Bodi ya Ligi kuu yaahirisha Mechi ya Derby kati ya Yanga dhidi ya Simba

Watoe taarifa ya nini wakati inajulikana ni matakwa ya kikanuni kufanya mazoezi muda sawa na muda wa mechi siku 1 kabla??
waulize TFF kwa nini unatoa taarifa, kwamba likiwa takwa la kikanuni huti taarifa
 
Ujinga kabisa, timu imevamia uwanja bila taarifa yoyote, na bado inalalamika na kusikilizwa. Tunabaki kuisingizia Yanga, hii Nchi haiwezi kuwa siriasi. Yaani sababu rahisi rahisi tu.
 
Simba hakutoa taarifa na ndio sababu ya kuzuiliwa, Yanga wapeleke timu uwanjani simba wasipokuja malalamiko yafike bodi ya ligi, naamini bodi itarahisisha maamuzi Yanga wakate rufaa kesi ifike juu maana kikanuni mechi haitakiwi kuahirishwa kabla ya masaa 24
 
mkuu kwamba wewe una akili

yaani TFF mwenye mpira wake na kanuni zake kasema simba hakuwasiliana na mamlaka ili afanyiwe maandalizi

ila wewe mwenye akili unasema haikuwa na sababu

kwa akili hizi huwezi kuwa hata mtaji wa ccm
Sasa mbona hawajaiadhibu hiyo simba.
 
Waganga uwanjani Kuku na Mbuzi unawapeleka uwanjani usiku?
Waganga gani?

Unayo hiyo video inayoonesha hao waganga?

Kwasababu waandishi wa habari wote walikuwa pale eneo la tukio wakirekodi kila kitu kilichofanyika.

Mtandaoni ndio kuna hayo maneno sijui Simba walikuja na mabasi mawili, nawewe saizi unasema waganga na kuku.

Lakini hakuna uthibitisho wowote wa video inayoonesha hayo unayoyataja.

Kwamba journalists wote waliokuwepo jana wanaipenda sana Simba? Hakuna journalist hata mmoja ambaye anaipenda Yanga ambaye angetuoneshea hayo mambo ambayo mnasema yakikuwepo?
 
Haki umeiongelea wewe... na nimekujibu hiyo hiyo haki wakati mwingine ina utaratibu wa kuipata ingawa ni yako...usijitoe ufahamu! Nb-Mimi ni mpenzi na mshabiki wa Simba SC ila sio mwananchama😁😁😁
Nimezungumzia haki kukusaidia kuelewa ulichouliza. Kama unaelewa taratibu taratibu basi utaelewa baadae
 
Hio Kauli ya bodi ya ligi eti kusema "kutoa taarifa" ni hoja ya kipumbavu sana, na wameiweka hio kubalance mambo tu ili wasiwachukize "wakubwa" walio nyuma ya hio timu wahuni wake waliozuia gari kuingia uwanjani..lakin hawajui kua matajiri upande wa pili wamewekeza pesa zao nyingi sana halafu muwafanyie UHUNI huo leo ndio imefika mwisho, mwisho wa siku watu waanze kuheshimiana Sasa.
 
Kwahiyo TFF waongo!? Haya unakwendaje uwanja wa taifa usiku bila taarifa, uliambiwa ule ni uwanja wa fisi!? Kwa utaratibu huo pia inaonekana timu mwenyeji ndio alitakiwa amtayarishie mgeni MAHALA PAZURI PA KULALIA, Ssasa mgeni unakurupuka tu MAJUMBANI MWA WATU hupigi hata simu UTALALA KIBARAZANI😁😁😁
 
Sasa kwanini wameisogeza mbele?
 
PARAGRAPH YA NNE
"Baada ya kupitia ........................maandalizi ya kikanuni..."
POROJO ZIMEANZIA HAPO.
 
Mpira umejaa uhuni na upangaji matokeo ndo maana soka linaanguka
 
na hili lililofanywa na simba sc liwe kama mwanzo wa kutokuvunjwa kanuni za michezo kwa lengo la kuibeba/kuiminya timu moja dhidi ya nyingine kisa tu kuna faini ambazo ni himilivu kulipika.

pia karia na tff kwa ukuaji wa mpira wa bongo waache unazi wa usimba na uyanga hauna faida kwa soka letu.

mwisho tff watafute namna ya kuongeza mapato yao badala ya kutegemea simba na yanga zinapokutana wao ndiyo wavune pesa, na kwenye hili simba walishika mpini karia na watu wake kimewaramba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…