Uchaguzi 2020 Yaliyojiri sehemu mbalimbali Tanzania katika zoezi la upigaji kura za Rais - Oktoba 28, 2020
Akiongea na vyombo mbalimbali vya habari vya ndani na nje, Tundu Lissu ambaye ni mgombea urais kupitia Chadema amesema kutokana na ukiukwaji mwingi wa sheria na kanuni za uchaguzi hayatambui matokeo hayo na amewataka wananchi kujiandaa kuchukua hatua zozote zile ikiwemo kuandamana kudai haki yao.

Amezitaka jumuia za kimataifa AU, UN, Commonwealth, EU, nchi za Marekani na Ulaya, marafiki, nchi jirani na watu mbalimbali kutoyatambua matokeo hayo.

Amezitaka jumuia za kimataifa kuwachukulia hatua wote waliohusika na kuvurugika kwa uchaguzi wakiwemo viongozi wa NEC, viongozi wa vyombo vya dola wao binafsi na taasisi zao.
Anajisumbua huyu. Uchaguzi umeisha sasa ajiandae tu kumaliza kesi zake mahakamani.
 
Akiongea na vyombo mbalimbali vya habari vya ndani na nje, Tundu Lissu ambaye ni mgombea urais kupitia CHADEMA amesema kutokana na ukiukwaji mwingi wa sheria na kanuni za uchaguzi hayatambui matokeo hayo na amewataka wananchi kujiandaa kuchukua hatua zozote zile ikiwemo kuandamana kudai haki yao.

Amezitaka jumuia za kimataifa AU, UN, Commonwealth, EU, nchi za Marekani na Ulaya, marafiki, nchi jirani na watu mbalimbali kutoyatambua matokeo hayo.

Amezitaka jumuia za kimataifa kuwachukulia hatua wote waliohusika na kuvurugika kwa uchaguzi wakiwemo viongozi wa NEC, viongozi wa vyombo vya dola wao binafsi na taasisi zao.
Zile nyodo zake zote za kipindi kile kumbe mweupe tu .............hao mashoga wake wameshamuacha solemba atulie Kisutu inamuita kwasasa
 
Sasa hapo Lissu ndio ameongea nini?
Yaani yeye atoke Ulaya moja kwa moja afike na kuitoa madarakani CCM iliyodumu zaidi ya miaka 20 kwenye nchi?

alafu kibaya zaidi anawaonyesha wazi wananchi kuwa watetezi na wanaomuunga mkono ni watu kutoka nje ya nchi,wakina Armstadam,kwamba yeye ni kibaraka wa wazungu?
alafu eti wampekura huyu lopolopo!?
 
Haya mnayo yaona leo ni matokeo ya mtu mmoja Mbowe ya kumleta Lowasa Ukawa,hili lilikuwa bonge la kosa ambalo kwa mtu makini kabisa kwa kosa lile alitakiwa ajihudhuru, ila Mbowe anadunda, untouchable, ukimkosoa humu watu wanakushambulia.
images (23).jpeg


Nilikiwa mwanasiasa kindakindaki wa CHADEMA chuo kuanzia 2009,ila baada ya Lowasa kuingia nilikaa pembeni,nikabezwa,nikapondwa baada ya UKAWA kupata viti vyingi bungeni,ila baada ya wabunge kuanza kurudi CCM ,kuna watu niliwaambia 2020 hali itakuwa mbaya sana na leo tuna yaona.

CHADEMA mlivyo mleta Lowasa UKAWA na kujiamini kwamba mpo imara,kumbe mliacha nyumba yenu mliyokuwa mnaijenga kidogo kidogo kwenye mwamba na kwenda kujenga kwenye mchanga kisa tu kuna urahisi.Sasa angalieni leo mnayo yapata ni haki yenu hamjaibiwa hata kura moja.

CHADEMA mkitaka kusimama tena mnabidi muanze upya mfumue chama chote na mkijenge CHAMA kupitia vijana wenu na watu wenu mlio waandaa nyinyi na si kunyakua wanasiasa kutoka CCM na mnatakiwa kiwaamini watu wenu.
 
Yaani uzuri ni kwamba ni sisi Watanzania ndio tutakao faidi au kuumia na maamuzi yetu wala sio viongozi tulio watuma
 
Back
Top Bottom