu leo anaendelea na kampeni za kuomba nafasi hiyo kubwa kwenye Mikoa ya Manyara na Arusha .
Kama kawaida mimi mtumishi wako nitakuletea kila kinachochijiri kutoka kote inakofanyika mikutano hii .
Endelea kubaki hapa hapa JF kwa taarifa za uhakika
" TANZANIA MPYA OYEEE , RAIS MPYA OYEEE "
View attachment 1603756
=======
Babati
[16:00, 10/18/2020] New Makene Tumaini Chadema: Mkutano mkubwa wa kampeni za uchaguzi kwenye viwanja vya kwa Raha, wilayani Babati, mkoani Manyara.
Mheshimiwa Tundu Lissu akiongea na wananchi wa Babati.
Ahsanteni sana watu wa Babati kwa mapokezi na wingi wenu hapa leo. Lakini nawapa pole kwa kuumizwa kwenye hii miaka mitano. Miaka hii mitano iliyopita ni miaka ya ajabu, nalakusikitisha zaidi kwa mara ya kwanza kwenye majimbo ambayo tumeshinda mwaka huu hatuna wagombea kwa sababu ya serikali na tume ya uchaguzi wanataka CCM isitoke madarakani. Mwaka huu wagombea 35 Chadema wameenguliwa kwasabau binafsi za tume.
Watu wa Babati zimebaki siku 10, tutapiga kura Kwenye mazingira haya Haya magumu na tutashinda uchaguzi. Kitu pekee walichobaki Nacho MaCCM ni Tume ya uchaguzi. CCM wamekosa kibali cha wananchi, mikutano yao sasahivi wanakodisha wasanii. Mwaka 2015 Magufuli alikuwa anapiga push-up Ila mwaka huu anapiga magoti. Babati tarehe 28 twende tukapige kura ya ukombozi na tumshinde Magufuli na washirika wake.
Magufuli ni mtu wa ovyo, amejenga kiwanja cha ndege Kwao, lakini wananchi hawana maji. Amejenga kanisa kubwa akaliita St. Joseph akawaambia wakatoliki mje msali hapa, akaambiwa sisi hatujengewi makanisa. Magufuli amekuwa raisi wa ovyo.
Babati kwenye hii miaka mitano tumeumizwa,........
Babati zimebaki siku 10 kuelekea uchaguzi mkuu, sasa nataka niwaambie kuhusu hatari..
- Hatari ya kwanza nikuapishwa kwa Mawakala. Sheria inataka mawakala lazma waapishwe. Sasa CCM watataka mawakala wetu wasiapishwe. Tume na Wakurugenzi wanawajibu wakuwaapisha mawakala na wasipo waapisha wanataka ugomvi. Hakikisheni Mawakala wanaapishwa na wasipowaapisha wanataka ugomvi wapeni ugomvi.
- Hatari ya pili ni mawakala kuingia kwenye vituo. Tume itataka mawakala wetu wasiingie kwenye vituo. Sheria inasema tunahaki kuwa na mawakala, sasa tume wakitaka kuwazuia ni wanataka ugomvi na tuwape ugomvi.
- Hatari ya Tatu ni mawakala kunyimwa formu ya matokeo, kila wakala ana haki kupata nakala za matokeo. Formu ya matokeo ni ushahidi wa Matokeo kwenye kituo husika. Nakupewa matokeo ni muhimu.
Hatari ya nne ni CCM watatengeneza vituo hewa. Kila mahali kuna orodha ya vituo, hakikisheni mnakuwa na orodha Ili wasije wakaingizie. Hakikisheni hamuendi kwenye majumuisho ya kura.
- Hatari ya Tano ni kwenye kutangaza matokeo. Dawa yakuwazuia wasitangaze mtu ambaye hajashinda, ikifika saa sita hakikisheni mna formu za matokeo mmejumlisha matokeo na mkiona mmeshinda ingieni mtaani ijulisheni dunia. Sio kosa la jinai ukijua umeshinda na ushahidi unao ukajitangaza. Lazima tuache uoga ili tusikubali kuibiwa.
