Haya nendeni mkapige kura sasa then mrudi sio tumeongea wee kumng’oa dikteta jiwe alafu siku yenyewe kura hampigi. Mi nimeshangaa familia nzima wananiambia hawapigi sababu mshindi ashapangwa nikawaambia acheni ujinga, watanzania ambao wanakaa bila kupiga kura huku uwezo wanao wasije hata kulaumu wanachofanyiwa na hili.
 
Mwaka huu sijashiriki mambo ya siasa tangu Lowasa aliponiangusha akarudi CCM, jambo lililoniumiza zaidi ni kumuweka Lissu wa mwisho kwenye list, hiyo ndo sababu itakayofanya nimchague hata kama hatashinda, nitamuongezea asilimia.
Mimi pia kama wewe.
 
Eti jina la Magufuli ndo la kwanza na la Lissu ndo la mwisho!

Mambo ya kitoto sana...
Ila wamekosa plan, maana the opposite is true, sasa mtu ukimwambia akifika kwenye karatasi jina la mwisho ndio uweke tik si sawa na ukimwambia jina la kwanza ndo uweke tik, hakuna tofauti, ni ujinga tu ambao watu wachache wanaona unawasaidia!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…