Afrika hakuna nchi vyama vya upinzani vimeleta nafuu kwa wananchi vikifika Ikulu

The most important fact is that people have the right to choose freely whomever they want, nothing more nothing less.
Kuna tofauti kati ya inavyotakiwa kuwa na ilivyo. Katika ideal situation mgombea anatakiwa kumwambia ukweli mpiga kura kuhusu nini wataweza kufanya na nini hawataweza ili mpiga kura afanye informed choice kati ya wagombea aliowasikiliza. Lakini hali ilivyo sasa sio hivyo, mgombea anawadanganya wapiga kura kuwa yeye akipewa kura atakuwa mwarubaini wa matatizo yooote ya tz ya vijana, wazee, wakinamama, watoto, wajane na yatima. Haelezi atafanyaje kwa pesa na technologia gani kutoka wapi kwa mashariti gani. Haelezi hela za kampeni anapewa na nani huko nje kwa mashiriti yapi kama akishinda uchaguzi. Askofu anawaambia waumini wake kura zote mpeni X na sheikh ivoivo, na mkuu wa kabila ivoivo.

Hata hivyo my null hypothesis inasema hakuna tofauti ya maendeleo Africa kati ya nchi zinazoongozwa na vyama vya ukombozi na nchi zinazoongozwa na vyama vipya vya saisa (vya upinzani). Sasa wewe njoo na takwimu za kupinga the null hyppthesis yangu hii. Sitaki utumie hisia zako au matusi.

Indicators ziwe: Levels of democracy, economy, human rights and social services.
 
Zambia, Malawi
Lini zilikuwa matajiri hizo nchi ili tupime umasikini wao baada ya wapinzani kuingia madarakani? Kenya hapo KANU iko kaburini, na uchumi wa Kenya ni mzuri kuliko wa sisi tunaotawaliwa na ccm kwa shuruti.
 
Unachoongea sio sahihi. Uchaguzi wa 2030 hakuna mtoto wa binadamu mwenye akili atakubali kushiriki vurugu kama zile. Zile vurugu hazikuwa kwa ajili ya kupinga uchaguzi bali kuipindua serikali. Na waliopanga na kushiriki sio chadema tu, agenda zilikuwa nyingi pale. Sio 2030 tu bali hata ukiitisha maandamano leo hupati tena vijana kama wale. Wale vijana waliingizwa mkenge tu na wahuni.
 
Sasa kamanda kama mlitia mpira kwapani ambayo ni haki yenu kuna shida gani mkae kimya msubiri awamu nyingine mshiriki au nayo msuse.
 
Tumetaka iundwe tume huru ya kuchunguza matukio yale na sababu zake, hamtaki mnatuletea taarifa za majizi ya kura na walioua vijana wetu ili mkae madarakani kwa shuruti. Usituletee habari za wanaotaka kujisafisha kwa kuficha ukweli. Tunataka tume ya kweli itaakayaanza na taarifa za kweli kuanzia utakeja, ufiraji wa watu, kura 31m zilipotokea nk. Unaniletea porojo za kubumba wakati ukweli halisi hamko tayari uchunguzwe!
 
Walipanga kupindua serekali, kisha kiongozi wa serekali akatangazwa kwa kura 31m za kupika! Ngoja uone kama waalimu watawekwa kwenye kachumba kupiga kura za uongo tena, ama polisi watasimamia mabox ya kura fake kuingizwa vituoni. Kubalini tume huru ichunguze kiini cha matatizo, na sio kupika taarifa za kuficha ukweli na kuzua uongo
 
Vyovyote vile kama mfumo wa vyama vingi umekubalika ni haki watu washindanishwe fairly, you can't bring the negativity kwenye 'yajayo'.
Unadai haujaona tofauti ya wale wanaobalisha vyama na wale wanaoendelea na chama hichohicho(here obviously you mean no matter how cruelty, remorselessly and brutally they become to win the election), this is disgustingly pathetic kwani ule uhuru tu wa kuongea kwamba kiongozi fulani na wala haumpendi pasina hofu ya kutekwa au kuuawa ni jambo la muhimu mno.
Uhuru na haki ni maendeleo pia, wakoloni walikuwa na mifumo bora na development programs zaidi viongozi wazawa lakini bado watu walipambania uhuru, SA during the apartheid era ilikuwa na viwango bora na standard ya maisha ya first world lakini walipambana kutokomeza huo mfumo hapo ndiyo ufahamu kuwa freedom na justice ni vya kupambania at any cost.
 