Babati tutashinda uchaguzi huu sababu watanzania wameshaamua na watafanya maamuzi, tutangazwa kwa heri au kwa shari. Jana mpwa wake Magufuli yule Kheri James wamesema hawatatumia risasi ila watatumia sindano za sumu, sasa sasa kama wanataka kufanya mchezo kuchezea uchaguzi huu wataishia thé Hegue. Wataishia kuwa wafungwa wahalifu wa Kimataifa wafanye hayo wanayoyasema.
Mwisho Babati nawaomba mtupe serikali, tupeni mamlaka tulinde haki yako na maslahi yako. Chadema tutatengeneza serikali itakayojali uhuru, haki na maendeleo ya watu.
Ahsanteni Babati na Mungu awabariki sana.
View attachment 1603956
View attachment 1603756
View attachment 1603942
View attachment 1603956View attachment 1604113View attachment 1604114View attachment 1604115View attachment 1604116View attachment 1604117View attachment 1604118View attachment 1603756
View attachment 1603942
View attachment 1603956View attachment 1604113View attachment 1604114View attachment 1604115View attachment 1604116View attachment 1604117View attachment 1604118View attachment 1604119View attachment 1604120View attachment 1604121View attachment 1604122View attachment 1604123
Wewe ni moja kati ya watu ambao wanahitaji kusaidiwa juu ya matumizi yako ya akili! Ili kukusaidia, itabidi tukuamulie nani awe kiongozi was nchi yako, upige au usipige kura, tutakuamulia!Maendeleo ya watu-Uwekezaji kwa rasilimali watu (mfano bima ya afya kupitia SWF ya gesi). Maana haina maana ya kuwekeza zaidi ya trillion 6 kwenye mradi ilihali vijana wanalia hawana mitaji ya biashara au wakulima wanalia hawana masoko au pesa za kuwekeza kilimo cha umwagiliaji.
Haki- Utawala wa sheria na siku 100 za kwanza anaanza na kuleta katiba mpya. Ataanzisha taxpayer bill of rights ili kuguarantee haki za mjasiriliamali kwenye masuala ya kodi na mifumo inayohusika.
Uhuru- Kuleta soko huria haswaa ambalo serikali haiingilii utendaji kazi wake ila inakua regulator tu. Vyombo vya habari kutoingiliwa uhuru. Wafanyabiashara kufanya kwa uhuri bila hofu ya TRA kuwalimbikizia makodi makubwa.
Karibu tujadili mapungufu au faida ya hizi sera zake.
Nmeleta sera yake umeshindwa ichambua unaanza kuleta propaganda.Wewe ni moja kati ya watu ambao wanahitaji kusaidiwa juu ya matumizi yako ya akili! Ili kukusaidia, itabidi tukuamulie nani awe kiongozi was nchi yako, upige au usipige kura, tutakuamulia!
Nisamehe bure kama nimejukwaza ila ukweli ndio huo, no way out! Ahsante, waambie na wenzio!
Wanaposema ndege sio kipaumbele hawamaanishi watu binafsi wasiwekeze kwenye aviation la hasha bali hela ya kodi ambayo inapaswa iwe reallocated kwa wote ielekezwe eneo ambalo linagusa maisha ya watu moja kwa moja.View attachment 1604230
Maendeleo ya vitu sio kabisa makamanda. Maendeleo ya watu ndio kila kitu.
