Uchaguzi 2020 Yaliyojiri upigaji kura za maoni za wagombea wa Ubunge na ujumbe wa Baraza la Wawakilishi kupitia CCM - Julai 20-21, 2020
Wanaccm kigamboni wamemkubali
Mkateni halafu mumpe huyo wowowo wenu muone uchaguzi utakavyokuwa simple kwa wapinzani
Ndungulile kwa Kigamboni anakubalika hadi na wapinzani
Naongea kama mkazi wa Kigamboni nitakayepiga kura.
Wapinzani wa kigamboni ipi ww na kwa lipi alilofanya kigamboni ww ...hebu niambie tangu achaguliwe 2015 huko kwenu alishakuja kusikiliza kero hebu kua mkweli
 
kiti cha Siha warudie kupiga kura tena baina ya Mollel na Mwanri. Tofauti waliyonayo siyo signficant kuonyesha mshindi; inabidi Kweka aondolewe zipigwe kura baina ya hao wawili tu

View attachment 1511955

Vile vile jimbo la Buchosa Mwanza warudia kupiga kura baina yaShigongo na Tizeba kwani wamefungana

Dkt. Charles Tizeba – 354
Eric Shigongo James – 354


Nassari kaangukia pua ya nguvu kweli kweli huko Arumeru Mashariki; atakoma kimbelembele

View attachment 1511958
Hapo kwa Mwanri na Mollel kuna namna hapoo...
 
Ukweli ndo huo, Mkuu anaweza kutumia yaliyomkuta Makonda Kigamboni kujitathmini na kujirekebisha inapobidi Badala ya kutunga Sheria za Kutoshitakiwa..

Makonda ameadhibiwa na WanaCCM kwa Sababu yake..

Makonda alivyo Chukizo, Ndivyo naye alivyo..:Wala ASIJIDANGANYE na ASIDANGANYWE

Katika Uchaguzi Huru na wa Haki, anachakazwa na Lissu mpaka ataita maji mmaa

Hapendwi Kihivo
Subiri Ifike 2023/2024

He will be Ignored mchana kweupe, Kwani yeye nani bana!
 
HONGERA Dk Tulia Ackson ,sugu lazima afungashwe virago Kyala akutule nkamu gwangu
 
Mpe Makonda moyo. Lakini Makonda sio mgeni, alikuwa Rc hapo Dar. Na Kigamboni ni eneo ndani ya Dar.. Kwa maneno nafupi ni kwamba Makonda hakuwa ana kubalika kama Rc Dar
Ushindi ni ushindi hata kura moja ni ushindi..
Fuatlia kwa Ndugai kongwa,isbani kwa lukuvi,Arusha mrisho Gambo halafu uje hapa tena
 
Nakumbuka kabisa ambavyo mlinihakikishia kuwa Mtu anaenda ' Kumalizwa ' kwa namna ya Kipekee kabisa na hatoamini Macho na Masikio yake nikawa ' nawabishia ' hatimaye kile kile mmekifanya. Kwa Furaha Kubwa niliyonayo kwa Kazi yenu nzuri nashindwa Kuendelea Kuandika hapa ila naomba mkubali na mpokee hizi Zawadi za Wanyama Mbuzi Watano ili mkachinje mle huko Makwenu na Familia zenu.

Hata Ubebwe vipi, utumie Vitisho gani na utumie Pesa zako za Dhuluma ila Mwenyezi Mungu akisema NO huwa anamaanisha NO mazima hasa.
Mnaenda kumuuza mtu hauzi. Matokeo magumu bila ile kamati aliyokuwa anaiongoza. Shikamoo JPM. Kweli Rais tunaye, maana ukibeep tu, yeye anapiga. Hasubiri kesho itakuwaje
 
Ukitathimni matokeo ya uchaguzi wa jimbo la kigamboni ,Nzega mjini,Mtama utaona wakongwe waliotetea majimbo yao , Bashe na Nape Nauye wamewaacha mbali sana wapinzani wao ,mfano Nape anakura Mia nne na ushee anayemfatia Ana kura miambili na Bashe kapiga kura miatatu na ushee, anaemfatia ana kura kumi na mbili .

Kwa kigamboni Ndugulile alitakiwa amuaache mbali sana Makonda ,kwa sababu ni mbunge jimbo hilo kwa miaka 10,halafu anatofautiana na mgeni kwa kura 68, hii si nzuri kwake. Kama ilivyoada kwa ccm kuongoza kura za maoni sio tiketi ya jina kurudi.


Safari ndio imeanza kuhusu hili jimbo la kigamboni,wagombea wakapitishwe kwenye kamati ya wilaya ya siasa ,kamati ya mkoa ya siasa kisha yapelekwe Dodoma kwa wazee cardinal rule ndio jina lirudi. Wale mnaompinga Makonda msishangilie kwa sasa, baadae msije kujikuta mnasonya
Inategemea na uyo mgeni ana nguvu kiasi gani, Ndugulile amepatta ushind mkubwa sana huo...kaangalie kwa Nchemba sasa
 
Matendo mabaya yana sauti kuliko matendo mazuri..

Sasa rasmi kigamboni wameunga juhudi za marekani kukemea udhalimu kwenye roho za watu..

Marekani asikanyage na kigamboni mwiko, wanambunge wao.
Ukweli ndo huo, Mkuu anaweza kutumia yaliyomkuta Makonda Kigamboni kujitathmini na kujirekebisha inapobidi Badala ya kutunga Sheria za Kutoshitakiwa..

Makonda ameadhibiwa na WanaCCM kwa Sababu yake..

Makonda alivyo Chukizo, Ndivyo naye alivyo..:Wala ASIJIDANGANYE na ASIDANGANYWE

Hapendwi Kihivo
Subiri Ifike 2023/2024

He will be Ignored mchana kweupe, Kwani yeye nani bana!
 
Ndugu unamjua Koola?
Huyo Engineer ni mwamba kweli kweli huko CCM Vunjo. Kuna watu wengi huko Uchagani wameshangaa kumuona Kimei ameweza kuleta huo ushindani.
Nina uhakika CCM hawataweza kumkata Koola, hata iweje. Kama Magufuli anampenda sana Kimei ili ampe waziri, basi atasubiri kuja kumteua kwa ubunge wa viti maalum ikiwa Magufuli atautwaa tena urais.

Lakini fahamu tu hili, hakuna mchaga atayevuna uwaziri chini ya utawala huu wa Magufuli, sembuse uwaziri wa Fedha.
CCM wapishaacha ule upuuzi wao na hatutegemei malalamiko kwa wagombea
 
Jamani mchakato bado kabisa, naona watu wanawehuka kwamba haya matokeo kura za maoni ndio mwisho wa kila kitu

Kumbe sio hivyo, majina bado yataendelea kuchujwa sana tu, na mwishowe yatapelekwa kwenye kamati ya WATU 24 ikiongozwa na Mwenyekiti, kwahio kuna possibility kubwa waliobwagwa au "watoto pendwa" wanaweza kupata.

Mambo bado kabisa!
 
Back
Top Bottom