Tume
Shida yenu hiyo tume huru ya kimataifa ya uchunguzi hamtaki wajumbe wa kimataifa watoke China, Urusi, Cuba au N.Korea, mnataka watoke Ulaya Magharibi ambao tayari wameshaonyesha upande wao kwenye mgogoro. Hiyo nayo haikubaliki maana hap wajumbe kutoka EU na commonwealth wana conflict of interest na mzozo. Kwanza, CCM ndio chama kilichowafukuza tz, pili ni wafadhili wa chadema na Lissu. Walimtibu Lissu kwa gharama zao, ni mtu wao.

Kama wajumbe watatoka chama cha united Russia cha Urusi mtasema tume sio huru, maandazi!!
 
Well said. Mimi ninaamini kwa dhati hakuna bunduki inayoweza kuzuia nguvu ya umma kama siku ikiuchoka mfumo kandamizi kwao. Hapa kwetu sisi hali kama hiyo bado iko mbali sana kutokea kwasababu mfumo bado haujawabana sana watu kiasi cha umma kuitumia hiyo turufu yao kuuondoa mfumo unaowabana kupitiliza.

Tunachokiona sasa hapa kwetu ni mtu su kakikundi ka watu wachache wanaojaribu kuwaelimisha watu ili waukatae mfumo uliopo. Katika kufanya hivyo mfumo unawaona watu hao kama wachochezi wa umma ambao hauna kero wala shida na mfumo. Vurugu za Oct29 hazikufua dafu kutokana na ukweli huo kuwa umma haukushiriki ipasavyo kwenye vurugu kinyume na matarajio ya kundi. Hata baada ya Mh. Lissu kuwa magereza umma unaendelea na pilikapilika zao za kawaida as if nothing is happening kwa mwenyekiti. Hii ilikuwa tofauti kwa case ya Mandela ambae umma wa SA ya weusi na wadau wengine nje ya SA walikuwa wanavibrate na ku oscillate pamoja na Mandela.
 
Vyama vya upinzani afrika vinasawazisha uwanja kabla ya kujenga. Kumbuka vyama vyote vilivyoleta uhuru afrika vimetibuatibua uwanja wa kujenga nchi zao kwa sababu walidai uhuru bila kujua watazijenga vipi nchi zao kiuchumi. Walijikita zaidi kulifukuza gari kama mbwa bila kujua wakilifikia watalifanya nini. Sasa vyama vya upinzani vimekuja kuondoa hizo mentality za vikundi vya watu kujifanya wao kupitia vyama vyao ni wamiliki wa wananchi wa nchi zao kama wazungu walivyojiona ni wamiliki wa wananchi wanao watawala.
 
Punguza unafiki.Ndio maana nasema bakini na CCM yenu kwani shida Nini? Iwatawale mpaka mwisho wa Dunia. Mnatumia visingizio vya kinafikia kutweza upinzani.
 
Hiyo common factor ni Raia wajinga. Waafrica wote Kwa asilimia 99 Bado ni wajinga na Bado wana akili za wanyama.

Ndio maana viongozi walionyooka watapondwa na hao hao raia achilia mbali viongozi wenzake.

Leo hapa Tanzania akifa Kiongozi ambae hajajilimbikizia Mali wananchi wote watasema alikuwa Hana akili.

Hivi unadhani huyo mwananchi akiwa Kiongozi ataleta mabadiriko?


Viongozi ni sehemu ya jamii. Huwez kupata Kiongozi Bora kutoka katika jamii corrupt.
 
