Arusha: Rais Samia ashiriki Maadhimisho ya Miaka 60 ya KKKT - Agosti 21, 2023
Safi Rais wetu, tupo pamoja na Rais wetu.
Kamwe asikubali kuyumba wala kuyumbishwa na waraka za kinafiki, chapa kazi songs mbele wananchi tunamtegemea.
 
Bila kupepesa macho, Rais Samia ameongea haya kanisani KKKT leo

---https://twitter.com/millardayo/status/1693589311843684651?t=NzjjjyFL8-WdjMrZJaeVfQ&s=19

Niliamua kunyamaza na naendelea kunyamaza. Hakuna mwenye misuli ya kuligawa Taifa.
Misuli hiyo na mabavu anayo yeye mwenyewe kwa hiyo asiulize maswali ambayo yeye ndio mwenye majibu
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Maadhimisho ya Miaka 60 ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) katika Chuo cha Tumaini Makumira – Arusha leo tarehe 21 Agosti, 2023.



DKT. FREDRICK SHOO - ASKOFU MKUU WA KKKT

- Hatupingi uwekezaji
Viongozi wa Dini zote kwa uwakilishi tuliomba kuja kukuona (Rais Samia) mwanzoni mwa jambo hili, kwa ungwana ukatupokea na tukakukabidhi maoni yetu na ukaahidi utayawasilisha kwa wataalam kufanyiwa kazi kwa maslahi mapana ya Taifa.

Naomba ieleweke wazi Kanisa linaunga mkono uwekezaji, hatupingingi uwekezaji na tunajua wewe kwenye nia yako unataka uwekezaji, hata hivyo jambo hilo limekuwa na maoni mbalimbali ya wananchi na vyombo vya habari, lakini Mheshimiwa Rais tunatambua kwamba sisi viongozi wa dini zote tuliomba kuja kukuona pale mwanzoni na ulitupokea na tulikuletea maoni yetu kama viongozi wakuu wa dini, ukaahidi kuwa maoni yatafanyiwa kazi, tuna imani na wewe"

Ninatambua kuwa ulipokea kijiti katika mazingira magumu sana, lakini pia pamoja na mazingira yale wewe ukaanza historia mpya ya nchi yetu ya kuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya Urais, kuna wengi hawakuamini, hawakutaki na mpaka leo wamebaki na jinamizi la namna hii, huu ulikuwa ni mpango wa Mungu

- Mungu amekujalia Hekima

Najua katika jambo hilo linaelekea mahali tunataka kugawanyika kabisa, wengine wanatumia sababu za kidini, wengine wana maslahi yao ya kisiasa na kiuchumi, nashukuru Mungu amekujalia hekima kama mama na kiongozi, umekaa kimya

- Tusiwagawe watu kwa utofauti wa Dini
Umoja wa Taifa letu la Tanzania, mshikamano ni muhimu kuliko Mtu au kundi lolote, niwaombe Viongozi wenzangu wa Dini zote, niwaombe Wanasiasa, kuacha kabisa kujaribu kuwagawa Watu kwa misingi ya Dini au kwa misingi ya itikadi iwayo yoyote ya kisiasa na kwa misingi ya maslahi binafsi

Niombe Serikali yako kukataa na kukemea kwa nguvu yote wale wote wanaoonesha dalili za kutugawa kwa utofauti wa Dini zetu, hata pale Mtu anaposema jambo la kuipendeza Serikali iwapo amejenga hoja yake katika msingi wa kutugawa kidini au kwasababu nyingine yoyote huyo akemewe, tumkatae hana nia njema

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

- Uharibifu wa mazingira

Katika nchi kama yetu ambayo asilimia kubwa tunategemea kilimo, madhara ya mabadiliko ya tabia nchi ni makubwa zaidi, binafsi nafarijika kuona viongozi wa dini wanalipigia kelele jambo hili, ningetamani kuona kila taasisi ya dini inajiwekea mkakati mahususi wa kupambana na uharibifu wa mazingira.

