Mkuu, kila jambo hutokea kwa sababu maalum na hushughulikiwa kwa sababu maalum.
Kama wafahamu yapo majaribu ya Mungu na yapo majaribu ya shetani.
Shetwani alipomjaribu Yesu kule milimani alimwonyesha ulimwengu na akamuahidi kwamba endapo Yesu angejitupa basi shetwani angempa madaraka ya kumiliki duniani yote na malai zake.
Lakini jaribio lile la shetwani kwa Yesu lilikuwa ni la kuonyesha matumizi mabaya ya madaraka yanavyoweza kumsahaulisha binadamu na akasahau kuwa kuna Mungu.
Mungu ndio kimbilio la wanaomhitaji na yeye ndie mponyaji wa wale wapatao taabu za dunia hii.
Tumwogope Mungu kwani ndie hutoa madaraka kwa wateule wachache na huwawezesha binadamu hao kuwa na nguvu na wasioyumba.
Wachache hao wakiyumba au kutetereka basi Mungu huwapa matumani na huwaponya kwa imani yao kwake.
majaribu ya Mungu humpa nguvu zaidi yule anaejaribiwa.
Hivyo, achana na hadithi na tetesi za mitandaoni maana hizi, zipo siku zote.