Japo wapo watakaodai ushindi ni ushindi tu, kwangu uchaguzi huu umeivua nguo, umemvua nguo na umewavua nguo.
Nchini , kikanda na kimataifa! hii ni aibu na fedheha sana kwa Taifa.
Japo wapo watakaosherehekea aina hii ya ushindi, kwangu naamini wengi nafsi zao zinawasuta na hawaamini walichokishuhudia.
Yaani hata CCM huku mitaani utaona nyuso zao zinavyowasuta. Ni aibu ya taifa. Aibu haina chama!
Magufuli ataingia kwenye vitabu vya historia kama kiongozi aliyewazindua Watanzania wadai upya nchi yao kutoka kwa wakoloni mamboleo, CCM.
Nina shock si ya matokeo bali hali ilivyo. Miaka 5 upinzani ulipigwa marufuku. Miaka 5 ya chama kutangaza sera za madaraja, midege, na flyovers. Miaka 5 ya manunuzi ya madiwani na Wabunge. Miaka 5 ya matumizi ya fedha za umma mengine bila uhakiki. Miaka 5 ya kutesa wapinzani, kutishwa n.k.
Sikutegemea ushindi unaoongozwa na Jeshi la Polisi(OCD Hai), TCRA kuhangaika na mitandao, TBC na propaganda, NEC na Msajili wa vyama kusaidia chama bado yametokea haya
1. Wananchi kuonyesha chuki wazi wazi
2. Upinzani kufufuka kutoka majivu hadi kushindwa na dola na si chama
3. Kubwa kuliko yote, aisee , Inachukiwa, Anachukiwa, wanachukiwa hadi inatisha
Kwa watu wenye akili timamu na fikra sahihi wanaoongozwa na ubinadamuna utu, kuna kitu cha kujiuliza
Kwanini , kwanini , kwanini! Nini kinapelekea kuchukiwa kiasi hiki.
Chuki niliyooina dhidi yao, yake na wao imenitisha na kusikitisha sana. Hilo ndilo lime ni shock!