Jiandaeni kisaikolojia. Oct 28, ni mkwaju kwa kwenda mbele. View attachment 1604237
Mbowe anafuja pesa za hilo genge, nyie washabiki mwatoa povu na kichangishwa kizwazwa kabisa. Hiyo saccos ya Mbowe, ni 100% mali yake mwenyewe. Watanzania makini hatuwezi chagua upuuzi, Lissu hawezi kuwa Rais wa Watanzania milele.angekuwa anahangaika sidhani kama angekuwa kapiga kampeni sehem zote alizotembelea.....kama huna hoja funga domo au cheki cartoon maybe ndio saiz yako na wana lumumba wenzako
Bora umejaribu kujitutumua kuokoa jahazi...maana wana Sumbawanga (Taja kabila), wamekula kona!!! Ha ha haaa! Turudi kwenye hoja zako.1. Sijaona swali la kisera zaidi ya speculations. 2. Sasa kweli tuuzwe kma manamba kweli? 3.Kuna nchi inakubali human slavery karne hii?
4. Vikwazo hta Mandela na Nyerere waliomba sauzi na Rhodesia ziwekewe vikwazo ili kupressure serikali zilizokua madarakani 5. je Nyerere hakujua waathirika watakua wale waafrika maskini?
6.Inaonekana uelewa wako ni mdogo wa kutofautisha nchi na serikali. 7.Yaani Lissu akipambana na magufuli mnadai anapambana na wananchi!!! 8.Hvi hamfundishwi masomo ya uraia huko mashuleni?
Nyomi kama magufuli hawezi kulipataView attachment 1604242
Najua inauma ila vumilieni tu
Kama utaendelea kuamini ya kwenye kampeni, lazima usiku wako uvurugike!Nmeleta sera yake umeshindwa ichambua unaanza kuleta propaganda.
Mtaji wa CCM ni watu wenye IQ ndogo kma ww. Nina uhakika hta ilani ya CCM hujasoma ila unashabikia tu bila reasoning!!
Hvi nkikuhoji Ajira million mbili mlizoahidi 2015 ziko wapi utajibu nni? Viwanda je? Embu tusivurugiane usiku
. ......kuwa mzalendo.....acha hasiraWapi aliwasaidia wapi? Deo mwanyika aliyefungwa kwa kukutwa na uhujumu mbona aliachiwa na kapewa na jimbo na huyo huyo mzalendo uchwara magufuli?
Akirudi hatutalimia meno,sijui tutalimia kitu gani,naona hali itakuwa ngumu zaidi ya hii miaka 5,kuminywa kwa haki kutaongezeka maradufu.Sasa imefika patamu.
Katibu Mkuu CCM na yule zezeta Popole ukiwasikiliza wanayonena sasa hivi utajua mkanganyiko tayari umeingia ndani ya chama hicho.
Hata zile 'Fiesta' sasa zimekosa maana; haziongezi chochote kwenye kampeni za mgombea wa chama hicho.
Hapa jamvini, hali haina tofauti. Akina Paskali wenye Njaa na ayohani Mbatizaji na kundi zima wamekuwa wa kuokoteza vijimaneno, au hawaonekani kabisa.
Hakika kuna jambo kubwa linategemewa kutokea hivi karibuni.
Huyu Jamaa aliyebugia shaba zaidi ya 16, ndio kwanza anaonekana kama kaongezewa damu mpya na nguvu zisizoelezeka zinatoka wapi!
Na yule mwenzake, zile 'pushup, safari hii zimegeuka na kuwa kutambaa kwa magoti, akiwalilia aliokuwa akiwafokea kama watoto wasimtupe mkono.
Lakini wapiga kura wasisahau, kiongozi anayekuwa juu ya sheria na katiba iliyomweka madarakani, wakifanya makosa baada ya kushuhudia yaliyofanyika, wakumbuke yatakayofuata wakifanya makosa tena safari hii, hawataishi kuyasahau.
Najibu original post yako maana naona unatanua mjadala kwa irrelevant issues.Ndugu Lissu, tupe majibu ya maswali haya kabla ya tarehe 28/10/2020.
====
Nawashukuru Jamiiforum.com kwa kutoa furusa hii ya kuuliza maswali. Nina imani mlengwa atayatendea haki maswali yetu kwa kuyajibu kwa ufasaha na kwa staha.