One step at a time, it took ages and a lot of international pressure mpaka apartheid ikapigwa chini hivyo mapambano dhidi ya udhalimu unaofanywa na watawala wa TZ bado yana safari isiyo nyepesi ila gradually yanaendelea kukua, katika ya mapambano huwa kuna traitors, two headed serpents na sellouts na hao ndiyo hurudisha nyuma, huchelewesha na kupambana kukatisha tamaa harakati.
Mapambano ya October-29th-2025 dhidi ya udhalimu wa Samia ni mfano halisi kwani yale mauaji aliyoyatekeleza huyo Samia na genge ni sawa na mauaji yaliyofanywa na SA apartheid regime yale ya Sharpeville massacre ya 1960 na baadaye mapambano makubwa zaidi na mauaji makubwa zaidi ya Soweto massacre(Soweto uprising) ya 1976. Ukiangalia revolt growth ya 1960 ilikuwa ni ndogo lakini wakati oppression ikiongezeka na watu wanakuwa more determined tena hao watu ni teens si watu wazima ndipo 1976 revolt ikawa kubwa na mauaji yakawa makubwa zaidi huku good numbers za Wazulu(Kwazulu Natal natives) waki-support utawala huo dhalimu kwani chifu wao alikuwa ni chawa wa Makaburu. A lot of similarities with our current pathetic TZ scenarios.
 
Kama huna facts acha kuleta hoja ambazo hazina back-up ya statistics. Unaposema hudhani... unaleta hisia badala ya facts
 
Toka 1961 mpaka 2026 wakazi Dar bado wanalalamikia huduma za elimu, afya, maji, umeme na barabara mbovu. Usilolijua, mwaka 1961 tunapata Uhuru pesa yetu ilikuwa na thamani sawa na ya Uingereza na India mna Kenya; leo pesa yetu iko chini ya nchi tajwa huku sisi tukijivunia kuongoza kwa machawa, pia Indonesia na China zilikuwa masikini kama Tanganyika lakini leo hatuna tofauti na mwaka 1971 wakati wa maduka ya kaya bidhaa toka Kenya na China.
Naomba unielewe sikukatishi tamaa endelea na uchawa, uchawa unalipa chap.
 
Ww ni bendera fuata upepo, nina uhakika huna ujualo. Unaweza ukasema ni shilingi ngapi cdm wanapatiwa na hizo nchi za magharibi, na ni kiasi gani nchi inapata toka kwa hizo nchi za magharibi ili tupime nani ni mfaidika halisi wa hizo hela za wazungu? Walipendekezwa sio hao wa Ulaya tu, bali ni Jumuiya ya AU na SADC, ama nao hawa wana maslahi na cdm?

Hao China sijui North Korea unaotaka wawe kwenye hiyo tume, wana sifa za diplomasia, ama ni kuwachukua tu? Ni sawa na leo ukatafute coach wa team ya mpira wa miguu toka China ama Korea kaskazini, utakuwa na akili timamu kweli? Kama umeishiwa na hoja piga kimya.
 
Kuwaza kwa aina hii safari yetu ya maendeleo inaonekana bado ndefu sana wallah.

Tanzania iko huru tayari baada ya kuwafukuza wazungu wa Ulaya Magaribi ambao waliligawana bara letu tukiwemo sisi kwasabu ya kupata malighafi za bwerere kama madini, pamba, pembe za ndovu, nk, kupata wafanyakazi (nguvukazi) wa ujira mdogo (manamba, watumwa) na masoko ya kuuzia bidhaa zao walizozalisha kwenye viwanda vyao kama vile nguo, sukari, shanga, vioo, bunduki, sahani, nk. Mahitaji haya bado wanayo mpaka leo hii ninapoandika hapa hatabkama vyama vya ukombozi viliwafukuza physically kutoka Afrika na kupata huo wanaouita uhuru.

Kwa kuwafukuza wazungu kutoka Afrika vyama vya ukombozi vilikosana sana na wazungu maana ziko nchi kama tz ambazo zilikwenda mbali zaidi kwa kutaifisha "mali zao" kama vile ardhi, mashamba viwanda, mashule; na mbaya zaidi zilihamia upande wa Urusi na China kiitikadi. Ugomvi ulikuwa mkubwa kiasi kwamba viongozi wengi waliowafukuza wakoloni na kuonekana kuwakatia upatikanaji wa malighafi, nguvukazi na masoko ya bidhaa zao waliwaondoa au waliuliwa na kuweka watu wao (viongozi mataahila) ambao wangewahakikishia upatikaji wa zile rasilimali, nguvukazi na masoko ya bidhaa zao bila vikwazo. Nchi za magharibi haziwezi kusurvive bila kupata rasilimali/malighafi ya bure, nguvu kazi rahisi na masoko ya bidhaa zao.

