Uchaguzi 2020 Yaliyojiri upigaji kura za maoni za wagombea wa Ubunge na ujumbe wa Baraza la Wawakilishi kupitia CCM - Julai 20-21, 2020
Hali ni tete sana kwa Dr Mwakyembe Kyela.

huenda akaangushwa na mpambe wake kwa jina la Kinanasi
 
Macho na masikio yangu yapo Same Mashariki,Mchuano mkali ni kati ya Daudi Mambo vs Mama Anna Kilango Malechela ambae mwaka 2015 alipeperusha bendera akasababisha CCM kupoteza jimbo.
 
Haya kumeshakucha tena La mgambo likilia ujue kuna jambo.


Kwa mujibu wa ratiba ya CCM, leo na kesho ni siku ya Mikutano Mikuu ya CCM ya Majimbo/Wilaya kupiga kura za maoni za wagombea wa ubunge na ujumbe wa baraza la wawakilishi

Kwa Mujibu wa Mwenyekiti wa CCM, Dkt. Magufuli waliochukua kugombea nafasi za Ubunge na uwakilishi ni 10,367. Waliokamilisha kujaza fomu na kurejesha ni 10,321.

Watanzania wataelekeza zaidi macho na masikio yao maeneo yenye upinzani mkali kama Kigamboni, Arusha mjini, Simanjiro, Kyela, Mbeya mjini, Mwibara, Misungwi, Same Mashariki, Tunduma, Tarime Vijijini na Ubungo ni baadhi ya maeneo yanayoangaliwa kwa jicho la tatu.

Ngoja tuone.

Up dates:

Jimbo la kinondoni jumla ya waliochukuwa fomu ni 81 na waliorejesha ni 79 ambao wanaendelea kujieleza .

Jimbo la Ubungo waliochukuwa fomu ni 113 na waliorejesha ni 111 na wanaendelea kujieleza, Mbarouk Masoud ambaye ni Katibu mwenezi anasema zege halilali.

Arusha mjini kuna watia nia 91 wanaoendelea kujieleza.

Jimbo la Lupembe mkoani Njombe watia nia 19 wanajieleza.

Abas Tarimba anaongoza kwa wingi wa kura za maoni Kinondoni akifuatiwa kwa ukaribu na IDD AZAN kura bado zinaendelea kuhesabiwa mubashara.
Mwamba alieunga juhudi kinondoni hali mbaya akipata kura 5 ashukuru laana ntakuelekeza jimbo ndio inamrudia😂😂😂
 
Habari za mchana huu kwa Atmosphere ya sehemu ambayo kura za maoni zinapigwa makonda paul anaenda kuchukua jimbo


Chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ni Ngome ya makonda wapiga kura wengi ni wanafunzi wa serikali ya wanafunzi chuoni MASO

Sijui icho chuo ni cha chama cha mapinduzi CCM au hapo sijafahamu vizuri

mnaoshindana na makonda mjiandae kisaikolojia tu

Mpoki haufikishi kura ata 8
 
Macho na masikio yangu yapo Same Mashariki,Mchuano mkali ni kati ya Daudi Mambo vs Mama Anna Kilango Malechela ambae mwaka 2015 alipeperusha bendera akasababisha CCM kupoteza jimbo. Huku Daudi Mambo ni Kijana msomi na Mwenye maarifa na kipenzi cha vijana wa Same
 
Kwa mfumo wa sasa wa ccm kura za maoni hazina maana yoyote ile maana anaweza chukuliwa hata mtu aliopata kura sifuri


Makonda atakumbana na baba yake

Maana ndio alisema.... kushinda maoni dodoma wanaamua upyaaaaaa
 
Nipo Ughaibuni, Bwana Mdogo wangu mmoja amenipenyeshea hapa, kwamba upepo mwingi unaonekana kumwelekea Bwana Kalist lazaro;

Maendeleo hayana Vyama
 
Back
Top Bottom