Clever505
JF-Expert Member
- Jul 27, 2020
- 2,282
- 3,351
🤣Sasa we jamaa,😁😁😁
Wee jamaa uongo unakupa faida gani asee
Ila kwakua unajileta mwenyewe kwenye mfumo acha tukupe dawa uache wenge
Kwanza khaibar hawakuvamiwa wao walikua na makubaliano na wao ndio waloanza kuvunja makubaliano
Pili baada ya wao kupigwa mama yetu saffiyah alipewa option achague mwenyewe
1.Asislimu awe kafiri kama alivyokua awali ila arudi kwa jamaa zake
2.Aslimu halafu s a w amuoe tena hakulazimishwa alitakiwa akubali mwenyewe
(Kwanza kwenye sharti za kutimu ndoa inatakiwa muolewaji aridhie jamaa uache kudanganya watu hapa ndani)
Muhammad aliuua kaka, baba na mume wa safiyyah halafu safiyyah kirahisi aolewe na muuaji wa wapendwa wake?
Kuwa serious japo kidogo mkuu.
Unasema akapewa chaguo kwamba asilimu aolewe na muuaji ama abaki na dini yake arudi kwao. Hivi kwa akili ya kawaida we unaweza kuishi kwa upendo na mtu aliyeua familia yako yote?
Aaaaaaaaaah ni uongo ulioje huu!😁
Alilazimishwa huyu,
Ok najaribu kuwaza kuwa hakulazimishwa ila inawezekana vipi awe na upendo na Muhammad kwa tukio hilo la mudi kuiua familia yake?
Hapo maelezo marefu yanahitajika kunielekeza ili nielewe.
Au labda aliwaza kwamba nyumbani hakuna kitu tena, ndugu wameuawa, Mali zimechukuliwa na Muhammad na marafiki zake, akaona ataenda wapi sasa! Akakubali kilazima kulingana na Hali aliyoihisi itakuwa mbaya zaidi akiwa kwao.
Akaona Bora aishi hata na asiowapenda ila ni sehemu salama kuliko akirudi kwenye dhiki, kama haya mawazo yangu yatakuwa sahihi, jibu ni wazi bado ameolewa kilazima