Sikitai watoto kufanya mitahani hata kila siku. Ila napinga ni kwa nini iwe kila siku mitihani tena asubuhi alfajiri. Elimu anayopewa mtoto ni yakukariri na kufaulu mitahini na wala sidhani kama itamsadia sana mtoto hapo baadae endapo atakosa ajira.
Mtoto wa namna hii anaamini akifaulu mtihani na kupata daraja la kwanza basi atapata ajira nzuri na ndivyo anavyoambiwa na walimu wake. Ifike mahali tuwe wa kweli kuwa sera yetu ya elimu inanapungufu kiasi. Hili la kwenda kufanya mitihani asubuhi alfajiri na kwenda shule jumamosi mpaka jion mimi siliafiki.
Waliopanga ratiba ya masono walikuwa wanaakili timamu na kuna vigezo walizingatia ndio maana wakaweka muda wa kusoma ni kuanzia jumatatu hadi ijumaa tena saa kumi.
Watoto wetu wanahitaji muda wa ziada wa kutembelea ndugu na marafiki, kusaidia wazazi majukumu mbalimbali kama ya shamba na biashara na kurefresh pia. Sasa ukimchukua mtoto wiki nzima unamkaririsha notes kwa ajili ya kufaulu mtihani ni kweli anaweza kifaulu lakini akawa hana maarifa yeyote yatakayomsadia kupambana na maisha ya kwenye jamii maana hayuko familiar na jamii mda mwingi anautumia shule na waalimu wake.
Nakumbuka enzi sisi tunasoma tulikuwa tunamashamba ya shule tunalima, tulikuwa na stadi za kazi na zilitusaidia sana, sasa hivi ambapo dunia inasonga mbele kwenye sayansi na technolojia hii mitaala sina hakika kama bado ipo.
Nilitegemea wanafunzi wa shule zetu hizi watumie mda wa ziada baada ya masomo kufanya mambo ya ziada hasa yanayolenge kutambua vipaji vyao ambavyo vingekuwa ni ajira kwao na pia vingekuwa na msaada mkubwa wa kiuchumi kwa taifa hapo baadae.
Kwa dunia ya leo sanaa, michezo na technolojia ndio vyanzo vikubwa vya mapato kwa watu na nchi pia. Tumeona wanamichezo, wanamuziki, wanariadha waigizaji na wabunifu mbalimbali wanavyojipatia kipato na kuchangia kwenye uchumi wa nchi zao. Mfano mzuri ni wanageria hawa jamaa wamesoma sana lakini pia utawakuta wapo karibu kila ligi kuu ya ulaya wakisakata kabumbu na wanachangia mapato kwa taifa lao.
Utaratibu huu wa ufundishaji kama wa Tanga unaenda kuuwa vipaji vya baadhi ya watoto labda kama wangekuwa wanafundishwa na physical education.
Najua kuna watu humu mtakuja kunipinga bila kuweka ushahidi wenye kueleweka. Kunabaadhi ya ajira zinazotoka na michezo tumeanza kuzipoteza kwa wageni na hii inachangiwa na vijana wetu kubanwa huku mashuleni muda wote bila kuzingatia ratiba hasa za michezo, talent show na sanaa. Tumeona hata kwenye ligi yetu ya sasa tumetawaliwa na wakongomani kila sehemu kuanzia mabeki hadi forward, hatufahamu hizi ni ajira tena zenye mapato makubwa tu. Wachezaji kama Joseph Kaniki Kumbakumba, Emanueli Gabrieli, Sekilojo Chambua, Bonifas Pawasa, Lunyamila, Nteze John Lungu, Ally Mayai Tembele, wazawa hawa waliotawala ligi yetu kipindi mpira haulipi kwa sasa hawapo tena.
Kipindi sisi tunasoma tulikuwa na break yaani mapunziko saa nne asabuhi hadi saa nne na nusu na saa tisa na nusu hadi saa kumi kila siku. Muda huo tuliutumia kucheza mpira, uzwiji, korosho, arita bao au kwenda kudokoa miwa kwenye mashamba ya wahindi au kwenda kuogelea tena kwenye mito yenye vina virefu kwa sisi wanaume na wasichana waliutumia kucheza rede, mdako au kukaa kwenye vikundi vikundi na kujadili mambo yao au ya watu wengine huku wengine wakibaki kuwa watazamaji wa hii michezo. Na hii haikuathiri uwezo wetu wa kitaaluma yaani unamkuta mtu darasani wa moto, kwenye mpira wa moto akipelekwe shamba wa moto na siku za weekend unamkuta kasimamia biashara ya baba yake kama duka au mashine ya kusaga na kule pia ni wa moto. Na hapo bado kunasiku mzee anaweza kukuzuia usinde shule akuchunge ng'ombe au ukang'olee mpunga au ukalinde ngedera mashambani na ukapoteza vipindi vya siku mbili tatu ila ukirudi shule akaandika notes na msela wako akakubrash kidogo unakuwa wa moto.
Baada ya mwanafunzi kujua kusoma na kuandika elimu yetu ilipaswa kumjenga huyo mwanafunzi kuwa mbobezi katika kada fulani, kama ni kilimo, mifugo, uvuvi, michezo ubunifu, biashara siasa n.k la sivyo tutaendelea kuwa na vijana wenye vyeti na ufaulu mzuri ila maarifa madogo, hii itapelekea kila wakati serikali kulalamikiwa kuwa haitoi ajira kwa vijana na ukweli ni kuwa srikali inaajiri kwa vipaumbele, hakuna serikali inayoweza kuajiri graduates wa vyuo vyote na fani zote kila mwaka.