Maswali yangu ni haya kwa kuanzia.
1. Miaka kadhaa iliyopitia, Mtanzania mwenzetu ndugu Lissu, ukiwa bado mbunge ulinukuliwa ukiitakia mabaya Tanzania na watanzania wote hasa wale wenye uwezo mdogo kiuchumi. Ndugu Lissu ulinukuliwa ukisema kuwaunaitaka dunia/ ulimwengu iifungie/ iwekee vikwazo vya kiuchumi, kidiplomasia, kisiasa, kijamii na mengine kama hayo, yaani dunia itemee mate Tanzania. Kwa uhalisia vikwazo hivi vilipotumika kwenye nchi nyingine mfano Zimbabwe, Iran, hata Venezuela uathiri wananchi wenye vipato vya chini na kati, ambao kwa hapa Tanzania ndio walio walio wengi.
Je, Katika mazingira kama haya Watanzania hawa, sisi, tulio wengi tutapa sababu gani za kukuamini kuwa unaweza kuwa kiongozi wa nchi yetu na kujali maslahi ya nchi hii na watu wake wakati kwa vikwazo ulivyotuombea sisi vitupate vina lenga kukuimarisha wewe binafsi mbele ya wale ambao hawatutakii mema sisi watanzania na nchi yetu kwa ujumla wake!?
2. Siku kadhaa zilizopita ukiwa Mkoani Kilimanjaro, ulinukuliwa kupitia vyombo vya habari ikiwemo televisheni ya ITV ukisema kuwa utarudisha madaraka kwa wananchi kama ilivyokuwa wakati wa Ukoloni. Tulio wengi tunajua wakati wa ukoloni watanzani/wananchi walifanywa manamba na wengine kuuzwa nje kama watumwa.
Je, Kwa kauli hii sisi watanzania tutaachaje kuamini kuwa kipindi tu Ndugu Yetu Lissu utakapopata madaraka ya nchi hii utatuuza watanzania kwa mafungu kama bidhaa sawa na kipindi cha Ukoloni na hivyo ni halali tukunyime kura!?
3. Vyombo kadhaa vya kimataifa na baadhi vya humu nchini vimeandika habari kuwa unasimamiwa na mwansheria wa kimataifa ambaye si mtanzania. Pia wakati wamchakato wako wakupat nafasi ya kugombea inasemwa ulishawishi wajumbe wa mkutano kuvuruga wimbo wa Taifa kwa kuongeza maneno ambayo hayapo. Je, Kwa mambo yote mawili yaliyotajwa sisi watanzania tunakosaje haki ya kukunyima kura kwa kuonyesha unatudharau watanzania na pia unadharau mambo yanayotambulisha utanzania wetu!?
Karibu kwa majibu.
Source:Uchaguzi 2020 - EXCLUSIVE: Maswali kwa Mgombea Urais wa JMT, Tundu Lissu kutoka kwa Watanzania watumiao mitandao ya kijamii
====
Kipi cha kwenye kampeni? Mliahidi kwenye ilani hivyo iliwekwa kwenye mpango wa maendeleo wa miaka 5!!Kama utaendelea kuamini ya kwenye kampeni, lazima usiku wako uvurugike!
Kwa ujinga huo, tutakuamulia tena safari hii!Kipi cha kwenye kampeni? Mliahidi kwenye ilani hivyo iliwekwa kwenye mpango wa maendeleo wa miaka 5!!
Shida hamsomi mnakimbilia kucomment tu mitandaoni. Na nyie ndio mtaji wa CCM, elimu ndogo hta kuchambua ilani na bajeti hamuwezi!!
Huyo JPM toka aingie madarakani hakuna bajeti imetekelezwa kwa hta 70% ila wanaCCM wangapi wanajua?
Endeleeni tu kushabikia ujinga