Askofu Mkuu Jimbo Kuu Katoliki Mwanza awataka wanyonge kukataa wanaomtukana Hayati Magufuli

Hawa ndio wanafanya tuache kutoa sadaka. Siwezi kutoa sadaka ili mtu mjinga kama huyu akaishi kwa raha.
 
Ni kweli. JPM apingwe kwa mabaya yake na sio kwa mazuri yake. Asante Baba Askofu kwa Kuliona Hilo.
 
Hata makaburu huko south Africa walijenga miundombinu bora,jpm ni liuaji likemewe to hell
 
Askofu mkabila na mdini , hakuyaona aliyo kuwa akiyafanya huyo muhuni anayemtetea hapo? Askofu mzima anatumia neno wanyonge kama silaha anasahau hata biblia imekataa unyonge! Akanye mbele askofu uchwara huyo.
Ustaadh imefunga kweli!?
 
Askofu mkabila na mdini , hakuyaona aliyo kuwa akiyafanya huyo muhuni anayemtetea hapo? Askofu mzima anatumia neno wanyonge kama silaha anasahau hata biblia imekataa unyonge! Akanye mbele askofu uchwara huyo.
Una mzigo wa takataka kichwani,
 
Mpumbavu ni yule maskini wa hikra kama wewe,
 
Lenatus Nkwande anajielewa sana sio kama wale waliochukua hela za escrow kwenye sandarusi.
Chawa wa mama na ufipa watapita kimya kimya.
askofu uchwara wakati utekaji unafanyika walikuwa kimya leo anabwabwaja maana sponsor wao kafa wajinga hao ndio maana namkubali sana RUWAICH NA FR. KITIMA.
 
Japo mimi ni mkatoliki, huyu askofu ananikwaza sana. Hivi hajui mkristo wake Tundu lisu alivyofanywa kwa amri ya huyo jamaa. Hivi hayo anayosema ni mazuri aliyofanya alifanya kwa hela ya mfukoni mwake?
Amesahau askofu mwenzake wa Rulenge alivyofanywa?
Amesahau Kodi mashirika ya kanisa yalivyobambikwa. Nachelea kusema huyu halustahili kuitwa askofu mkuu, Mungu anisamehe
 
Lenatus Nkwande anajielewa sana sio kama wale waliochukua hela za escrow kwenye sandarusi.
Chawa wa mama na ufipa watapita kimya kimya.
Mimi ni mwumini wa Kanisa Katoliki, na nimekuwa karibu sana na baadhi ya viongozi wa Kanisa kama maaskofu na mapadre Lakini niwe mkweli wa nafsi yangu, kuwa taasisi hii kubwa, licha ya mwongozo wake ulio thabiti, lakini inaongozwa na wanadamu. Na mwanadamu, siyo wakati wote anakuwa sahihi. Kuna wakati hulka ya mtu haimwachi kwa sababu yupo kwenye nafasi fulani, na kuna wakati ushawishi wa mwili unazidi nguvu ya Roho. Na ndiyo maana utasikia mengi pia yasiyopendeza yanayowagusa viongozi wa Kanisa. Na hiyo siyo kwa Kanisa Katoliki pekee, bali ni kwa taasisi zote za dini.

Lililo jema kwa Kanisa Katoliki, ni taasisi, siyo Kanisa la mtu mmoja. Hivyo kukitokea makosa ya mtu mmoja au kikundi fulani, makosa hayo yanaweza kudumu kwa muda tu, na baadaye husahihishwa.

Wakati wa utawala wa marehemu Magufuli Kanisa liliyumba sana. Na hiyo siyo kauli yangu. Kauli hii ilitamkwa na Askofu mmoja (siwezi kumtaja), mbele ya mapadre wake wawili, na mimi nisiye padre nikiwepo.

Alisema hivi:

"Mnakumbuka tulitoa waraka wa Kwaresma, na tukaigusa Serikali. Tulieleza kuzorota kwa haki na demokrasia, tukstaja matukio kadhaa: kushambuliwa kwa risasi Tundu Lisu, watu kutekwa, maiti kupatikana kwenye viroba, na mengine yasiyopendeza. Baada ya waraka ule watawala hawakupenda, na hasa Rais. Mambo mengi ya hovyo yakaanza. Vitu vya Kanisa na taasisi za Kanisa vinavyotoka nje tukaambiwa tulipie kodi. Kanisa Katoliki la Tanzania miaka yote limefurahia uhusiano mzuri na Serikali zote. Haya sasa yakawa mapya. Kwa hiyo kipindi cha Askofu Ngalelikumtwa kilipoisha, kulikuwa na mjadala mkali juu ya nani awe Rais wa TEC. Ndipo likatolewa pendekezo lililokubaliwa kuwa atafutwe mtu ambaye ana ukaribu au tuseme urafiki binafsi na Rais. Na kazi yake ya kwanza iwe ni kutafuta kurudisha uhusiano mzuri na Serikali. Lilifanyika hivyo. Na baada ya hapo, kodi zote kwa vitu vinavyotoka nje kwaajili ya Kanisa na taasisi zake, ikaondolewa. Sisi wengine, tuliona kuna ukakasi mkubwa lilipotolewa pendekezo lile la kumchagua Rais wa TEC kwa kigezo kuwa awe ni mtu mwenye urafiki binafsi na Rais. Lakini ikawa hivyo, kwa sababu Kanisa halijazoea purukushani dhidi ya Serikali"

Nimeyaweka haya, ili tufahamu kuwa japo hawa maaskofu na mapadre ni mababa wetu wa kuroho lakini kuna wakati matashi yao binafsi yanawaondoa kwenye ukweli.

Sitarajii Askofu au Padre au shekhe, asimame na kusema kuwa lazima usiku na mchana tumseme marehemu yeyote yule kwa sababu alifanya ubaya fulani. Dini zote zinafundisha kusamehe. Lakini pia kumsifia mtu fulani kuwa aliwapigania wanyonge, wakati huo huo kuna waraka wa TEC unaoonya juu ya matendo yasiyofaa dhidi yake, siyo sahihi.
 
Tunawafahamu maaskofu na wachungaji SKG hasa wewe askofu. Umeharibu Mwanza kuliko ilivyokuwa kanisa kuu linajengwa huku likitafunwa!. Umebakia kulinda wezi mapadre ambao wamebaki kujengea nyumba michepuko kwa fedha za michango ya waumini. NKWANDE mungu anakuona!
 
Pamoja kwamba wewe ni Baba wangu kiimani lakini Magufuri atasemwa kwa ubaya mpaka mwisho wa dunia kwa sababu alipenda vitu na akawachukia watumiaji wa vitu kwa kutuletea sheria mbaya za kitapeli.
 
Amen mtumishi.

Hao tunashughulika nao hao.
 
Kuna watu wanaficha madhaifu ya uwajibikaji duni kwa kupambana na marehemu, huu nao ni ujuha.....bora baba Askofu ameliona hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…