Ndugu zangu Watanzania,
Rais Samia anaendelea kupokea na kumiminiwa pongezi kutoka taasisi mbalimbali ndani na nje ya Nchi. Kutokana na ushindi mnono na wa kishindo alioupata katika uchaguzi Mkuu uliofanyika Mwezi uliopita . Ambapo Taifa lilishuhudia Rais wetu kipenzi cha watanzania akiibuka kidedea kwa kupata ushindi wa 98% wa kura zote.
Ushindi ambao ulichagizwa na uchapakazi wake na kazi kubwa aliyoifanya ndani ya muda mfupi wa uongozi wake. Ambapo kila mtanzania mamilioni kwa mamilioni waliamua kumpigia kura za ndio ili aendeleze kazi njema aliyoianza katika awamu yake ya kwanza ya uongozi wake.
Embu soma Hapa 👉Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za Kiislamu nchini, limelaani vikali vitendo vya uhalifu vilivyotokea wakati na baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025, na kuisihi serikali kufanya uchunguzi wa kina kubaini chanzo na vinara wa machafuko hayo.
Katika tamko lililotolewa siku ya Alhamisi, viongozi wa taasisi hizo wamesema tukio hilo limeacha majonzi makubwa kutokana na vifo vya watu wasio na hatia, ulemavu wa kudumu, na uharibifu wa mali na miundombinu ya umma na binafsi.
Viongozi hao wameeleza kuwa kabla ya uchaguzi mkuu, walifanya jitihada kubwa kuhimiza utunzaji wa amani, wakisisitiza kuwa kudai haki ni jambo la msingi, lakini lisifanywe kwa njia zinazohatarisha usalama wa taifa.
BAKWATA imeiomba serikali kuwa na jicho la huruma kwa familia zilizopoteza ndugu zao, waliojeruhiwa au kuathirika kwa njia yoyote katika machafuko hayo, huku ikiitaka pia kuchukua hatua dhidi ya wale ‘waliowachochea vijana kujiingiza kwenye vurugu’.
Aidha, tamko hilo limehimiza serikali kuzingatia suluhu na maridhiano pale inapobidi, kwa maslahi mapana ya taifa. Hata hivyo, viongozi hao wameonya kuwa maridhiano yasitumike kama zawadi kwa watu waliotenda uhalifu, wakisema vitendo vya namna hiyo havipaswi kufumbiwa macho.
Aidha viongozi wa Kiislamu hao wamempongeza Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ushindi wa kishindo wa uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka mitano ijayo huku wakimtakia heri katika utekelezaji wa majukumu yake.
View attachment 3501584
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.