Uchaguzi 2020 Yaliyojiri upigaji kura za maoni za wagombea wa Ubunge na ujumbe wa Baraza la Wawakilishi kupitia CCM - Julai 20-21, 2020
CCM inapendwa sana. Huu uzi unakimbia kwa spidi ya SGR
Hahahha... Ule uzi wa unaohusu kura za maoni huko chadema una karibia wiki 2 na una coment 440

Huu wa ccm ni wa leo kakini tayari coment ni 460
 
Kuna wabunge wa kuteuliwa atamfikiria huyu mvuta bangi,Mtulia,Lijualikali,Waitara,Kalanga.

Wengine wanaweza kupewa ukatibu tawala au ukuu wa wilaya.

Nafikir wakishika nyadhifa hizo wasahau tena ubunge.
Kumbuka nafasi za ubunge wa Kuteua anazo 10 tu mkuu.

Ila nafasi ya dac/ras/dc kipindi hiki imeshushwa sana aisee,itachukua muda sana kurudisha hadhi yake.3
 
Hata matapta wanataka kwenda bungeni?? Daaah sijui nani ameondoa ''utakatifu'' wa bunge
Marcas ni mwonevu, hafai hata kuwa katibu kata. Marcas nilimkuta mahali ameonea mwananchi, waandishi wa habari waliokuwa wanafatilia tukio marcas aliwaambia atawatoboa macho. Tena hadharani akijitapa Hamna wa kimfanya kitu. Marcas hafai,,, watu wanauonaje ubunge???

Sent from my Infinix X653 using JamiiForums mobile app
 
Jam
Embu fafanunua vizuri Mkuu, Ukisemaccm imenunuliwa mahali fulani inanunuliawaje?
Jamaa alitembeza mlungula miaka miwili nyuma akishirikiana na mwenyekiti.na anayenunua chama mwaka 2015 alikuwa kampeni meja wa mwenyekiti huyo kugombea ubunge Jimbo la Moshi akakosa.sasa wamebadillisha karata kuwa aliyekuwa meneja kampeni Sasa apewa Jimbo na aliyekosa ubunge 2015 Sasa Ni mwenyekiti .chama kimenunuliwa na kitakaa mikononi mwa watu wawili.huko kigamboni bado wanaendelea kuhesabu Kura.
 
Kuhusu Kigamboni naomba mwenye matokeo ya uhakika awe anatujuza.

Ieleweke Kigamboni ndipo anapogombea aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam na ambaye kwa namna moja ama nyingine aligusa watu wengi walio kubaliana naye na walio kuwa hawakubaliani naye.

Hivyo kwa mada hii naomba tujuzane kwa yanayojili huko Kigamboni.
 
Back
Top Bottom