Bodi ya Ligi kuu yaahirisha Mechi ya Derby kati ya Yanga dhidi ya Simba

Bodi ya Ligi kuu yaahirisha Mechi ya Derby kati ya Yanga dhidi ya Simba

Watoe taarifa ya nini wakati inajulikana ni matakwa ya kikanuni kufanya mazoezi muda sawa na muda wa mechi siku 1 kabla??
waulize TFF kwa nini unatoa taarifa, kwamba likiwa takwa la kikanuni huti taarifa
 
Ujinga kabisa, timu imevamia uwanja bila taarifa yoyote, na bado inalalamika na kusikilizwa. Tunabaki kuisingizia Yanga, hii Nchi haiwezi kuwa siriasi. Yaani sababu rahisi rahisi tu.
 
Simba hakutoa taarifa na ndio sababu ya kuzuiliwa, Yanga wapeleke timu uwanjani simba wasipokuja malalamiko yafike bodi ya ligi, naamini bodi itarahisisha maamuzi Yanga wakate rufaa kesi ifike juu maana kikanuni mechi haitakiwi kuahirishwa kabla ya masaa 24
 
Waganga uwanjani Kuku na Mbuzi unawapeleka uwanjani usiku?
Waganga gani?

Unayo hiyo video inayoonesha hao waganga?

Kwasababu waandishi wa habari wote walikuwa pale eneo la tukio wakirekodi kila kitu kilichofanyika.

Mtandaoni ndio kuna hayo maneno sijui Simba walikuja na mabasi mawili, nawewe saizi unasema waganga na kuku.

Lakini hakuna uthibitisho wowote wa video inayoonesha hayo unayoyataja.

Kwamba journalists wote waliokuwepo jana wanaipenda sana Simba? Hakuna journalist hata mmoja ambaye anaipenda Yanga ambaye angetuoneshea hayo mambo ambayo mnasema yakikuwepo?
 
Haki umeiongelea wewe... na nimekujibu hiyo hiyo haki wakati mwingine ina utaratibu wa kuipata ingawa ni yako...usijitoe ufahamu! Nb-Mimi ni mpenzi na mshabiki wa Simba SC ila sio mwananchama😁😁😁
Nimezungumzia haki kukusaidia kuelewa ulichouliza. Kama unaelewa taratibu taratibu basi utaelewa baadae
 
Sasa mlitaka simba itoe taarifa gani wakati haki yao ya kisheria ya kutumia uwanja ipo wazi? Watoe taarifa kwani nyie Body ya ligi hamjui kama leo kulikua na mechi?

Masaa mawili yote waliyosimama getini huku wakisubiri muafaka wa kuruhusiwa kuingia uwanjani kwanini hamkutoa maamuzi waruhusiwe ?maana ni haki yao

Simba inatakiwa iendelee kugomea huo mchezo hadi waliozuia wachukuliwe hatua ili iwe funzo kwa wavunja sheria wengine
Hio Kauli ya bodi ya ligi eti kusema "kutoa taarifa" ni hoja ya kipumbavu sana, na wameiweka hio kubalance mambo tu ili wasiwachukize "wakubwa" walio nyuma ya hio timu wahuni wake waliozuia gari kuingia uwanjani..lakin hawajui kua matajiri upande wa pili wamewekeza pesa zao nyingi sana halafu muwafanyie UHUNI huo leo ndio imefika mwisho, mwisho wa siku watu waanze kuheshimiana Sasa.
 
Kanuni haisemi inabidi kutoa taarif maana kwanza ni utaratibu wa kawaida kutumia uwanja siku moja kabla ya mechi, inakuwaje wanachulia kama vile wameshtulizwa?

Haya timu haijatoa taarifa, inakuwaje wakae nje masaa mawili bila muafaka kufikiwa ili timu iingie.

Adhabu za kuvunja kanuni ni ndogo sana ndiyo maana kila siku Yanga haiogopi kuzivunja.
Kwahiyo TFF waongo!? Haya unakwendaje uwanja wa taifa usiku bila taarifa, uliambiwa ule ni uwanja wa fisi!? Kwa utaratibu huo pia inaonekana timu mwenyeji ndio alitakiwa amtayarishie mgeni MAHALA PAZURI PA KULALIA, Ssasa mgeni unakurupuka tu MAJUMBANI MWA WATU hupigi hata simu UTALALA KIBARAZANI😁😁😁
 
Umeisoma vizuri hiyo taarifa? Bodi ya ligi inasema Simba haikuwasiliana na yeyote kuhusu nia yake ya kufanya hayo mazoezi ili wahusika wawaandalie mazingila ya hayo mazoezi kilichopo ni kwamba jamaa walichungulia wakaona leo ni maafa wametafuta sababu
Sasa kwanini wameisogeza mbele?
 
Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha leo Machi 8, 2025, ilipitia shauri la klabu ya Simba kuzuiliwa kuingia kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kwa ajili ya kufanya mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo namba 184 wa Ligi Kuu ya NBC (Young Africans SC vs Simba SC) uliopangwa kufanyika kwenye uwanja huo leo kuanzia saa 1:15 usiku.

Soma Pia: Simba SC yatangaza haitacheza mechi dhidi ya Yanga, Wakidai vitendo visivyo vya kiungwana dhidi yao

Katika shauri hilo, klabu ya Simba iliandika barua kwa Bodi ya Ligi kueleza kususu tukio tajwa hapo juu, huku pia ikieleza nia yao ya kuto shiriki mchezo huo kwa sababu wamezuiliwa kutumia haki yao ya kikanuni kama ilivyoainishwa kwenye Kanuni ya 17:45 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

View attachment 3263593
PARAGRAPH YA NNE
"Baada ya kupitia ........................maandalizi ya kikanuni..."
POROJO ZIMEANZIA HAPO.
 
Mpira umejaa uhuni na upangaji matokeo ndo maana soka linaanguka
 
na hili lililofanywa na simba sc liwe kama mwanzo wa kutokuvunjwa kanuni za michezo kwa lengo la kuibeba/kuiminya timu moja dhidi ya nyingine kisa tu kuna faini ambazo ni himilivu kulipika.

pia karia na tff kwa ukuaji wa mpira wa bongo waache unazi wa usimba na uyanga hauna faida kwa soka letu.

mwisho tff watafute namna ya kuongeza mapato yao badala ya kutegemea simba na yanga zinapokutana wao ndiyo wavune pesa, na kwenye hili simba walishika mpini karia na watu wake kimewaramba.
 
Back
Top Bottom