Countrywide
JF-Expert Member
- Mar 2, 2015
- 20,694
- 32,527
Wanawake wa Tanga ni walalamishi sana, sijui mna shida gani
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
We need a timetable to be followed upuuzi huu zamani haukuwepo and all was well!Walimu ndo wanafundisha wanaelewa changamoto za watoto wanapojifunza kama hutaki mtoto wako afundishwe muda wa ziada wasiliana nao watamruhusu mapema arudi nyumbani apumzike kama unavyotaka usitafute justification kuharibu mipango mizuri ya walimu kwa hawa watoto.
Tunasema tunayo yaona , huwezi kuwa na uangalizi wa watoto 200 darasani, never . How can you control them and make learning take place effectively? Unajua maana ya learning ad how it is effected?Kipi bora kwa mtazamo wako!
Ni bora hilo darasa lenye watoto 200 lenye uangalizi wa huyo mwalimu mmoja kuliko atoke mapema ili akalindwe na shamba boy.
unajua kinachoendelea shuleni? Shule ya watot elfu 2 kwa walimu kumi kuna uangalizi gani? Think deep!SHULE NI SOCIAL ORGANIZATION KUBWA AMBAPO KILA KITU KWA MTOTO ANAKIPATA kwani hata michezo ipo na inakuwa na uangalizi bora kutoka kwa walimu.
Ulitaka wafanye bure?Pamoja na mambo yote lakini mtoto anatakiwa apate muda wa kupumzisha mwili na akili. Ashiriki kufanya kazi za nyumbani hata kwakiasi kidogo sana.
Ukitazama hao wanao wasaidia wanafunzi muda wa ziada(WENGI WAO) wanalenga hela kwahiyo kama hamna hela huduma haipo.
Maisha yanataka kwenda kwa kazi na kupumzika. Mtatia watoto uwendawazimu
zamani hakukua na shinikizo la kufaulisha, hata likifeli darasa zima poa Tu. Sasa hiv tamisemi wamekuja na Key performing Indicators, shule zimepewa malengo zifikie, kila mwalim, kila shule, kila wilaya na kila mkoa wanatakiwa kuwa na mpango kazi kufikia malengo.hili jambo huwa naliwaza na kulisema kila siku. Nimesoma msingi miaka ya 90. Tuliingia shule saa 2 mpaka saa 8 na hii ilikuwa ni Jumatatu mpaka Ijumaa, darasa la kwanza mpaka la saba.
Sasa najiuliza leo wanafundishwa nini cha ziada kiasi kuwekwa mashule mpaka saa 1 usiku, Jumapili wanakwenda shule pia. Matokeo yakitoka na uoza ule ule.
sasa hapo shida ni walimu au wizara?Watoto wa saiv wanatakiwa kufundishwa kwa vitendo kuliko kukaririshwa na tatizo waalimu sio wabunifu. Na mitaala imebakia kukaririsha masuala ya vita vya maji maji badala ya kwenda na wakati wa technology. Yanayofundishwa veta yangepelekwa shule ya msingi ingependeza sana
Mimi nilikua na mtoto st fransis mbeya, Mtoto akifunga shule anakuja na maswali mengi Sana, Yan akitoka chumbani ni kuja Kula na kurudi chumbani kufanya maswali mpaka wanafungua, mpaka namuonea huruma mtoto. Matokeo kutoka watoto wote one za Saba na nane chache, Nina mtoto mwingine lasaba mwaka huu wazaz tumetoa mil 1 Kwajil ya masomo ya ziada, ELIMU ni gharama, hakuna kizuri chabureKuna baadhi ya wazazi wanaoelewa maana ya elimu bora wanaona kugharamika wao ili watoto wao wapate elimu bora japo elimu yetu ndio hivyoo ina changamoto nyingi
heb ukipata muda fatilia shule binafsi zinazofanya vizuri, unaweza kuta hayo matus umeyapeleka kusiko sahihiHakika wewe ni fala sana.
Inaelekea huna elimu yoyote ktk bichwa lako.
Shule kama hiyo na zingine za namna hiyo hakuna elimu yoyote wanayopata watoto hapo. Ni mateso na kukonda tu.
Sana sana wanakaririshwa maswali tu. Baada ya miezi 2 au 3 Kila kitu hakuna kichwani.
Walioweka mapumziko ya likizo Kwa ajili ya mtoto walikuwa na akili sanaaaa .
unaongelea zamani ipi, Kwanza zamani ilikua likizo lazima twende tution maana walimu walikua hawamaliz topics, kama hujaenda tution unakuja kuomba rafiki akufundishe. Zamani hakukua na shinikizo walimu wafaulishe, hivyo ilikua ukikaa kusubir ufundishwe kila kitu imekula kwako. O level nimesoma mpwapwa sec na advance MusomaWe need a timetable to be followed upuuzi huu zamani haukuwepo and all was well!
mtaala wa zamani ukoje wenye makosa mengi?Mimi kitu ninachoshangaa sio mitihani ila mitihani inatungwa kwa mtaala wa zamani.mitihani ina makosa mengi sana.
Serikali inataka wanafunzi wafaulu wote kwa 100%.kwahyo walimu lazima wajiongeze kwa kila mbinu
hiyo mitihani ya alfajiri ni kwa madarasa yote au yale yanayojitayarisha na mitihani mwisho wa mwaka huu?1. Kila asubuhi watoto eti wanafanya mitihani. Mtoto anawajibika kuripoti shuleni saa 12 asubuhi na kuanza mtihani saa 12.30 asubuhi.
Kwa uwingi wa watoto kwa darasa moja pale Olympio na level ya ufaulu wanayopata ni sahihi kabisa njia wanayotumia.Niliangalia matokeo darasa la saba Olympio darasa lina wahitimu zaidi ya 600.Ndiyo maana wazazi wengi wanapeleka watoto wao hapo maana ni nafuu na bado inashindana na shule nyingi za Private zenye ada kubwa.Kuna shule inaitwa Diamond na mwenzie Olympio. Hawa jamaa mpaka jumapili watoto wa darasa la saba wanakwenda shule na wasipoenda walimu wanapiga kama wanapiga mwizi. Ukihoji kama mzazi unaambiwa ndio tushapanga kama shule.
Serikali kuna haja wakaja na kauli moja kuhusu swala la elimu na masaa ya masomo. Tunakoelekea watoto watakuwa hawapati hata muda wa kulala.
Hoja yangu silengi kama wafundishwe bure hoja nimuda wa mapumziko angalau mwili na akili vipumue. Inavyoonekana sikuhizi hata likizo hazina maana.
Wewe ndio kichwa maji,unafikiri kazi ni kufundisha mda wote!Waalimu wengi vichwa maji, mtoto unamfundisha saa 11 jioni ana njaa ataelewa nini
Ndo maana watu wanazarau waalimu