- Hakuna mwenye msuli wa kuharibu amani yetu
Ndugu zangu, na hususani Baba Askofu Shoo, Kaka yangu Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT, nimeyasikia yote uliyoyasema kuhusu usalama, amani, umoja na mwendelezo wa Taifa letu, niliamua kunyazama kimya na naendelea kunyama kimya, ninachotaka kuwahakikishia hakuna mwenye misuli na ubavu wa kuligawa Taifa hili, hakuna mwenye misuli na ubavu wa kuuza Taifa hili

Hakuna mwenye misuli na ubavu wa kuharibu amani na usalama tuliojenga kwenye Taifa hili, hayo itoshe kuwa ni ujumbe wangu kwenu, asanteni sana

Mbona maoni yao aliyopewa hajayafanyia kazi anaachia vitu vile vile kama ulivyo mkataba vikiendelea kutekelezwa? Kwanini aliamuru wananchi waliokuwa wakipinga kuwakamata na kuwafungulia kesi ya makosa yasiyokuwepo?
 
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) limetoa msimamo wa kuunga mkono Uwekezaji wa Bandari.

Mkuu wa Kanisa hilo, Askofu FREDRICK SHOO ametoa msimamo huo leo Agosti 21, 2023 Mkoani Arusha.

=========

Naomba ieleweke wazi Kanisa linaunga mkono uwekezaji, hatupingi uwekezaji na tunajua wewe kwenye nia yako unataka uwekezaji, hata hivyo jambo hilo limekuwa na maoni mbalimbali ya wananchi na vyombo vya habari, lakini Mheshimiwa Rais tunatambua kwamba sisi viongozi wa dini zote tuliomba kuja kukuona pale mwanzoni na ulitupokea na tulikuletea maoni yetu kama viongozi wakuu wa dini, ukaahidi kuwa maoni yatafanyiwa kazi, tuna imani na wewe
Kwa hiyo hapo ameunga mkono au amesisitiza waliyompelekea yatekelezwe?
 
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) limetoa msimamo wa kuunga mkono Uwekezaji wa Bandari.

Mkuu wa Kanisa hilo, Askofu FREDRICK SHOO ametoa msimamo huo leo Agosti 21, 2023 Mkoani Arusha.

=========

Naomba ieleweke wazi Kanisa linaunga mkono uwekezaji, hatupingi uwekezaji na tunajua wewe kwenye nia yako unataka uwekezaji, hata hivyo jambo hilo limekuwa na maoni mbalimbali ya wananchi na vyombo vya habari, lakini Mheshimiwa Rais tunatambua kwamba sisi viongozi wa dini zote tuliomba kuja kukuona pale mwanzoni na ulitupokea na tulikuletea maoni yetu kama viongozi wakuu wa dini, ukaahidi kuwa maoni yatafanyiwa kazi, tuna imani na wewe
Mbona unajitekenya mwenyewe na kucheka? Unadanganya unadhani kuwa utapata nafuu na waarabu wako? Hatutaki waarabu ni makatili.
Ona hapa wanavyoua wahamiaji.
 
Kuna cost kubwa kuwanenea uongo watumishi wa Mungu.
😂😂 mtumish wa Mungu unamjua ww ukimuona?? nyie ndo mnao waabudu viongoz wenu wadini.. kumbuka hao si malaika ni binadawamu kama wew.. njaa zinawauma kama ww inavyokuuma
 
Shoo kamwambia kihekima ili ajiongeze kuukataa huo mkataba wa kihuni au kurekebisha vipengele tata. Na akamkumbusha wanasiasa wasipende kuwaambia viongozi wa dini kuwa wanachanganya dini na siasa wakati wanatetea taifa lao.
 
Bila kupepesa macho, Rais Samia ameongea haya kanisani KKKT leo

---https://twitter.com/millardayo/status/1693589311843684651?t=NzjjjyFL8-WdjMrZJaeVfQ&s=19

Niliamua kunyamaza na naendelea kunyamaza. Hakuna mwenye misuli ya kuligawa Taifa.
Kama "...Hakuna mwenye misuli na ubavu wa kuligawa Taifa...." kwanini Dk Slaa, Mdude na Mwabhukusi walikamatwa na kubambikwa kesi ya uhaini usiokuwepo?
 
Huu mkataba wa DP World utakuwa una matatizo ndio maana hata Rais anakosa courage ya kuusifia waziwazi.

Naona kama anaendelea kujificha ingawa alipata jukwaa zuuri ya kumaliza utata uliopo lakini hakufanya hivyo!!!.
Hilo la kuukaa kimya ndo analolimudu ,baa ya kulikoroga ,kkk naona wanauma na kupuliza
 
Back
Top Bottom