Vyama vya upinzani vyooye 100% Afrika huwa vinapata msaada wa kujijenga, kujiendesha na kupambana na vyama vya ukombozi kutoka nchi zilezile zilizofukuzwa Afrika na vyama vya ukomnozi kama CCM, ANC, Frelimo, etc. Vyama vyote vya upinzani ni vyama rafiki na nchi za Magharibi, na sio rafiki wa nchi za Mashariki kama China, Urusi, Cuba au N.Korea. Jiulize ni kwanini chadema sio rafiki wa China au Urusi?. Maana yake ni nchi zilezile ambazo zilikuwa wakoloni wetu ndiyo zinakuwa nyuma ya vyama vyetu vya upinzani Afrika.

Na inafahamika agenda kuu ya nchi za Magharibi (wakoloni wetu) ni malighafi rahisi, nguvukazi rahisi na masoko rahisi ya bidhaa zao. Hivyo, tunaweza kusema moja kwamoja kuwa demokrasia safi kwa jicho la nchi za Magharibi ni vyama vya upinzani wanavyovilea na kuvipatia fedha zao kushinda uchaguzi, kinyume na hapo uchaguzi haukua huru na haki. Katika hali tu ya kawaida kama mwanafunzi wako akifeli na wewebmwalimu wake utahesabiwa umefeli, hivyo kushindwa kwa vyama vya upinzani Afrika ni kushindwa kwa wakoloni pia; comments zao lazima ziwe nyingi na negatives kuhusu chaguzi zetu. Na wakishindwa kwenye chaguzi wako tayari kusupport kijeshi, lengo likiwa kupata rasilimali rahisi, nguvukazi na masoko kutoka kwa wanaemsapoti.

CCM ni chama cha ukombozi kinachosambaza nchi nzima huduma za umeme, maji, elimu, afya, barabara, reli, pembejeo, ardhi kwa kila mtanzania na uchimbaji madini kwa kila mtanzania. Ubaya wa CCM uko wapi ili wote tuwe na ufahamu mmoja. Mpaka sasa vyama vya upinzani vinashindwa kuwashawishi watanzania ili nao wauone ubaya wa CCM na waunge mkono kile wanachokisema vyama vya upinzani.

Watanzania nao wana akili, macho, masikio na pua ya kunusa na mikono ya kupapasia. Wanaona wenyewe kwa macho yao:
1. Amani na utulivu
2. Mgawanyo wa ardhi yao, kila mtu ni rahisi kipata kipande
3. Huduma za usafiri
4. Huma za umeme
5. Elimu kila kijiji, kila kata
6. Afya kila kijiji, kila kata kila tarafa kila wilaya
7. Michezo, timu zetu zinafanya vizuri na ligi imejaa wachezaji wageni
8. Chakula kipo
9. Madini yanachimbwi
10. BANDARIA zinatema. Etc.

Watanzania hawa pia huwa wanatembea nchi nyingine za Afrika na kujifanyia benchmarking na wenzao, wanajiona ama wako sawa nao au wamewazidi mbali sana kwenye ardhi, amani, afya, etc.
 
Mnyika alitangaza hadharani kuwa amerudisha fedha za wazungu ambazo hazikutumika, zimekosa activity. Nchi ni yetu tunaelimishana tu huma usiwe too much defensive, inawezekakana wewe na mimi hakuna anaepata hata sh 1 ya CCM wala chadema. Tuongee facts. Mimi sina ugomvi binafsi na chadema, ni madau tu wa ukweli, amani na utulivu baasi. Hata yule Mzee Lwaitama ni mwalimu wangu wa communication skills pale chuoni kwake, nampenda sana, ni rafiki yangu.
 
KUna yofauti kubwa kati ya exchange rates na purchasing power. Pesa yetu ina uwezo mkubwa wa kununua kuliko fedha ya Kenya.

Pesa ya China iko chini kuliko US dola lakini hela ya China ina nguvu kubwa ya manunizi kuliko dola. Kashule kanahitajika hapo mwenzangu ka kutofautisha kati ya nguvu ya kubadilisha fedha, nguvu ya kununua na ughali wa maisha kwenye nchi husika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…