Arusha: Ole Sabaya na wenzake wamefikishwa Mahakamani, kesi yaahirishwa
View attachment 1822472

Aliyekua DC wa Hai Lengai Ole Sabaya pamoja na wenzake leo wamefikishwa tena kwenye Mahakama ya Wilaya iliyopo Sekei Arusha,ili kujibu tuhuma zinazowakabili, Sabaya na wenzake wanakabiliwa na mashtaka matano.

Itakumbukwa June 04,2021 Sabaya na wenzake walifikishwa Mahakamani hapo ambapo baadaye Tumaini Kweka, Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Taifa ya Mashtaka anayeshughulika na usimamizi wa kesi alisema———-“uchunguzi katika baadhi ya makosa yanayomkabili Lengai na wenzake umefikia kwenye kiwango ambacho tunasema ni tamati ya kuweza kuwafikisha Mahakamani”

“Mkurugenzi wa Mashtaka baada ya kujiridhisha kwamba kweli tuhuma zilizokua zinamkabiki Lengai na wenzake kisheria zinatengeneza kosa akaamua leo wafikishwe Mahakamani, kama mlivyoona alikua akituhumiwa kuongoza magenge ya kihalifu, vitendo vya rushwa, kutakatisha fedha haramu ambayo ni matokeo ya vitendo vya rushwa”

“Vilevile Mkurugenzi alijiridhisha kwamba kuna unyang'anyi wa kutumia silaha, ndio maana amefikishwa Mahakamani leo kwa hayo makosa matano lakini kwa unyang'anyi wa kutumia silaha ni makosa mawili aliyatenda katika wakati mmoja lakini kwa wakati tofautitofauti, na kama tuhuma nyingine zitathibitika basi Mkurugenzi wa Mashtaka ataamua vinginevyo"

My Take
Mahakama na DPP huu ndiyo wa kutuaminisha umahiri wenu. Chapa ilale
JAMBAZI afikishwa mahakamani.

GOD FATHER wake huko mawinguni kwa malaika haoni hili, si alikuwa anampa kiburi?
Bado Juma Raibu na wenzake
 
Mbona wanamuwahisha mapema Sana mahakamani kwann asikae kama miaka 6 hivi kama wazee wa escrow au uhamsho kusubiria ushahidi kukamilika ndipo aanze pelekwa mahakamani.
Wamuwahishe tu kumpeleka huko Mahakamani, na ikiwezekana wamfunge kabisa mapema iwezekanavyo, ili Mataga wenzake waache kuanzisha nyuzi humu kila baada ya dakika kadhaa kumlilia Mataga na jambazi mwenzao.
 
Kesi inayomkabili Ole Sabaya na walinzi wake imetajwa tena kwenye Mahakama ya Arusha na kuahirishwa hadi July 2 , kwa kile ambacho mwendesha mashitaka amedai upelelezi wake bado haujakamilika .

Sabaya ambaye Suti aliyoivaa leo inaonekana kumpwaya , amerejeshwa rumande ya Kisongo akisubiri kesi itakapotajwa tena .
"Upelelezi wake bado haujakamilika"-kasentensi katamu sana haka, hii ngoma inaweza kwenda hadi 2025 kwa kutumia tu hako kasentensi.
 
Back
Top Bottom