Yuko wapi Rais Magufuli? Msiache tetesi zienee. Kama anaumwa mnasema "ANAUMWA"

Yuko wapi Rais Magufuli? Msiache tetesi zienee. Kama anaumwa mnasema "ANAUMWA"

Status
Not open for further replies.
Mzee wangu nakuheshimu sana na ninaungana na wewe watoe taarifa Kama anaumwa ila sioni kuwa ni sahihi ikiwa haumwi watoe taarifa kwa ajili ya kujibu tuhuma maana hawa wapuuzi wamekua wakizusha sio Mara moja wala mbili ni kawaida yao, je unaona ni sahihi kuwajibu hivo tuhuma zao ovu kila Mara?
Huu "uzushi" sasa hivi ni mkubwa sana. Lazima ujibiwe, sio lazima iwe maneno, anaweza akaenda hata kumsalimia Kikwete inatosha.

Hii imekuwa kubwa kuliko, kwa wiki 2 haonekani, Lissu akaongea jambo. Nation ndio gazeti kubwa kabisa Kenya, limeandika hii habari. Sio jambo dogo.

Wewe umeona namna gani familia ya malkia ilivyojitokeza haraka kujibu interview ya Prince Harry. PR ni kitu muhimu, huwezi kusema waache waongee.
 
Mi naona tupige kimya tu as long as hakuna kitu kilichosimama kutokana na ukimya wake, kama tukio litatokea lenye ulazima wa kutangazwa ama kama kuna ishu inashindikana kufanyika na inamuhusu basi lisemwe linalotakiwa kusemwa.
 
Rais wetu yuko imara, Mungu anamtunza na kumlinda. Matarajio ya shetani na vibaraka wake wameshindwa na wataaibika vibaya!

Kwanza wengi wao wanaishi nje ya nchi kama wakimbizi kwa hiari yao wenyewe!! Wako kama Yule mwana mpotevu wa kwenye Biblia!! Hivi mtu na akili yako utaondokaje Tanzania kwa mfano halafu ukaishi ughaibuni ambako hakuna anayeheshimu hata utu wako?

Dunia na ijue kuwa Tanzania tuko vizuri Sana na tunampenda Sana Rais wetu!!
 
Ifike mahali wakizusha ikabainika sio kweli wakione cha mtema kuni

Walimzushia Sabaya, kaonekana mzima hana hata dalili na bila aibu wapo tu wanadunda
Hata wakatiule (2019) walizusha mabaya na kufanya fujo zote mitandaoni. Alipoonekana akawatangazia msamaha kama alivyofanya Mhe. Mpango na Mhe. Sabaya
 
  • Thanks
Reactions: T11
Kwani ile ya china ilikuwa feki.Au ipo kwenye majaribio.Dawa za madagascar je ni og au feki, kujifukiza na maombi hata navyo vimeshindwa?
Mmoja alisema yapo makundi mengine ya damu dawa zinadunda.
 
Mkuu, kila jambo hutokea kwa sababu maalum na hushughulikiwa kwa sababu maalum.

Kama wafahamu yapo majaribu ya Mungu na yapo majaribu ya shetani.

Shetwani alipomjaribu Yesu kule milimani alimwonyesha ulimwengu na akamuahidi kwamba endapo Yesu angejitupa basi shetwani angempa madaraka ya kumiliki duniani yote na malai zake.

Lakini jaribio lile la shetwani kwa Yesu lilikuwa ni la kuonyesha matumizi mabaya ya madaraka yanavyoweza kumsahaulisha binadamu na akasahau kuwa kuna Mungu.

Mungu ndio kimbilio la wanaomhitaji na yeye ndie mponyaji wa wale wapatao taabu za dunia hii.

Tumwogope Mungu kwani ndie hutoa madaraka kwa wateule wachache na huwawezesha binadamu hao kuwa na nguvu na wasioyumba.

Wachache hao wakiyumba au kutetereka basi Mungu huwapa matumani na huwaponya kwa imani yao kwake.

majaribu ya Mungu humpa nguvu zaidi yule anaejaribiwa.

Hivyo, achana na hadithi na tetesi za mitandaoni maana hizi, zipo siku zote.
 
Njia pekee na nzuri yakumtesa kiumbe mwongo na anayeokoteza maneno nikukaa kimya pale anapokuitaji useme.

Wanaharakati wengi huko mitandaoni wanamtafuta Presidaa ,wanazusha mambo na Sasa wameanza kushambuliana wenyewe kwa wenyewe. Kisa tu presidaa katulia ajjawafokea.

Baadhi yao wameanza kusoma na katiba kukoleza uongo wao, nawashauri wasome kila kitu ila Presidaa atazidi kuwanyonya maarifa maana wamezoe kuishi na kutafuta popularity kupitia kauli zao. Mzee ameamua atulie asome na kutengeneza mikakati ya kesho.

Ametulia anachambua wanaomfaa na wasiomfaa kisha atumbue alete watu wenye kasi. Msimtingishe mzee mwacheni asome mafaili atoe maamuzi mshudie Bashiru Ally akileta safu mpya Kama Katibu mkuu kiongozi.

Nikutakue afya njema, nikutakie kazi njema nakukuombe usisononeke moyoni mwako Mwamini Mungu ukitambua mti wenye matunda ndo upigwa mawe.
 
Waambie hilo gazeti linaloitwa Nation, Lisu na Ngurumo wampige picha huko Nairobi na watume Tanzania na waweke kwenye mitandao yao! Sijui wanakwama wapi kuleta ushahidi wa hayo maneno yao!!
 
Sijasikia winbo wa taifa redioni muda mrefu! Kipindi cha Nyerere ukisikia wimbo wa taifa tu RTD unajua kimenuka!

Namtakia Rais wetu afya njema na maisha marefu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom